Hili la kuugawa mkoa wa Mbeya! Jamani kweli kuna umuhimu huo hivi sasa?

SULEIMAN ABEID

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
390
385
Hatimaye Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametangaza rasmi kuwa Makao makuu ya Mkoa Mpya wa Songwe uliopendekezwa kuundwa kutoka sehemu ya Mkoa wa Mbeya sasa yatakuwa wilaya ya Mbozi

Akihutubia kwenye mkutano wa habadhara alioufanya jioni hii katika viwanja vya Vwawa Mbozi, Pinda amesema kinachoenda kufanyika sasa ni kuigawa wilaya ya Chunya ili sehemu ya wilaya hiyo kubakia mkoa wa Mbeya na sehemu nyingine kuunda wilaya mpya itakayoungana na wilaya za Mbozi, Ileje na Momba ili kuunda mkoa wa Songwe.

Hatua hiyo imepokelewa kwa furaha na wananchi wa Mbozi kutokana na mvutano wa muda mrefu wa wapi mkoa huo utakuwa makao makuu, hatua ambayo wakati fulani baadhi ya wilaya zilitishia kupiga kura za maruhani katika chaguzi zijazo
Ameagiza wilaya ya Mbozi kutenga eneo ambalo litakuwa makao makuu ya mkoa huo ili kurahisisha wakati wa kutekeleza hatua ya ujenzi wa mkoa, aidha ameitaka wilaya ya mbozi kuanza mchakato wa kuigawa halmashauri ya Mbozi ili kupata halmashauri nyingine kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wananchi ambayo inakaribia 500,000

Amesema wilaya hiyo ki eneo, ina kilometa za mraba 3400 ambazo hazitosherezi kuigawa wilaya kuwa mbili na badala yake idadi ya watu ndiyo inayoibeba wilaya hiyo hivyo ili kuruhusu ugawaji ni vyema wakaangalia uwezekano wa kuomba halmashauri nyingine kusogeza huduma kwa wananchi. :msela:
 
Sipati picha ya mkoa unaoitwa Songwe utakuwaje?
Unatokea mkoa gani "sisi ni wakazi wa mkoa wa Songwe" Uwiiii.......!
 
Hongera. Ilikuwa proposed Mkoa mpya wenye makao makuu Tukuyu, wazo likapigwa chini na Mkuu wa mkoa ati wanyakyusa hawatatawalika wakiwa peke yao mkoa mzima ingawa proposal ilikuwa na logic kubwa kwa uwingi wa watu na pia shughurli zao za kimaendeleo. Walishatenga na ofisi ya mkoa mpya. Eneo lake lingekuwa ni pamoja na wilaya yote ya Rungwe, Wilaya yote ya Kyela, Sehemu ya wilaya ya Mbeya vijijini, Sehemu ya Wilaya ya Ileje na sehemu ya Wilaya ya Makete ambao huduma zao karibia zote wanapata kutoka wilaya ya Busokelo/Rungwe. Bahati mbaya maeneo yote hayo ni wanyakyusa tupu. Mtani wao mnyalukolo akasema swalo na ikawa asuhi ikawa jioni. Suala likazimika.
 
Tunachoangalia hapa ni mzigo kwa mlipa kodi wa nchi hii!!! Tusipokuwa makini rais ajaye naye atagawa hata tarafa na kuzifanya wilaya! Imefika watanzania tuseme basi inatosha!!!! Mbona nchi jirani hatusikii utaratibu huu! Kwani huko hawazaani na kuongezeka???
 
Mbona kila kipindi tunagawa mikoa, kwa nini tusiigawe kabisa hii nchi tupate walau nchi mbili au tatu ili tuweze tawalika kirahisi?
Hahaaaaa
 
Mbona kila kipindi tunagawa mikoa, kwa nini tusiigawe kabisa hii nchi tupate walau nchi mbili au tatu ili tuweze tawalika kirahisi?
Hahaaaaa

Word.
Hata mimi nawaza vivyo hivyo.
Kama serokali imezidiwa na jiografia na idadi ya wananchi wake, basi na tuitishe ipendekeze tu maeneo yaliyo tayaro yakajianzishie nchi na kujitafutia.
 
Waziri mkuu kwa uamziwake wa kuigawa wilaya ya chunya amefanya la maana sana maana wilaya ya chunya haielezek kwa mapana yake na marefu ukisikia sehemu inaitwa KAMBIKATOTO, SOME ,NGWALA, BINTI MANYANGA .ukapelekwa huko utahisi kama umetengwa na dunia lakini waziri mkuu na weza sema kuna watu watazaliwa kambikatoto ,watazaliwa some .watakuwa na kuzeeka bila ku uona ama kufika katika mkoa huo wa SONGWE sababu kubwa zikiwa ni umbali ,kutokuwepo kwa miundombinu mizuri nayo ikiwa ni barabara hata vyombo vya usafiri huko hakuendeki WAZIRI MKUU tumeona hata mwenyewe uki ishia tu MKWAJUNI ,SAZA,MAKONGOLOSI N.K na sehem hizo ndizo zenye barabara angalau japo nazo huwezi sema ni barabara ukitazama zime jaa mashimo mawe na wachimba madini wakidhid kuongeza mashimo pembezoni mwa barabara na hata ndani ya barabara. HOJA YANGU AMA PENDEKEZO LANGU mh waziri mkuu kabla ya kutangaza kuigawa wilaya ya chunya pamoja na kutuhaidi mkoa mpya wa SONGWE ungeweza kuji lizisha na maendeleo ya wilaya zote zitakazo unda mkoa mpya.
 
Kila kitu ni siasa na siasa ni kila kitu. Ajabu zaidi Mulugo alitaka makao makuu yawe Mkwajuni.
 
Hii mikowa wanayo igawa je serikali imepanga kuiyendelez mimi naona hawapo sahihi. kipind tuna mikowa 24 serikali imeshindwa kuihudumia, sasa hii wanayo iyongeza itaendelezwaje kiuchumi?
kiukweli wameshindwa kugundua mbinu mpya za kuongoza mikowa
 
Tanzania SIASA ndiyo inayotumikia UCHUMI

Kwa wenzetu wenye AKILI UCHUMI ndiyo unaotumikia SIASA.

Sisi tusiokuwa na AKILI ambao tumeamua SIASA itumikie uchumi ni sawa na Binadamu kujaribu kutembelea kichwa miguu juu. Wakati dunia nzima na watoto wanajua kiungo cha kutembelea ni MIGUU sio KICHWA.

Swali kuu la kumuuliza Pinda, Je wanazo resources (UCHUMI) wa kujenga infrastructures ili Mkoa wa Songwe ufanane kweli na mkoa.

Kama huelewi ninachoongea jaribu kuangalia hiyo mikoa mipya walioianzisha, Simiyu, Geita, Katavi, Njombe etc. Utachoka mwenyewe! hata Wilaya za mkoloni zina afadhari items of infrastructures. Ila mikoa hiyo yote mipya ina viongozi wote wa ki-utawala wa mkoa i.e. Siasa kutumikia Uchumi!
 
Hivi kwanini hawagawi Dar es Salaam? Maana hapo wangeweza kupata mikoa kama sita au saba hivi. Mfano Mkoa wa Mbagala. Mkoa wa Ilala, Mkoa wa Temeke, Mkoa wa Kinondoni, Mkoa wa Kimara, Mkoa wa Kigamboni nk
 
mi sina cha kusema ila ukiniambia chunya yenye wananchi 300,000 na eneo la 29,000km square sawa na na rwanda yenye wananchi 11,000,000 na eneo la 24,000km square lgawanywe ntakubaliana nawe. chunya ni kubwa mno.
 
Back
Top Bottom