Hili la katibu wa bunge kashililah likoje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili la katibu wa bunge kashililah likoje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamanda Mlo, Jun 7, 2012.

 1. K

  Kamanda Mlo Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thomas Kashililah na ufisadi wa kutisha bunge
  Kwa waliosoma ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh, naomba wanisaidie katika hili.
  Nimewahi kulisoma katika gazeti moja juu juu, nikajua kuwa lina mwendelezo kutokakana na unyeti wake, lakini ajabu ni kwamba halijawahi kuandikwa tena.
  Hili linahusu jinsi yule mkubwa wa bunge, Thomas kashililah. Nasikia anaitwa Dokta, anavyotafuna mapesa yetu pasipo kuhojiwa na mtu. Ripoti ya CAG imemuanika wazi lakini wabunge kimya, wamebaki kuwashughulikia mawaziri na watendaji wengine.
  Jana nimesoma mahali Fulani habari iliyokuwa ikijadiliwa na waandishi Fulani ambao nasikia wamekatazwa kuandika taarifa kuwa CAG amemuanika Kashilila kwa kutafuna posho za wabunge 86,960,000.
  Pia amebainika kusaini na kujilipa yeye na wasaidizi wake
  malipo ya kiasi cha shilingi 20,915,126 kinyume cha kanuni za bunge.
  Kama hiyo haikutosha uongozi wa ofisi ya bunge umeripotiwa kuwa na madeni katika taarifa zake za fedha kiasi cha shilingi 209,010,235!
  Pia malipo ya kiasi cha shilingi 163,195,130.34 hayakuweza kuwa na nyaraka zinazostahiki.
  Ukaguzi huo CAG umebaini shilingi 94,000,000 zililipwa kama posho za muda wa ziada wa kazi lakini zote ziliishia mfukoni mwa Kashililah.
  Kiasi cha shilingi 65,803,144 ambazo zilikuwa ni fedha za masurufu ya safari hazikuweza kurudishwa kwa mwaka jana kinyume cha kanuni ya 103(1)(7) na kanuni ya fedha ya mwaka 2001.
  CAG amebainisha kiasi cha shilingi 170,858,030 za vocha za malipo kuwa hazipo.
  Kashililah ameanikwa na CAG kwa kununua mashine mbovu ya kupigachapa ya shilingi 370,019,894 lakini tangu iliponunuliwa haijawahi kufanya kazi.
  Badala yake sasa amekula dili na washkaji zake akakodi kwao mashine nyingine ya kupigia pacha na hao jamaa wanakatiwa kila mwaka 190,480,496 ambazo huwa anagawana nao.
  Taarifa hizi zimenistua kweli manake ni zaidi ya ufisadi. na inakuwaje kama kweli CAG kamuanika hivi kwanini mtu huyu haguswi. Au ndiyo wale vijana wa bwana mkubwa wanaochuma kiulani kabla ya 2015 ili wakimbie mapema.
  [FONT=Garamond, Calibri, Verdana, Geneva, sans-serif]
  [/FONT]
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu, katika mihimili 3, bunge ndio watz tulikuwa na imana nalo, lakini ndilo limezidi kuwa onvyo , Mbunge anakamatwa na Rushwa na Fisadi CHENGE kawa mwenyekiti wa kamati ya kudum ya bunge Uchum na Fedha, Katibu wa bunge ndio OVYO, nchi hii mamabo yako Ovyo Ovyo tu, sivyo ndivyo, mahakama zinaingiliwa na serikali ya mkuu... inauma sana Jombaa
   
 3. B

  Bujigile JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 247
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ingependeza sana kama usingeficha ficha hizo sources maana jf we dare to talk openly sasa sijui unaficha nini au unachuki binafsi na Kashililah sema wazi umesoma wapi na kwanini usome juu juu sensitive information kama hiyo, kaa ukijua kuwa hizo pesa kama ni kweli ni pesa zetu walipa kodi. weka wazi watu wajadili.
   
 4. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mie pia nimesoma ripoti ya CAG, nadhani Bunge linahitaji kupelekewa special auditing ili kijiridhisha na yanayosemwa. Kuna mbunge aliwahi kuniambia kuwa kama kuna mahali pesa inaliwa kiulaini ni ktk mhimili wetu wa Bunge. Hata tenda zinazotolewa Bunge ni za kifisadi tangu alipokuwepo Sitta ambaye ni muasisi wa ufisadi ofisi ya bunge. Tenda na manunuzi mengi huko ni balaa. Wajuzi wanasema katibu wa bunge ana udaktari wenye shaka, ebu tuanzie hapo na mwenye data atuletee.

  Spika Makinda asafishe ofisi yake.
   
Loading...