Uchaguzi 2020 Hili la kurudia kupiga kura ukikosea na Vitambulisho Mbadala, kwanini uchaguzi huu?

residentura

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
7,020
9,609
Tume imeruhusu vitu viwili vya ajabu.
Mosi ni kuruhusu watu kutumia vitambulisho mbadala (Pasi ya kusafiria na leseni ya udereva).
Pili ni kuruhusu mpiga kura kurudia kupiga tena kura iwapo alikosea.
Je,huu sio mwanya wa "ushindi wa kishindo"!?

Hii ya kuruhusu vitambulisho mbadala nakubaliana nalo,lakini kwa nini huu uamuzi uje wakati huu?
Hili la kurudia kupiga kura,hapana kwa kweli.
Kukosea kupi kunaruhusiwa kurudia?
 
Mh Kuna ya kurudia ukikosea kweli.
Kama hiyo ipo haijakaa sawa. Maana hapo zikiharibiwa zilizokosewa. Kuna uhakikia gani hakutakua na njama za kujaribu za mgombea Fulani na kuhesabiwa Kama zilizokosewa.

Au je Kama mtu akipiga Mara mbili au zaidi kwa kisingizio Cha kukosea Kisha kujumlishiwa kwa mchaguzi wake?

Utaratibu wa hizo rejects umekaaje?

Idadi ya Kura iwe moja kwa mmoja. Suluhisho la kukosea liwe elimu ya upigaji kura kabla ya kupiga.

"Kama kweli Kuna hiyo yakurudia" kwa mtu mmoja.
 
Binafsi hayo yote sikubaliani nayo... Kitambulisho cha mpiga kura ndicho pekee chenye sifa yakutumiwa na mpiga kura..

Hili lakukosewa na kurudia ndio wizi wa mchana kabisa, kwasababu moja ya hoja zao za kwanini watu wasipige kura walipo hasa ya uRais ni kwamba idadi ya karatasi vituoni inapelekwa kulingana na idadi ya waliojiandikisha.

Sasa watajuaje wangapi watakosea ili katika idadi waongeze za ziada.

TUSHTUKE?
 
Kura ni ile iliyopigwa na kudumbukizwa kwenye sanduku la kura baada ya hapo hakuna kiachoweza kusahihishwa wala kurudiwa.

nadhani tume imetoa nafasi kwa mpiga kura akigundua amekosea aombe karatasi nyingine ili aanze upya- cha kuangalia ni mawakala kuhakikisha hiyo karatasi inachanwa basi. MKUU USIWE MUUGA WA KUSHINDWA MAANA MTASHINDWA TU
 
Kwamba idadi ya karatasi vituoni inapelekwa kulingana na idadi ya waliojiandikisha.

Mkuu hili hapana siyo kweli ni uongo na uzushi
 
Tume imeruhusu vitu viwili vya ajabu.
Mosi ni kuruhusu watu kutumia vitambulisho mbadala (Pasi ya kusafiria na leseni ya udereva).
Pili ni kuruhusu mpiga kura kurudia kupiga tena kura iwapo alikosea.
Je,huu sio mwanya wa "ushindi wa kishindo"!?

Hii ya kuruhusu vitambulisho mbadala nakubaliana nalo,lakini kwa nini huu uamuzi uje wakati huu?
Hili la kurudia kupiga kura,hapana kwa kweli.
Kukosea kupi kunaruhusiwa kurudia?

NEC wakishirikiana na CCM wamepima upepo wanaona kimbunga Cha Lissu hakizuiliki!
Wanachofanya hivi sasa ni KUTAFUTA UCHOCHORO WA KUHALALISHA KURA ZA WIZI KWA AJILI YA CCM!!
Chaguzi zote kuna kura ZILIZO HARIBIKA.....Je, Tume wanataka kusema safari hii hakuna kura zitakazo HARIBIKA?
 
Kura ni ile iliyopigwa na kudumbukizwa kwenye sanduku la kura baada ya hapo hakuna kiachoweza kusahihishwa wala kurudiwa.
nadhani tume imetoa nafasi kwa mpiga kura akigundua amekosea aombe karatasi nyingine ili aanze upya- cha kuangalia ni mawakala kuhakikisha hiyo karatasi inachanwa basi. MKUU USIWE MUUGA WA KUSHINDWA MAANA MTASHINDWA TU
Unajua mana ya idadi ya karatasi za kura zinazopelekwa kituoni hutokana na idadi ya wapiga kura kwenye kituo husika!?
Kitu A kina wapiga kura 100,watapeleka karatasi ngapi za kupigia kura? Watatumia kanuni ipi?
 
Kura ni ile iliyopigwa na kudumbukizwa kwenye sanduku la kura baada ya hapo hakuna kiachoweza kusahihishwa wala kurudiwa.
nadhani tume imetoa nafasi kwa mpiga kura akigundua amekosea aombe karatasi nyingine ili aanze upya- cha kuangalia ni mawakala kuhakikisha hiyo karatasi inachanwa basi. MKUU USIWE MUUGA WA KUSHINDWA MAANA MTASHINDWA TU
Tatizo hapa ni kuwa Tume ya Uchaguzi ilisema itapeleka kila kituo idadi ya karatasi sawa na idadi ya wapiga kura. Sasa je msimamizi atapata wapi karatasi za ziada kwa watakao kosea kupiga kura?
 
That's the main point.
Hilo ndio suala la msingi.
 
Kuna baadhi ya watu hapa tz ni wajinga waliopitiliza zamani mlikuwa mnasema serikali na tume kwa nini wasiruhusu watu kupiga kura hata kama wana passport au kitambulisho cha NIDA.

Wakaenda mbali na kusema bado tupo nyuma, nchi za wenzetu wanapiga kura hata kwa passport tu. Maneno yakawa mengi
Haya mwaka huu tume imewasikiliza na kufanyia kazi
 
Kura ni ile iliyopigwa na kudumbukizwa kwenye sanduku la kura baada ya hapo hakuna kiachoweza kusahihishwa wala kurudiwa.

nadhani tume imetoa nafasi kwa mpiga kura akigundua amekosea aombe karatasi nyingine ili aanze upya- cha kuangalia ni mawakala kuhakikisha hiyo karatasi inachanwa basi. MKUU USIWE MUUGA WA KUSHINDWA MAANA MTASHINDWA TU
Ugonjwa alionao mleta mada ni hatari sana! Kuona uovu katika kila jambo....tatizo la ugonjwa huu haliishii kwenye siasa hata masomo, chakula, jamii unayoishi nayo, nk!
 
Back
Top Bottom