Hili la kuchinja lisitugawe, Linazungumzika

Naungana kabisa na mtoa mada,lakini swali langu ni kwamba mi binafsi nawafahamu waislamu wengi tu ambao tunapiga nao kitimoto,sasa hiyo kitimoto inakuwa imechinjwa na nani?Ok sasa tukikubaliana kuwa waislamu ndio pekee wenye haki ya kuchinja,je wako tayari pia kutusaidia kuchinja kitimoto?
 
kwani kuna ubaya gani kila mtu kugawana , mbona nyumba za ibada kila mtu ana yake misikiti kwa waisilamu na makanisa kwa wakiristo, hata kwa sasa tuna halal resturant na haram resturant hakuna shida , tuna mabenki ya kiisilamu na ya kikafiri mbona hilo halipigiwi kelele, nasema hivi hata hili a kuchinja tutakuwa na bucha za halali na bucha za kikafiri
 
ibada zikafanyikie misikitini na makanisani jamani. Mambo ya kulazimishana kushirk ibada za watu wengine si sahihi. Au la mtu asilazimishe kufanyia ibada ya kuchinja kwenye kmoto ya wengine ili tu ale. Afanyie kwenye mbuzi wake. Tuweni wawazi tuache kuendekezana hadi sasa tunazani ni sheria
 
Kwa anayeweza kunikumbusha, kipindi cha loliondo kulikuwa na nini tena kisiasa?
 
mimi nadhani kwa mkristo haijalishi nani kachinja ila inategemea ni maneno gani yananuiziwa wakati wa kuchinja kama yanakwaza au la imani ya kikristo! je waislam wanaweza wakatuambia ni maneno gani (na maana yake) hunuiziwa wakati wa kuchinja ili tuweze ku judge kwa haki?
 
Nafikiri waislamu kwa kuwa hawajaenda shule ndiyo maana wanang'ang'ania kuwa wachinjaji wataifa angalau nao wapate ajira maana kuchinja siyo lazima uende shule. Na kama ndivyo wangekuwa wazi tu waseme kuchinja kunawapa ajira ili sisi wakristo tuwaachie, lakini pamoja na hayo, waende shule wakasome itawasaidia kuwa na hoja zenye mashiko. Taifa lina mambo muhimu sana ya kuzungumzia, siyo suala la kuchinja, kuchinja ni nini
 
pesonally,i really dont see sababu ya kuvimbiana nyuso.
tuna matatizo mengi sana ya kutatua inji hii.
tukianza kulumbana kwa hab'ri za kitoto ivi tutasema mpaka wanaume wasiuze chupi za kike kariakoo basi...

Lets think big and ahead....asiyetaka kula asile kwani kalazimishwa...AAARghhhhhh.!
 
Nimekuwa nikifuatilia sakata la nani achinje nyama kule Mwanza, na nimebaki kushikwa na butwaa.

Jamani, nadhani tumesahau mauwaji ya kimbari kule Rwanda na sisi tunatamani kuchinjana wenyewe kwa wenyewe.

Ni jambo linanishangaza nakutokuelewa mim ni mkristo na sion ubaya wa muislam kuchinja kutokana na utamaduni tumeuzowea kuwa waislam ndio wanachinja na pasipo katiba kusema mahali popote na mimi sioni ubaya.

Jamani mbona haya ni mambo ya tangu miaka mingi na haijawahi kuonekana mtu akilalamika imekuwaje ghafla tunataka kuchinja liwe swala la katiba. Jamani hili ni taifa moja na tu wamoja tusianze kubaguwana kwa udini na ukabila maana hakika hakuna atakaye pona.

Yatupasa kumuomba Mungu na kuishi ktk hali ya umoja na upendo kama taifa moja chini ya Rais mmoja. Tusibaguwane wala viongozi wa dini tusiwe wachochezi na ikiwezekana hao wakristo wakaondoe kesi mahakamani.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake..
 
Wazee wa kupiga mpunga,wamesema mambo yasiishie kwenye bucha tu yaende mbali zaidi kuwe na necta ya waislam etc
 
Tatizo siyo waislam kuchinja ndugu yangu, bali kwao ni ibada sasa wanatulisha vitu vilivyofanyiwa ibada tofauti na misingi ya imani yetu. Hapo ndipo tumepata utata kwamba kumbe kulikuwa na ibada nyuma ya kuchinja huko.
 
Tatizo liko kwa yule mkuu wa mkoa wa mwanza pamoja na Wasira kushindwa kutumia busara kulitatua tatizo hili hadi wakristo kufikia hapo pili wakristo walikuwa hawajui kuwa mwislamu kuchinja ni ibada hivyo hawataki kushiriki ibada hiyo.
 
Nimesikia leo hapa Tunduma kwa waliokua kanisani, kuwa viongozi wa kidini wamewahasisha sana waumini wao kususia nyama mabuchani.Naona hili swala ni bichi sana,tuiombe serikali irekebishe kauli yake hali inazidi kuwa mbaya.!
 
Ibada gani kusema alahuu wakbaru maana yake mungu mkubwa kwani wakristo wanavyo chinja usemaje?tusiwe tuna tafuta sababu za kukosana.miaka nenda rudi waislamu ndio wachinjaji hii mambo ya ccm kutugawa kusema cdm ni chama cha wakristo matokeo yake ndio haya cdm hawataki kuchinjiwa na ccm ambao ndio wanajidai waislamu safi.
 
Nilidhani tunetumia muda mwingi kujadili mambo ya muhimu kama jinsi ya kujenga nchi yetu, kupambana na ufisadi, kuepuka uombaomba na upuuzi mwingine. Kumbe tunapoteza muda kwenye masuala madogo kama nani achinje na nani asichinje! Hao waliotuletea hizo sheria mbona hawakusema hata ng'ombe na mbuzi hata kuku watakaozalishwa na makafir wasiliwe na wenye dini? Mbona ni simpo issue kuwa hawa wanyonyaji waliona kila tulichozalisha kuwa chema isipokuwa mila na tamaduni zetu. Walilenga kuua tamaduni zetu ili kutugeuza watumwa wao milele. Walikata uzi uliotuunganisha na kuzalisha hili tabaka la walalamishi wa mambo madogo kama kuchinja. Mbona amuulizii kufuga? Shame on you!
 
We TumainiEL unalilia jambo uclolijua, watu walitumia udini kupata madaraka 2010, ndugu zako wametumia ustaarabu kama haki yao,bado watu wanataka kuanzisha mahakama za kidini, ikulu zamu za kidini, nk nk, sasa serikal ikajichanganya hapo, ikawakemea wakristu kwamba huo ndio utaratibu., acha wavune walichopanda.. mchezo huu ni mauti yetu sote!!
 
Tatizo siyo waislam kuchinja ndugu yangu, bali kwao ni ibada sasa wanatulisha vitu vilivyofanyiwa ibada tofauti na misingi ya imani yetu. Hapo ndipo tumepata utata kwamba kumbe kulikuwa na ibada nyuma ya kuchinja huko.

Nani kakudanganya kuwa kuchinja ni ibada kwa waislamu? Toa ushahidi. Kwa taarifa yako hakuna uhusiano wa ibada na kuchinja kwa sababu hakuna sehemu yoyote katika qurani inayoamrisha ibada ya kuchinja. Pengine watu wanachanganya kitendo cha kuchinja wakati wa Idd el Hajj na kuchinja katika siku zingine. Kuchinja huwa ni ibada kwa siku hii tu na tena imeamrishwa kwa kila mtu mzima mwenye uwezo na siyo watu maalum. Kwa hiyo ni upotoshaji wenye nia ovu kudai kuwa kuchinja ni ibada kwa waislam.
 
Ibada gani kusema alahuu wakbaru maana yake mungu mkubwa kwani wakristo wanavyo chinja usemaje?tusiwe tuna tafuta sababu za kukosana.miaka nenda rudi waislamu ndio wachinjaji hii mambo ya ccm kutugawa kusema cdm ni chama cha wakristo matokeo yake ndio haya cdm hawataki kuchinjiwa na ccm ambao ndio wanajidai waislamu safi.

Usibishe kilicho wazi, watumie maneno yoyote yale, mwisho wa siku kwa waislamu kuchinja kwao ni ibada.....kama mkristu, kushiriki ibadaya kiislamu haitakiwi.
 
Nimekuwa nikifuwatilia saka la nani achinje nyama kule Mwanza, nanimebaki kushikwa na butwa. Jaman nadhan tumesahau mauwaji yakimbari kule Rwanda na sisi tunataman kuchinjana wenyewe kwa wenyewe. Nijambo linanishangaza nakutokuelewa mim ni mkiristo na sion ubaya wa muislam kuchinya kutokana na utamadun tumeuzowea kuwa waislam ndio wanachinja na pasipo katiba kusema mahal popote na mim sion ubaya jaman mbona haya nimambo yatangu miaka mingi nahaijawah kuonekana mtu akilalamika imekuwaje ghafla tunataka kuchinja liwe swala la katiba. Jaman hili ni taifa moja na tu wa moja tusianze kubaguwana kwa udin na ukabila maana hakika hakuna atakaye pona. Yatupasa kumuomba Mungu nakuishi ktk hali ya umoja na upendo kama taifa moja chini ya Rais mmoja. Tusibaguwane wala viongoz wa din tusiwe wa chochez na ikiwezekana hao wakristo wakaondoe kes mahakaman. Mungu ibarik Tanzania na watu wake..

Kiherehere cha CCM; DEMOKRASIA sio VYAMA vya SIASA ni ITIKADI za KULINDA wananchi HURU... Kwa zaidi ya MIAKA 50 kulikuwa hakuna TATIZO hadi CCM ilipoonawapi suala la kujitofautisha na VYAMA VINGINE???
 
Back
Top Bottom