Hili la kuwa na Halmashauri mbili(2)ndani ya Wilaya moja limekaa vibaya

mweongo

Member
Aug 23, 2010
62
228
Raisi Magufuli aliagiza Halimashari za vijijini kuhama kutoka makao makuu ya Wilayana kwenda nje ya miji. Na leo nimeona Majaliwa akisisitiza hilo.

Kwa mtazamo wangu naona jambo hili halikutazamwa kwa mapana na marefu kujua umuhimu wake na adhari zake kwa watu wa Wilaya husika. Mfano, huduma nyingi za kijamii hupatikana makao makuu ya Wilaya, hata njia nyingi za usafiri zimejengwa kuelekea makao makuu ya Wilaya hizo. Sasa Halimashari za vijijini zinahamishiwa nje ya makao makuu ya wilaya husika ambako hakuna huduma za msingi na wananchi wa maeneo mengine Wilayani ni vigumu kufika huko kupata huduma za msingi. Wakati mwingine wananchi inabidi wapite makao makuu ya Wilaya kwenda upande wa pili kufuata makao makuu ya Halimshauri yao. naona hapa ni kama kuanzisha Wilaya ndani ya Wilaya.

Hata ugawaji wa Majimbo ya uchaguzi naona haufanyiki vizuri. Mfano, Mbunge wa Korogwe mjini ana eneo dogo sana la kuhudumia kasi kwamba ndani ya saa moja anaweza kutembelea eneo lake lote. Lakini Mbunge wa Korogwe vijijini inaweza kumchukua mwezi mzima kutembelea kata na vijiji vyake. Nashashauri kungekuwa na tume ya kuunda mipaka au Bunge litumike wakati wa kuunda maeneo ya kiutawela. kuliko ilivyo sasa ambapo Magu akisema inakuwa hivyo.
 
Mfano ni Nzega DC.

Sijui kama hiyo halmashauri imehama kwenye majengo ya shule ya secondary.
 
Uyui DC na Mbeya DC zinashida zaidi maaana zina Umbile la Upinde yaani hazieleweki kati kati ni wapi
 
Hiyo. Ni kawaida ..ili kurahisisha utawala ....MFANO WILAYA YA RUNGWE INA HALMASHAURI MBILI .......YA RUNGWE NA. BUSOKELO ......PIA INA WABUNGE WAWILI ....NDANI YA WILAYA MOJA ....ILA HALMASHAUR 2
 
Raisi Magufuli aliagiza Halimashari za vijijini kuhama kutoka makao makuu ya Wilayana kwenda nje ya miji. Na leo nimeona Majaliwa akisisitiza hilo.

Kwa mtazamo wangu naona jambo hili halikutazamwa kwa mapana na marefu kujua umuhimu wake na adhari zake kwa watu wa Wilaya husika. Mfano, huduma nyingi za kijamii hupatikana makao makuu ya Wilaya, hata njia nyingi za usafiri zimejengwa kuelekea makao makuu ya Wilaya hizo. Sasa Halimashari za vijijini zinahamishiwa nje ya makao makuu ya wilaya husika ambako hakuna huduma za msingi na wananchi wa maeneo mengine Wilayani ni vigumu kufika huko kupata huduma za msingi. Wakati mwingine wananchi inabidi wapite makao makuu ya Wilaya kwenda upande wa pili kufuata makao makuu ya Halimshauri yao. naona hapa ni kama kuanzisha Wilaya ndani ya Wilaya.

Hata ugawaji wa Majimbo ya uchaguzi naona haufanyiki vizuri. Mfano, Mbunge wa Korogwe mjini ana eneo dogo sana la kuhudumia kasi kwamba ndani ya saa moja anaweza kutembelea eneo lake lote. Lakini Mbunge wa Korogwe vijijini inaweza kumchukua mwezi mzima kutembelea kata na vijiji vyake. Nashashauri kungekuwa na tume ya kuunda mipaka au Bunge litumike wakati wa kuunda maeneo ya kiutawela. kuliko ilivyo sasa ambapo Magu akisema inakuwa hivyo.
Hiyo ni mbaya sana hata King Msukuma auliza swali bungeni
Via
 
Tunahitaji katiba bora tuongozwe na taasis na mifumo imara.Hili la kutegemea mwanadamu kaamkaje ni aibu na fedheha zama hizi.
 
Back
Top Bottom