Hili la kwenye risiti za kulipa Kodi ya kuegesha magari Dar linanitatiza

Daddo

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
1,433
1,019
Wakubwa hili jambo limekuwa likinitafakarisha sana. Kuna baadhi ya maeneo hapa katika jiji la Makonda ukipaki chombo cha moto unaona anakuja mtu anakuwekea risiti kwenye Wiper.

Hilo kwangu halina tatizo, shida ni kile kilichoandikwa kwenye risiti. Kuna sentensi kama PARK AT YOUR OWN RISK na nyingine inasema STAKABADHI HII NI HALALI KWA FEDHA ILIYOLIPWA.

Hii inakuwaje? Kwamba pesa nalipa inachukuliwa lakini nikikuta shida kwenye chombo nisiulize Wala tusijuane na aliyenilipisha?

Nimeambatisha picha hapo ili muweze kuelewa ninachozungumzia.View attachment 1331169
IMG_20200122_205325_3.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mambo ya ajabu sana nchi hii, parking zipo mbele ya maeneo ya huduma, unapaki ili uigie ndani kuhudumiwa anakuja mtu kukudai parking fee. Kwa hiyo watu wawe wanaingia na magari yao madukani au kumwona daktari
 
Nashauri, msaidie huyo muajiriwa wa hizo Parking Agency. Mwambie asiweke hiyi risiti, utampa tu hiyo pesa.

Hauwezi kukwepa kwa kuwa wanasiasa wameshaamua hivyo, hakuna maboresho yoyote wanayofanya hata kwenye hizo sehemu, wanachukua tu pesa na kutunisha matumbo yao.

Dawa ni kumpa yule mnyonge, aweze kusafiri, kunununua vocha kwa mangi, mzunguko wa pesa ukue kuliko kuwapa hao ambao, hawataboresha huduma na wataishia kuficha pesa nje ya nchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom