Hili la kumchangia Tundu Lissu linakwama wapi? Kuondoka kwa Lowassa kwatajwa

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu,

Wiki chache zilizopita ilizinduliwa kampeni kabambe ya kumchangia Tundu Lissu kupitia akaunti ya benki na kwenye mitandao ya simu.

Zoezi lilipokelewa kwa hisia kali na makamanda waliotaka wapiga kura milioni sita waliompigia Lowassa wachange kila mmoja angalau shilingi 1000.

Nakumbuka hamasa ilikuwa kubwa kabla Mbowe hajapata dhamana na mara alipotoka jela zoezi likafifia. Je, mkono wa chuma umepita?

Huenda wale wapiga kura milioni sita walikasirishwa na matusi na dhihaka za wafuasi wa Chadema dhidi ya Edward Lowassa na familia yake baada ya kurejea CCM. Ni dalili kuwa wananchi waliompigia kura Lowassa walihuzunika.

Je, hawa makamanda waliobaki mitandaoni aka "keyboard worriors" ni maneno matupu?

Nimetumia vyanzo vyangu kutoka benki husika na wamekiri kuwa hakuna chechote zaidi ya salio la kufungulia akaunti, kwenye mitandao ya simu nako ni ukame huenda ndio sababu Lissu kaamua kupambania hali yake kortini.

Ni dhahiri kishindo cha watu milioni sita kimeondoka kimyakimya, tujifunze kuweka akiba ya maneno.Ikumbukwe kipindi Lissu kapigwa risasi michango ilipatikana fasta bila shaka watu hawa milioni sita wameondoka na Lowassa.

Muda utatujibu, mambo mengi mno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unasemea Lissu yupi? Kama ni Mheshimiwa Tundu Antipasi Lissu the Brightest Parliamentarian in the Bunge of Tanzania, sio kweli. Nina ushahidi wa kuingiziwa fedha pale Azikiwe Branch more than 10M wiki iliyopita.

BTW nasikia hata Spika hatimaye kaachia mshahara wake.
 
Pitia habari hapo chini

 
Tatizo hakuna uhamasishaji,vilevile kuna wanafiki wengi sana makeyboard warriors, si mliona walivyomwacha mange kimambi kwenye keepleft, hadi nae akaamua kuwapotezea
 
Tatizo lenu nikwamba suala lá Lissu mnalichukulia kichuki zaidi hampendi kumuona ni mzima, mnapenda yamfike zaidi ya hayo mliomuanZishia,kufa,kuteseka ikiwa anaishi. Okay tuseme yamemfika hayo.

Mungu humuondoa mja wake kwa mda aliopanga yeye na sio binadamu kupanga kumfisha mtu.

Tufanye vise verse ya hayo ingekuwa ni babayo au mamayo au jamaa wa familia yako jee ungekuwa unakuja na kejeli za na utumbo wa maneno mabovu kama hayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo lenu nikwamba suala lá Lissu mnalichukulia kichuki zaidi hampendi kumuona ni mzima, mnapenda yamfike zaidi ya hayo mliomuanZishia,kufa,kuteseka ikiwa anaishi. Okay tuseme yamemfika hayo.

Mungu humuondoa mja wake kwa mda aliopanga yeye na sio binadamu kupanga kumfisha mtu.


Tufanye vise verse ya hayo ingekuwa ni babayo au mamayo au jamaa WA familia yako jee ungekuwa unakuja na kejeli za na utumbo WA maneno mabovu kama hayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nje ya mada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom