Hili la foleni kwenda chooni limenishinda

bartenderznz

JF-Expert Member
Jul 18, 2016
398
195
Katika nyumba za kupanga matatizo na masharti kama vile ratiba za usafi,matatizo ya maji na nyumba kutoifikia kwa urahisi,mikataba bubu,si ajabu kumsikia mwenye nyumba hataki mpangaji mwanamke au mwanaume.

Lakini hili la foleni kwenda chooni ambacho pia ni bafu limenishinda kabisa.

Maisha yangu ni ya mlo mmoja kwa siku ni maisha ambayo Watanzania wengi tunaishi,lakini hili la foleni kwenda chooni hapana kabisa.

Tafakari chukua hataua, weka akiba ili uweze kujikwamua, anza leo taritibu na muombe Mungu akutangulie kwa kila jambo.
 
Wakati unajipanga kutafuta kodi ya chumba cha selfie au kuhamia kwako kabisa, nunua pipa kubwa la plastic ndoo kadhaa na kisado kwa ajili ya haja. Siku kukiwa na foleni ya chooni na umebanwa na haja unatumia kisado chako au kindoo cha lita 10.
Siku kukiwa na foleni na unataka kuoga unatumbukia mwenye pipa usiliweke maji kisha unaogea humo. Usiku ambapo watu wamelala unafanya usafi wa chumba chako na hapo unakuwa umepunguza stress ya foleni ya chooni. Ila kuhamia kwako kunatakiwa kuwa palepale vinginevyo utabweteka hapo.

Kasie.
 
M folen ndo zinanifanyaga naoga saa 11 asubuh....
 
mkuu unataka awe kama yule dereva taksi wa mbezi luis.
 
Usipoangalia hata kwenye nyumba yako kutakuwa na foleni
Jipange....!
 
Katika nyumba za kupanga matatizo na masharti kama vile ratiba za usafi,matatizo ya maji na nyumba kutoifikia kwa urahisi,mikataba bubu,si ajabu kumsikia mwenye nyumba hataki mpangaji mwanamke au mwanaume.

Lakini hili la foleni kwenda chooni ambacho pia ni bafu limenishinda kabisa.

Maisha yangu ni ya mlo mmoja kwa siku ni maisha ambayo Watanzania wengi tunaishi,lakini hili la foleni kwenda chooni hapana kabisa.

Tafakari chukua hataua, weka akiba ili uweze kujikwamua, anza leo taritibu na muombe Mungu akutangulie kwa kila jambo.

M folen ndo zinanifanyaga naoga saa 11 asubuh....

Naam, huo ndio muda wa kuamka na kwenda chooni. Katika nyumba za kupanga kitu kilichokuwa kinanikasirisha ni zamu ya kusafisha choo. Aisee kila nikimkumbuka mama mwenye nyumba aliyenishikisha fagio, huwa namshukuru sana. Na yeye ndiye alikuwa chachu ya kutafuta sehemu yangu ya kujistiri. Aliniokoa na ndiye alinifanya nijue maisha yakoje.
We acha kabisa, kufagia choo! Ingawa tulisafisha vyoo kama adhabu wakati tunasoma lakini hili la kusafisha choo huku mimi ni muajiriwa na tena kuna watu ofisini wananiita bosi lilinikosesha raha kabisa. Usiombe uwe umetembelewa na "mchumba" au mgeni, sheria ya zamu ya kufagia uwanja au choo ni kwa wale anaowatambua tu, mwenye nyumba haikubali mgeni yeyote kushika fagio.
 
Back
Top Bottom