sijajua kama kuna nini ambacho unataka kuilaumu serikali. Hebu fanya utafiti ili uongee vitu ambavyo ukuleata tutakuelewa, unajua ugonjwa wa sukari umeuwa watu wangapi hadi sasa kwa kupitia dawa za kitaalam? Je ukimwi? Je kansa? Na mengine mengi, unajua madhara ya dawa za kitaalamu? Au we unakunywa na kulala tu, unataka nani aje atuthibitishie usalama wa dawa ya babu kama soyo wataalamu tulionao? Huu ni ushamba; acheni babu aponye magonjwa sugu, kama una hospitali au mladi uliyotegemea kuwavuna wa tz masikini kwa dawa zisizoponyesha shauri yako hapo imekula kwako. Krolokwini unayosema iligundulika eti inasumu, we ni muongo mkubwa, utafiti unasema iligundulika kuishiwa nguvu za kuua wadudu wa maralia. Nadhani kunahaja ukanywe dawa loliondo itasaidia uwena maamuzi sahihi.
Ni miezi kadhaa sasa tangu jina la Loliondo lilipojipatia umaarufu mkubwa Afrika ya mashariki.Kwa kadiri ninavyoelewa mimi,uganga wa kienyeji ni kitu cha kurithi katika ukoo. Japo babu,baba na wewe hamkuwa waganga lakini kama kuna uganga kwenye ukoo unaweza ukawaruka wote hao ukaja tokea kwa mjukuu wako bila kujali nafasi yake katika dini,elimu na jamii kwa ujumla.
Endapo mizimu hii ya uganga itamtaka awe mganga wakati yeye tayari ni padre,mchungaji shehe ua imamu na akaanza kutenda miujiza nani anaweza kuwashawishi watu kuwa miujiza ile haitoki kwa mungu wakati muhusika yuko katika nafasi fulani ya dini? au kuanza kufuatilia background ya mtu huyu kwa kinaga ubaga?Au watu wanakurupuka tu na kufanya mambo kwa ushabiki bila kujua mafanikio au madhara ya kufanya hivyo?
Kwa wale wenzangu na mimi niwaulize chloroquine iliyokuwa dawa maarufu ya malaria ilitumika kwa miaka mingapi na baadaye kuja kugundulika kuwa ina madhara kwenye mwili wa binadamu? Kwa nini serikali ikurupuke na kuanza kusema dawa imepimwa na TFDA haina tatizo hivi badae ikagundulika ina tatizo serikali itaficha wapi uso wake?
Sawa ni suala la imani lakini tusikurupuke.
Mambo ya babu yaacheni hivi hivi, kila mtu ana imani yake. Mimi simwamini hata kwa mtutu wa bunduki, I will choose death. Ila wengine wenye imani yao ebu tuwape nafasi wewe usiyeamini kimyaaaaaaaa!! watu wakali kweli ukianza kumcrush babu.
Blessing to you all! have a wonderfu saturday
Ni serikali ya CCM. Hapo hapana ubishi!Serikali gani hii inafanya maamuzi kwa maneno ya kusikia yasiyo na uthibitisho?
Hivi maposema kukurupukia hiyo tiba mna maana gani hasa? Mna maana mpaka taarifa ipelekwe WHO na tuelezwe kuwa tuanze matibabu au?
Au ina maana hamfahamu kuwa miti shamba nazo ni dawa? Hivi mtu akikuambia twanga tangawizi ,kamua maji yake kisha changanya na kijiko kimoja cha asali mbichi halafu kunywa utapona kikohozi , huyu naye ni mgamga wa kienyeji? Mganga wa kienyeji ni yupi hasa, maana hata Hospitali tunashauriwa kula mchicha ili kuongeza damu.Katika Biblia Yesu alikoroga tope akampaka kipofu na akapata kuona. Hii nayo ni tiba ipi?
Mkuu well said,
Unajua waafrika ni wajinga sana. Tiba hii ingetolewa na Sheikh wa Kiarabu, au Mzungu wa Roma wangeiita inatoka kwa Mungu. Lakini kwa kuwa ni ya mtu mweusi watamponda hadi basi. Ndo laana hiyo, tumekuwa watumwa wa Ukristo na Uislamu, vyote ambavyo ni tamaduni tu za wenzetu na hakuna u Mungu wowote kwenye hizo dini. Ila kwa kuwa ni za watu weupe, ah ! Tunajidharau halafu tunalaumu wazungu kwamba wanatudharau. Aibu sana!
Huyu naye anaitwa NyumbuUnajua waafrika ni wajinga sana...
Mwenye shida haralamiki ni kujaribu
Wewe hujapata shida na ndio unaandika yote haya
Omba Mubgu yasikukute
Hi waganga wa kienyeji wale wanaojiita maprofesa na madokta hasa kule jangwani (dar) wana leseni ya kufanya hizo shughuli? Ni lini serikali ilithibitisha wanauwezo wakutibu magonjwa sugu kama inavyoonekana kwenye matangazo yao?
Wakuu, uiko hivi, mnaompiga vita babu:
1. Hamuugui kisukari, cancer, ukimwi wala hamna ndugu wanaosumbuliwa na magonjwa hayo au,
2. Mko kwenye ileeee miradi ya ukimwi ... watu wakipata tiba si miradi itakufa? au,
3. Mnamiliki makanisha kama yale ya kina nabii ambayo ustawi wake unategemea sana waumini wenye matatizo.
Ushauri wangu, kabla hamjaanza vita dhidi ya babu, anzisheni ya wangango wa kienyeji wale wapiga ramli kwanza.