Hili la kituo kikuu cha mabasi Nyegezi nani anapaswa kuwajibishwa au kuwajibika?

povour3

Member
Dec 11, 2019
5
3
Hili Jambo limekuwa kero kwa wakazi, wafanyabiashara, abiria na wapita njia. Kituo kikuu Cha mabasi Nyegezi -Mwanza, hasa kwa upande wa nyuma Kuna eneo ambalo liko wazi, sehemu hiyo ndio inatumika Kama sehemu ya kuhifadhia takataka.

Vifaa maalumu vya kuhifadhia takataka vimejaa, hivyo kupelekea takataka kutupwa chini na kuzagaa hovyo, hii imekuwa kero kwa, abiria, wafanyabiashara, wapita njia na wakazi wanao zunguka eneo hili ukizingatia huu ni msimu wa mvua (kunaweza tokea mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu nk), pia kumekuwa na harufu mbaya Sana inayo sababishwa na takataka hizi, pia baadhi ya wafanyabiasha wamefungua magenge karibu na takataka hizi wakituo huduma mbalimbali kwa wakazi na watu mbalimbili wanao pita katika eneo hili je,hii sio hatari kwa afya zao na wateja?

Je,nani anapaswa kuwajibika na suala hili au kuwajibishwa kwa maslahi mapema ya jamii kumbuka "Kinga ni Bora kuliko tiba" nawasilisha.
IMG_20191220_165317_7.jpeg
IMG_20191220_165311_0.jpeg
IMG_20191219_171434_2.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli hili dambo ni shida. Mpaka unajiuliza hivi viongozi wa jiji na mamlaka husika hawalioni hili ? Kwa hiyo wanangoja mpaka kiongozi wa Kitaifa aje hapo ndio washugjulikie ? Mbunge wa Nyamagana na Diwani wa kata ya Nyegezi hamlioni tatizo hilo ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom