Hili la katibu wa bunge kashililah likoje?

Kamanda Mlo

Member
Feb 9, 2012
10
4
Thomas Kashililah na ufisadi wa kutisha bunge
Kwa waliosoma ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh, naomba wanisaidie katika hili.
Nimewahi kulisoma katika gazeti moja juu juu, nikajua kuwa lina mwendelezo kutokakana na unyeti wake, lakini ajabu ni kwamba halijawahi kuandikwa tena.
Hili linahusu jinsi yule mkubwa wa bunge, Thomas kashililah. Nasikia anaitwa Dokta, anavyotafuna mapesa yetu pasipo kuhojiwa na mtu. Ripoti ya CAG imemuanika wazi lakini wabunge kimya, wamebaki kuwashughulikia mawaziri na watendaji wengine.
Jana nimesoma mahali Fulani habari iliyokuwa ikijadiliwa na waandishi Fulani ambao nasikia wamekatazwa kuandika taarifa kuwa CAG amemuanika Kashilila kwa kutafuna posho za wabunge 86,960,000.
Pia amebainika kusaini na kujilipa yeye na wasaidizi wake
malipo ya kiasi cha shilingi 20,915,126 kinyume cha kanuni za bunge.
Kama hiyo haikutosha uongozi wa ofisi ya bunge umeripotiwa kuwa na madeni katika taarifa zake za fedha kiasi cha shilingi 209,010,235!
Pia malipo ya kiasi cha shilingi 163,195,130.34 hayakuweza kuwa na nyaraka zinazostahiki.
Ukaguzi huo CAG umebaini shilingi 94,000,000 zililipwa kama posho za muda wa ziada wa kazi lakini zote ziliishia mfukoni mwa Kashililah.
Kiasi cha shilingi 65,803,144 ambazo zilikuwa ni fedha za masurufu ya safari hazikuweza kurudishwa kwa mwaka jana kinyume cha kanuni ya 103(1)(7) na kanuni ya fedha ya mwaka 2001.
CAG amebainisha kiasi cha shilingi 170,858,030 za vocha za malipo kuwa hazipo.
Kashililah ameanikwa na CAG kwa kununua mashine mbovu ya kupigachapa ya shilingi 370,019,894 lakini tangu iliponunuliwa haijawahi kufanya kazi.
Badala yake sasa amekula dili na washkaji zake akakodi kwao mashine nyingine ya kupigia pacha na hao jamaa wanakatiwa kila mwaka 190,480,496 ambazo huwa anagawana nao.
Taarifa hizi zimenistua kweli manake ni zaidi ya ufisadi. na inakuwaje kama kweli CAG kamuanika hivi kwanini mtu huyu haguswi. Au ndiyo wale vijana wa bwana mkubwa wanaochuma kiulani kabla ya 2015 ili wakimbie mapema.
[FONT=Garamond, Calibri, Verdana, Geneva, sans-serif]
[/FONT]
 
Kwa wizi wa Tz kwa sasa figure interms of millions huwa hazifuatiliwi sana mara nyingi ni mwendo wa billion ndo watu hustuka.
Angekuwa Nyerere angesema tumeendelea siku izi na wizi umepanda grade
 
Back
Top Bottom