Hili la Maalim Seif kupatikana na maambukizi ya COVID19 linatia ukakasi. Ni aibu kubwa kwa Serikali yetu

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Kwanza kabisa limewashtua watu wengi sababu kwa mujibu wa muongozo wa utoaji taarifa ni Rais,Waziri Mkuu au Waziri wa Afya, kwanini hawajatupa taarifa kuwa kuna maabukizi ya Covid 19 hapa nchini?

Ok fine, kama kiongozi wa Serikali ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar amepata Covid 19,je muuza vitumbua huko forodhani Zanzibar? Je, haiwezi kuwa imeshavuka mpaka Dar es Salaam maana kuna muingiliano mkubwa wa watu kati ya Zanzibar na Dar es salaam.

Kwanini Serikali ya Rais Magufuli haitaki kutupa ukweli kuwa kuna maambukizi ya Covid 19? Mnataka yaliyotokea Brazil yatokee hapa Tanzania? Maana kama kuna maambukizi kwanini tusiambiwe ukweli ili tuchukue tahadhali kwa hali ya juu?

Watanzania tuchukue hatua kujilinda maana tutapukukutika kama njugu. Maana kama viongozi wakubwa wanapata maambukizi halafu Serikali inafanya siri,je sisi makabwela tukipata maambukizi tutaweza kutoboa?
 
Hapo lazima dunia nzima itatushangaa na kutuona sisi ni watu wa ajabu kuwahi kutokea tangu kuumbwa kwa dunia kwani ni juzi tu tulikuwa tunaibeza Chanjo ya corona kwa kutangaza kuwa tupo salama na hatuna Korona kabisa alafu leo Hii Makamu wa Rais anakutwa na virusi vya korona
. Ni aibu ya mwaka
 
Ukiona inadanganya kwenye taarifa hata zisizo na sababu ya kudanganya, basi utakuwa mwendawazimu kuamini hizo nyingine.
Kumbuka mimi sio wa kukurupuka lazima ni digest. Kwa hiyo sidhani kuwa ni mtu wa kudanganywa.
 
Hata wewe!?

Chagu wa Malunde, are you serious?

Serekali ya Magu huwa haikosei bana, acha kuanza kutumika na wewe.

Hivi wewe tangu mwanzo uliamini kuwa Tanzania hamna Corona?
Nawashangaa mpaka sasa wanaojaribu kuishawishi serikali ikiri uwepo wa Corona nchini. Ilishagoma imegoma, kilichobaki ni kuchukua tahadhari binafsi na familia zetu na kufuata taratibu zote za kujikinga na hili dubwana
 
Nawashangaa mpaka sasa wanaojaribu kuishawishi serikali ikiri uwepo wa Corona nchini. Ilishagoma imegoma, kilichobaki ni kuchukua tahadhari binafsi na familia zetu na kufuata taratibu zote za kujikinga na hili dubwana
Kumbuka hii kitu inasambaa vibaya,je tuna vifaa na wahudumu wa kutosha kukabiliana nayo?
 
Back
Top Bottom