Hili la kustaafu, Ni sahihi watanzania wenzangu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili la kustaafu, Ni sahihi watanzania wenzangu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwamola, Jul 6, 2012.

 1. m

  mwamola Senior Member

  #1
  Jul 6, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa sasa kumezuka mtindo ambao watu fulani wanatakiwa kustaafu ama muda unafika wa kustaafu kwa kuwa anastaafu akiwa anaongoza idara ama taasisi fulani unasikia kapewa likizo ya kustaafu ya siku kumi hadi kumi na nne na wakati huohuo tayari kashapewa mkataba hata hajachukua likizo ya kustaafu.

  Kibaya zaidi anapewa mkataba nafasi yake ya ukuu wa idara ama mkuu wa chuo anaendelea nayo bila hata kutangazwa kuwa wazi. Nilimsikia Waziri Kombani katika mahimisho yake akisema haya yanatokea pale mtumishi anaestaafu kuwa anahitajika na taifa ama watu wa taasisi ile. Swali ni je mnatumia kigezo gani kusema anahitajika na watu wa sehemu husika wakati hata huo mkataba anasainishwa kisirisiri? Ama kustaafu nakupisha ofisi kutawakuta walimu wa shule za msingi na sekondari tu na kuwaacha principals wa colleges mbalimbali nchini tena za umma wakipata mikataba hiyo chinichini? Hiyo uihitajikao wao mnaupimia wapi?

  Wadau nisaidie na labda mtakuwa mmelisaidia taifa hili lenye taasisi nyingi na nyingi pia zikiongozwa na wastaafu
   
 2. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hapo Bongo kuna maduka ya silaha??? Kama hakuna nunueni hata gobole kila mtu, halafu muanze kuwadungua hao mafisadi wa ajira mmojammoja! Serikali ya dhaifu ilishachanganyikiwa haijui cha kufanya zaidi ya kuzidi kujichanganya.
   
 3. M

  Magimbi JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 1,069
  Likes Received: 517
  Trophy Points: 280
  NA wakifa wataenda kuwapa Mikataba huko kuzimu waendelee na kazi!! Nini maana ya succession plan? Maana hapo ni kama kutegemea mtu mmoja tu bila kuwaandaa wengine..akiondoka maishani sijui nani atakuwa mkuu hapo..lazima kuwepo na watu ambao watakuwa tayari na najua wapo tatizo ni ni kujuana na kubabena kama serikali ilivyozoea..wastaaafu wanatakiwa kupunzika vijana waendeleze nchi...........
   
 4. HOMOSAPIEN

  HOMOSAPIEN JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 719
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  mwamola Hizi ni janja zao tu,viti vyao vina manufaa binafsi sio nchi,je?ikiwa Israeli kachukua roho yake ina maana taasisi itkakufa?.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...