Hili la kukopa pesa IMF/ WB kwa ajili ya Ruzuku ya Mafuta hapana

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,586
14,137
Pamoja na Nia njema ya kuleta unafuu wa bei za mafuta/ petroli lakini njia ya kwenda Kukopa haifai.

Tulikubaliana kama Taifa tutakopa kwa ajili ya miradi ila sio kwa ajili ya kula na mambo kama hayo.

Kwa sasa Tanzania ina nafasi ya kukopesheka na ni fursa ya kuitumia kwa ajili ya kujengea miradi ya kimkakati ya kuchochea uchumi kama Bagamoyo Port,Liganga/ Mchuchuma,Magadi soda Engaruka nk lakini sio Kukopa Ili kulipia mafuta.

Serikali isipende kutafuta njia shortcut ambazo kesho zitaumiza uchumi na maisha ya watu.Nchi nyingi zinaumizwa na mikopo kama Zambia,Kenya,Ghana,Angola,Sri Lanka nk.

Serikali inaweza kabisa kutoa ruzuku kwa kupunguza gharama zake za utawala,kwa kufanya yafuatayo'

1. Kufuta au kupunguza kwa nusu ruzuku za vyama vya siasa.

2. Kuacha kununua Magari ya serikali yanayotumia mafuta mengi kama mashangingi kwa maofisa wake isipokuwa viongozi wa kitaifa tuu.

3. Kupunguza bajeti ya mafuta Kwa viongozi wa serikali maana yanatumika kwa binafsi kuliko kwa Kazi za serikali,na wengine huwa wanaenda kubadilisha kwenye vituo vya mafuta wanapewa pesa wanatafuna.

4. Kubadili mfumo wa magari ya serikali kuwa ya gas au umeme Ili kupunguza au kuacha kutumia mafuta..Hili hata watu binafsi wawekewe hii huduma ila lazima Serikali ionyeshe mfano.

4.Kupunguza au kufuta kabisa ile inayoitwa Mfuko wa Jimbo, yaani serikali inapeleka mabilioni kwenye Mfuko wa Jimbo kwa ajili ya nini hasa?

5. Kupunguza mishahara,marupurupu nk kwa viongozi wote wa juu kuanzia kwa wakuu wa Idara na Taasisi hadi Kwa Rais wakiwemo Wabunge.

6.Kupunguza na kufuta mamikataba yasiyo na tija kwa mfano Ule wa Tanesco na wahindi kwa ajili ya software..

7.Kupunguza Utitiri wa Taasisi za serikali zinazofanya majukumu yanayofanana eg Sido,Tirdo,Temdo,NDC,CAMARTEC,Temesa,Brela,TanTrade,TIC,EPZA,Wakala wa vipimo,TBS,TBA,NHC,Watumishi Housing,Mzinga Corporation,FCC,FCT,NEEC ,kila wizara kuwa na chuo/ vyuo vyake huko kozi zinazofundishwa zipo pia kwenye vyuo vingine nk

7.Kukusanya Kodi stahiki kwa sababu TRA inazembea kukusanya na kubuni vyanzo vipya vya mapato..

Yaani haihitaji Kukopa wala kuondoa Kodi kwenye mafuta au kufuta vyanzo vya maendeleo kama Kodi za Tarura,TanRoads,Fuwasa na Reli..

Tukikomaa na hayo niliyoeleza hapo juu na mengine mtakayoongeza tutaokoa na kupata pesa nyingi sana zaidi ya bil.600 ambayo inaweza kutoa ruzuku walau kwa miezi 5- 7 wakati tunajipanga kwa hatua za mda mrefu.

Wananchi tuungane kupinga na kukataa kuchukua mkopo kwa ajili ya Ruzuku.👇

Screenshot_20220511-085217.png
 
kuna yule kiazi aliyeshauri wananchi kama hawawezi kununua mikate basi wanunue hata keki.

yaani kimsingi hakuelewa hoja iliyopo katika malalamiko hayo,kwamba ni umasikini wa kukosa hela.
tumeililia govnt bei ya mafuta kupaa juu,wanakwenda kukopa ili kuikata,bln 100 itafubaza bei wiki mbili tu.
 
Pamoja na Nia njema ya kuleta unafuu wa bei za mafuta/ petroli lakini njia ya kwenda Kukopa haifai..

Tulikubaliana kama Taifa tutakopa kwa ajili ya miradi ila sio kwa ajili ya kula na mambo kama hayo..

Kwa sasa Tanzania ina nafasi ya kukopesheka na ni fursa ya kuitumia kwa ajili ya kujengea miradi ya kimkakati ya kuchochea uchumi kama Bagamoyo Port,Liganga/ Mchuchuma,Magadi soda Engaruka nk lakini sio Kukopa Ili kulipia mafuta..

Serikali isipende kutafuta njia shortcut ambazo kesho zitaumiza uchumi na maisha ya watu.Nchi nyingi zinaumizwa na mikopo kama Zambia,Kenya,Ghana,Angola,Sri Lanka nk..

Serikali inaweza kabisa kutoa ruzuku kwa kupunguza gharama zake za utawala,kwa kufanya yafuatayo'

1.Kufuta au kupunguza kwa nusu ruzuku za vyama vya siasa.,

2.Kuacha kununua Magari ya serikali yanayotumia mafuta mengi kama mashangingi kwa maofisa wake isipokuwa viongozi wa kitaifa tuu..

3.Kupunguza bajeti ya mafuta Kwa viongozi wa serikali maana yanatumika kwa binafsi kuliko kwa Kazi za serikali,na wengine huwa wanaenda kubadilisha kwenye vituo vya mafuta wanapewa pesa wanatafuna..

4.Kubadili mfumo wa magari ya serikali kuwa ya gas au umeme Ili kupunguza au kuacha kutumia mafuta..Hili hata watu binafsi wawekewe hii huduma ila lazima Serikali ionyeshe mfano..

4.Kupunguza au kufuta kabisa ile inayoitwa Mfuko wa Jimbo, yaani serikali inapeleka mabilioni kwenye Mfuko wa Jimbo kwa ajili ya nini hasa?

5..Kupunguza mishahara,marupurupu nk kwa viongozi wote wa juu kuanzia kwa wakuu wa Idara na Taasisi hadi Kwa Rais wakiwemo Wabunge.

Tukifanya haya na mengine ambayo wadau watapendekeza inaweza patikana Karibu bil.500 ambayo inaweza kutoa ruzuku walau kwa miezi 4 au 5 wakati tunajipanga kwa hatua za mda mrefu..

Wananchi tuungane kupinga na kukataa kuchukua mkopo kwa ajili ya Ruzuku..

View attachment 2220394
Hiyo no.1, CCM hawawezi kukubali. Wao ndio wanachukua 95% ya pesa yote ya ruzuku kwa vyama vya siasa. Kwa ujumla ni ruzuku kwa CCM, siyo kwa vyama vya siasa.
 
Kupinga kukopa bila kukokotoa masharti ya mkopo na riba kwa kulinganisha madhara au faida za kutokopa, ni kujadili mambo kiitikadi bila kuchambua uchumi.

Weka namba hapa uoneshe mkopo wa riba hii na masharti haya haufai kwa sababu ukiingia kwenye uchumi utaleta ufanisi wa kiuchumi mdogo kuliko gharama za kuulipa.

Jenga hoja kwa hesabu, kwa kuangalia masharti ya mkopo, si kwa itikadi kwamba hatutaki kukopa.
 
Tanzania tunawabunge vilaza sana

Bunge linashindwa kujadili mikakati mizuri ya kuweza kupunguza hii kitu ndani ya miaka 10 au 15 ijayo

Linakaa kujadili kukopa fedha kwa ajili ya oil price regulations
Let say hii situation ikakaa 25 years ndo ikaja kutoweka
Je watakopa for 25 years

Tutauzwa na hawa wachumia tumbo walahi

Kwenye kidonda unaweka spirit what happens
 
Kupinga kukopa bila kukokotoa masharti ya mkopo na riba kwa kulinganisha madhara au faida za kutokopa, ni kujadili mambo kiitikadi bila kuchambua uchumi.

Weka namba hapa uoneshe mkopo wa riba hii na masharti haya haufaibkwa sababu ukiingia kwenye uchumi utaleta ufanisi wa kiu humi mdogo kuliko gharama za kuulipa.

Jenga hoja kwa hesabu, kwa kuangalia masharti ya mkopo, si kwa itikadi kwamba hatutaki kukopa.
Wewe nimeshakueleza mambo yanayotakiwa kufanyika,nimesema Kukopa kuwepo kwa ajili ya miradi tuu sio kwa ajili ya kula..

Kwa nini tusipunguze matumizi yasiyo ya lazima? Ruzuku ya vyama vya siasa ndio nini? Utitiri wa mataasisi yanayofanya majukumu yanayofanana wewe unaona ni sawa?
 
Naunga mkono hoja yako

Kukopa kwa ajiri ya mafuta hapana! Je itakuwaje bei ikizidi kupanda? Tutaendelea kukopa?

Hapa zitumike njia mbadala kama hii iliyotumika sasa ya kutoa bil 100. Kukopa ni mzigo sana
Marehemu angekosa kuwavuruga wawekezaji, sahizi tungekuwa na LNG plant. Magari mengi, hasa madogo, yangekuwa yanatumia liquidified gas badala ya petrol. Mapato makubwa toka kwenye gas yangeweza ku-subsidize bei ya diesel. Mtu mmoja akaharibu prospects za Watanzania wote.

Leo tunaanza upya kuwabembeleza wawekezaji ambao tayari tulikuwa nao.

Baada ya kutambua kuwa ameharibu,marehemu, akaanza kuwadanganya wajinga eti gas yetu imeuzwa kwa Wachina. Na majitu majinga yakaanza kushangilia, bila ya kujiuliza hiyo gas imeuzwaje kwa Wachina!!

Nchi hii tatizo kubwa ni kukosa viongozi wenye maono na uwezo. We had agreat leader Nyerere, akaja Mwinyi, akatudondosha, Mkapa alituinua sana toka kwenye lindi la uharibifu wa uchumi, Kikwete alipoingia akatapanya pesa lakini akaweza pia kutafuta pesa, akaja Magufuli akaharibu kabisa. Akaua hata kidogo tulichokuwa tumefanikiwa. Akafukuza wawekezaji wa ndani na wa kimataifa kutokana na uongozi wake mbaya. Sasa tunaye Samia, sijui atatufikisha wapi, lakini kwa vyovyote, she is much better than Magufuli.

Suluhisho ni kuwa na katiba itakayowabana watawala kuliko hii inayompa uhuru Rais kupuyanga kama anavyotaka.
 
kweli kabisa! Endapo Majadiliano na wawekezaji wa Gesi yangeanza pale tulilopitisha Sheria zetu za Mafuta, Gesi na Petrol mwaka 2014 basi leo mradi wetu wa LNG ungekuwa unaanza kutake off na maumivu yasingekuwa makubwa kiasi hiki
 
Wewe nimeshakueleza mambo yanayotakiwa kufanyika,nimesema Kukopa kuwepo kwa ajili ya miradi tuu sio kwa ajili ya kula..

Kwa nini tusipunguze matumizi yasiyo ya lazima? Ruzuku ya vyama vya siasa ndio nini? Utitiri wa mataasisi yanayofanya majukumu yanayofanana wewe unaona ni sawa?

That is a logical non sequitur and a false dichotomy.

Ukichukua mkopo haina maana huwezi kubana matumizi. There is no mutual exclusivity there.

Tukianza kupunguza matumizi leo unajuaje kwamba tutaanza kupata ufanisi mara moja?

Hujaweka namba za kuonesha ubaya wa mkopo, hivyo, unaujadili mkopo kiitikadi na si kiuchumi.
 
Magufuli alikopa Trilioni 30 mkakaa kimya ila hiyo bilioni 100 inawawasha.
Sukuma gang MNA shida sana.
sidhani kama ni kweli bilion 100 ni fedha kidogo sana ukiangalia na ukubwa wa tatizo matajiri wachache wanaweza kukopesha serikali hiyo hela au kwa selikali kuuza bond zake hivyo sio kweli tunadanganyana
 
That is a logical non sequitur and a false dichotomy.

Ukichukua mkopo haina maana huwezi kubana matumizi. There is no mutual exclusivity there.

Tukianza kupunguza matumizi leo unajuaje kwamba tutaanza kupata ufanisi mara moja?

Hujaweka namba za kuonesha ubaya wa mkopo, hivyo, unaujadili mkopo kiitikadi na si kiuchumi.
Hivi wewe uliyekariri makaratasi inakutosha kichwani kweli?

Kwa hiyo ukiunganisha mataasisi hayo kibao huokoi pesa zilizokuwa zimetengwa huko kwa ajili ya administration?

Tarura walikuwa na Meneja kila Halmashauri jumla 184 wakapunguza wakawa na Meneja kila wailaya ikapunguza gharama za utawala kwa 30% ,sasa wewe unaongea nini?

Nyie majitu ya makaratasi huwa ni zero kabisa,mna akili za makaratasi ila IQ zenu ni ndogo Sana.
 
Me nilichoelewa kuwa tunakopa fedha ili iende kugharamia miradi ya maendeleo ambayo ilikuwa financed na tozo mbalimbali za mafuta,that means tunaenda kuondoa hizo tozo kwenye mafuta ili kuleta unafuu na utulivu kwenye bei ya mafuta kwa kukopa pesa kwenye hiyo mifuko ya kifedha ya kimataifa ili ije I-finance miradi ya kimaendeleo ambayo tozo za mafuta ilikuwa ikilipia hizo gharama.The idea here of our government ni kuhakikisha miradi yetu mbalimbali ya kitaida haisimami
Pamoja na Nia njema ya kuleta unafuu wa bei za mafuta/ petroli lakini njia ya kwenda Kukopa haifai.

Tulikubaliana kama Taifa tutakopa kwa ajili ya miradi ila sio kwa ajili ya kula na mambo kama hayo.

Kwa sasa Tanzania ina nafasi ya kukopesheka na ni fursa ya kuitumia kwa ajili ya kujengea miradi ya kimkakati ya kuchochea uchumi kama Bagamoyo Port,Liganga/ Mchuchuma,Magadi soda Engaruka nk lakini sio Kukopa Ili kulipia mafuta.

Serikali isipende kutafuta njia shortcut ambazo kesho zitaumiza uchumi na maisha ya watu.Nchi nyingi zinaumizwa na mikopo kama Zambia,Kenya,Ghana,Angola,Sri Lanka nk.

Serikali inaweza kabisa kutoa ruzuku kwa kupunguza gharama zake za utawala,kwa kufanya yafuatayo'

1. Kufuta au kupunguza kwa nusu ruzuku za vyama vya siasa.

2. Kuacha kununua Magari ya serikali yanayotumia mafuta mengi kama mashangingi kwa maofisa wake isipokuwa viongozi wa kitaifa tuu.

3. Kupunguza bajeti ya mafuta Kwa viongozi wa serikali maana yanatumika kwa binafsi kuliko kwa Kazi za serikali,na wengine huwa wanaenda kubadilisha kwenye vituo vya mafuta wanapewa pesa wanatafuna.

4. Kubadili mfumo wa magari ya serikali kuwa ya gas au umeme Ili kupunguza au kuacha kutumia mafuta..Hili hata watu binafsi wawekewe hii huduma ila lazima Serikali ionyeshe mfano.

4.Kupunguza au kufuta kabisa ile inayoitwa Mfuko wa Jimbo, yaani serikali inapeleka mabilioni kwenye Mfuko wa Jimbo kwa ajili ya nini hasa?

5. Kupunguza mishahara,marupurupu nk kwa viongozi wote wa juu kuanzia kwa wakuu wa Idara na Taasisi hadi Kwa Rais wakiwemo Wabunge.

6.Kupunguza na kufuta mamikataba yasiyo na tija kwa mfano Ule wa Tanesco na wahindi kwa ajili ya software..

7.Kupunguza Utitiri wa Taasisi za serikali zinazofanya majukumu yanayofanana eg Sido,Tirdo,Temdo,NDC,CAMARTEC,Temesa,Brela,TanTrade,TIC,EPZA,Wakala wa vipimo,TBS,TBA,NHC,Watumishi Housing,Mzinga Corporation,FCC,FCT,NEEC ,kila wizara kuwa na chuo/ vyuo vyake huko kozi zinazofundishwa zipo pia kwenye vyuo vingine nk

7.Kukusanya Kodi stahiki kwa sababu TRA inazembea kukusanya na kubuni vyanzo vipya vya mapato..

Yaani haihitaji Kukopa wala kuondoa Kodi kwenye mafuta au kufuta vyanzo vya maendeleo kama Kodi za Tarura,TanRoads,Fuwasa na Reli..

Tukikomaa na hayo niliyoeleza hapo juu na mengine mtakayoongeza tutaokoa na kupata pesa nyingi sana zaidi ya bil.600 ambayo inaweza kutoa ruzuku walau kwa miezi 5- 7 wakati tunajipanga kwa hatua za mda mrefu.

Wananchi tuungane kupinga na kukataa kuchukua mkopo kwa ajili ya Ruzuku.

Me nilichoelewa kuwa tunakopa fedha ili iende kugharamia miradi ya maendeleo ambayo ilikuwa financed na tozo mbalimbali za mafuta,that means tunaenda kuondoa hizo tozo kwenye mafuta ili kuleta unafuu na utulivu kwenye bei ya mafuta kwa kukopa pesa kwenye hiyo mifuko ya kifedha ya kimataifa ili ije I-finance miradi ya kimaendeleo ambayo tozo za mafuta ilikuwa ikilipia hizo gharama.The idea here of our government ni kuhakikisha miradi yetu mbalimbali ya kitaida haisimami
Hili inaeleza Wewe
 
Hebu nitoeni ushamba katika hili, ina maana serikali ikishalipa mishahara huwa haibakiwi na kitu hazina,

sababu karibu Kila wakitaka kufanya kitu wanakopa, lakini ndege tunaambiwa pesa inalipwa yote bila kuacha hata deni la shilingi 100,
Kama Wana jeuri ya kununua ndege cash kwa nini katika hili pia wasitoe cash kumaliza tatizo,

hapo hujakutana na msafara wa mawaziri achilia mbali ule wa raisi magari mengi kupita kiasi
Kuna vitu ambavyo waki vipunguza wanaweza kufanya mengi tuu bila mikopo

Ni mawazo yangu tuu ya kijinga
🚶🚶🚶🚶🚶🚶🚶🚶🚶🚶🚶🚶
 
Back
Top Bottom