Habari wadau.
Naangalia kituo cha Televisheni cha Clouds TV kuna kipindi kinarushwa Live ambacho ni mkutano
wa Mkoa wa dar es salaam Ndugu Paul Makonda na wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam Wilaya ya kinondoni kata ya Tandale kwa Tumbo.
Nimefurahi kuona wananchi wanapata fursa ya kutoa kero zao na wengine kutoa ushauri. Na baadhi ya malamiko yanatolewa majibu kutoka kwa wahusika wa ngazi mbalimbali.
Sehemu kubwa majibu yake yanapatikana ambayo kwa muda mrefu hayakuwa yanapata majibu aidha kwa kwa uzembe au kuna harufu ya rushwa.
Ni jambo zuri na la kuigwa. Aina hii ya kuonana na wananchi moja kwa moja na kusikiliza kero zao ni jambo zuri na linalovunja wigo wa viongozi wajanja wanaotengeneza ugumu wa kuwasaidia wananchi katika kupata haki zao wanazodhulumiwa na wenye pesa.
Kesi mbili za malalamiko ya ardhi nimeona zimepata ufumbuzi kutoka kwa wahusika ambao katika wakati wote hawakuweza kutoa haki kwa wahusika.
Ni jambo la kumpongeza mkuu wa mkoa kwa kazi nzuri anayoifanya. Kwa hili namuunga mkono
aendelee kukutana na wananchi kutatua kero zao.