Hili la kuanzisha shule za kata lilikuwa ni la maamuzi magumu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili la kuanzisha shule za kata lilikuwa ni la maamuzi magumu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Karata, Jul 3, 2011.

 1. K

  Karata JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Watanzania tumekumbushwa dhana ya maamuzi magumu ambayo serikali imekuwa inashindwa kuchukua. Bahati mbaya, kila mara wapinzani walipokuwa wanazungumza kauli ya kuitaka serikali kuchukua maamuzi magumu, walikuwa wakizomewa na wabunge wa CCM Mjengoni. Zamu hii kauli ile ile imezungumzwa na mwana-CCM mwenzao, kigogo na mwasisi wa serikali ya awamu ya nne, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa. Ameitaka serikali iache kuogopa, ichukue maamuzi na ikubali sifa au lawama kwa uamuzi wake.

  Nilimsikiliza na kumuona Lowassa akitoa hotuba yake bungeni. Wabunge wengi wa CCM, isipokuwa Samuel Sitta, walikuwa wakimshangilia badala ya kumzomea. Maana yake ni kwamba walikubaliana na kauli yake – ile ile wanayoizomea kila inapozungumzwa na wapinzani!. Lakini kikubwa zaidi ni majibu yaliyotolewa na serikali. Ni majibu ya kejeli. Hayaonyeshi umakini. Yanaendekeza uchovu na ubabaishaji ule ule ulioifikisha hapa ilipo. Serikali, kupitia kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ilipuuza kauli ya Lowassa na kusisitiza kwamba katika miaka 50 ya historia ya Tanzania huru, hakuna serikali iliyofanya maamuzi magumu kama serikali ya awamu ya nne.

  Akataja miradi waliyotekeleza: ujenzi wa shule za kata, umaliziaji wa barabara zilizoachwa na Rais Benjamin Mkapa, ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, kuvunja Baraza la Mawaziri mwaka 2008 na mengine machache. Katika yote haya, sikuona uamuzi wowote mgumu uliotolewa. Ujenzi wa shule za kata nchi nzima ni uamuzi wa kisera ulioanzishwa na Lowassa mwenyewe, lakini haukuwa umefanyiwa maadalizi ya kina. Si uamuzi mgumu kuanzisha shule nyingi zisizo na walimu, vitabu, maabara, mabweni na vifaa vingine muhimu. Hata kama ungekuwa uamuzi mgumu, matokeo ya mitihani ya taifa katika shule hizo, hayaonyeshi kama ni jambo la kujivunia kuingiza watoto kwenye shule wakakaa miaka minne bila kuelimika, wakapoteza mwelekeo wa maisha yao kitaaluma. Badala ya shule za kata, bora wangeanzisha vyuo vichache vya ufundi katika kila wilaya, kwa maandalizi ya kuwapatia wanafunzi stadi za maisha ambazo ni bora kuliko kidato cha nne kisicho na cheti au chenye alama zisizoweza kumsaidia mtoto kuendelea na masomo ya juu. Na bado huu si muujiza, wala si uamuzi mgumu. Ni wajibu wa serikali. Na Siamini kwamba haya ninayojadili ndiyo maamuzi magumu aliyokuwa amekusudia Lowassa bungeni, lakini ni wazi kwamba Lowassa ametupatia fursa ya nyongeza kuibana serikali ifanye maamuzi magumu. Na kama hayo iliyofanya ndiyo inaita maamuzi magumu, basi ice cream imekwisha utamu.

  Ingekuwa heri kama Pinda angepuuza kabisa hoja hii, kuliko kuthubutu kuijibu kwa kutoa kauli inayozidi kushusha heshima ya serikali mbele ya umma. Lakini kama tunakubaliana kwamba haya aliyotaja ndiyo maamuzi magumu ya serikali ya awamu ya nne, basi serikali haijaanza kazi. Je, na huu tuuite uamuzi mgumu?

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Azimio la Arusha,ujenz wa reli ya Tazara,muungano wa tanganyika na zanzibar,kukubali vyama vingi,ujenz wa viwanda pasipo wasomi miaka ya sabini na suala la utaifishaji wa mali za wahujumu uchum ndio maamuz magumu
   
 3. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,433
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Mkuu, kuanzisha shule za kata iinaweza ikawa ni maamuzi magumu kwa sababu hata mlevi kutoa fedha ya matumizi nyumbani ni uamuzi mgumu lakini kununua kerti ya bia sio vigumu
   
Loading...