SHILINDE
Member
- Jul 23, 2010
- 14
- 6
Taifa lolote duniani linapopatwa na majanga na dharula serikali yake inapaswa kusimamia kifua mbele. Tanzania tumepatwa na ugonjwa wa Dengue ambapo serikali katika kutimiza jukumu lake la kukinga na kuzuia maambukizi yasiwapate watanzania ikabidi kuamuru mabasi yote yanayoenda mikoani kupuliziwa dawa ya kinga (fumigation) sasa kinachotokea ni kutupiana mpira kati ya serikali na wamiliki wa vyombo vya usafiri juu ya gharama za dawa hizo.
Busara ndogo na sahihi hapa ni kwamba Serikali iwajibike na ichukuwe jukumu hilo na si kuwabambika wamiliki wa mabasi kwa sababu kubwa zifuatazo,
1. ni jukumu la serikali kuzuia/kukinga wananchi wake kwenye majanga
2. wamiliki wa mabasi hawahusiki katika kupelekea/kuzalisha mbu wanaoambukiza dengue, ingepasa waombwe na si kuamuriwa kama ilivyo sasa
Natoa hoja.

Iko hivi: wamiliki wa mabasi yanayotoa huduma za usafiri DSM walikutana na mkuu wa mkoa wa Dsm pamoja na SUMATRA na wakakubaliana kwamba wafanye fumigation ndani ya mabasi hayo kwa hiyari.
Leo, Afisa Mfawaidhi wa Sumatra kanda ya Mashariki Condrad Shio amesema kwamba mpaka kufika jana saa mbili na robo usiku, takribani mabasi 580 Yamekwisha puliziwa dawa hizo za homa ya dengi.
Na si mabasi yote yaendayo mikoani yatahusika na zoezi hilo..La Hasha! bali ni mabasi yatoayo huduma kwa mikoa ya Dsm, Morogoro, Lindi na Mtwara..Zoezi lote hadi hivi sasa Serikali inaligharimia na wala si kweli kwamba kuna kutupiana mpira!
Sosi-Mimi Mwenyewe!