Hili la Jonas Mkude kuingia kambini akiwa kapendeza sio poa kabisa

Jana nilipata nafasi ya kuzama Kambini kwa timu ya Taifa.

Nikiwa Bongo mara nyingi napenda kujibanza na watu wa soka ili kujua mambo mbalimbali ambayo kwa namna moja au nyingine siyatambui.

Kwa bahati nzuri/mbaya mwamba mmoja hivi kutoka pande za Msimbazi akaingi akiwa amependeza kinoma. Nadhani aliutumia vyema ule wakati wa alasiri wa siku ya jana kufanya yake.

Labda huenda alidhani ameonja kidogo na hakuna mtu angeshindwa kumtambua, kwa bahati mbaya mwana alionekana dhahiri hata na wachezaji wenzake kuwa Jey yuko pombe.

Mwalimu hakuweza kulitambua hilo mapema ila baadhi ya maafisa wa benchi la ufundi la Stars waliligundua hilo.

Nikaona Nadir Cannavaro akimuita kando na kuzungumza na mkude kwa dakika kadhaa kabla drill ya kupasha misuli haijaanza.

Baadaye nikapewa taarifa kuwa Nadir alikuwa anamsaidia Jey ili hadha ili isije kujulikana kwa Kocha, Nadir akamshauri kuwa ajifanye kama anaomba ruhusa ya kwenda nyumbani ya kuwa kumetokea na dharura.

Jey akasaidiwa na baadhi ya maafisa wengine hadi akapata ruhusu ya kuondoka.

Ni kocha pakee ambaye mpaka sasa hajafahamu kuwa Mkude alikuja kambini amelewa. Baadhi ya viongozi wengine wa benchi hilo hilo hawakupendezewa kabisa kwa Jey kuja amelewa, waliona kama ni kitendo cha dharau na ukosefu wa heshima kwa kazi.

Leo Nikiwa naongea kwa simu na mmoja wa afisa niliyekutana naye jana kambini jana, akanitaarifu kuwa Kocha ameambiwa mchezo wote ulio tokea. Huenda ametonywa na lile kundi dogo ambalo walichukizwa na lile tukio.

Akaongeza zaidi kwa kuniambia kuwa Kocha ameanza kujenga "kutokuwa" na uaminifu na baadhi ya watu katika benchi la Ufundi. Akasema nisisangae kama baada ya game ya Benin kukawa na mabadiliko katika benchi hilo.

Nashauri:- Ni wakati sasa Jonas Mkude asitishe kuichezea Taifa Stars na awape nafasi Vijawa wengine chipukizi.
Nenda kamshtaki CAS
 
Sikatai kulewa unaweza kulewa muda wowote, lakini kwa mchezaji Tena anayeenda kambini kweli,

Jonas mkude hajitambui
 
Huyu jamaa si aachwe tu,.....

yani utafikiri ni bonge la player kumbe ni average player with confidence......
 
Siku moja Asubuhi ataamka Jonas Mkude pale kambini kwao Bunju na atachoma moto kambi nzima ndio watajua mwamba ana matatizo makubwa ya kisaikolojia
 
Siku moja Asubuhi ataamka Jonas Mkude pale kambini kwao Bunju na atachoma moto kambi nzima ndio watajua mwamba ana matatizo makubwa ya kisaikolojia
Simba walishampima akili,ila sikumbuki matokeo ya vipimo.
 
Back
Top Bottom