gango2
JF-Expert Member
- Aug 31, 2011
- 1,941
- 2,251
Habarini za mchana! (mods naomba thread hii isiunganishwe tafadhari)
Kwanza kabisa napenda kudeclear kuwa mimi ni mpenzi wa burudani na sio Fiesta au wasafi festival, hizi zote mimi nilikuwa naona ni chachu ya maendeleo ya sanaa na burudani Tanzania!
sasa nikija kwenye maada, nimeshangazwa sana na taarifa zilizotolewa hivi karibuni kuhusu hii FIESTA kuahirishwa! Kwa mtu yeyote anayefikiria au anayeangalia investments iliyofanywa hapo ni dhahiri atakuwa amesikitishwa sana na hichi kilichotokea. Hasa ukizingatia muda wa zuio ulipotolewa Nimesema hivi kwa sababu
mwisho! kama tunataka ushindani wenye tija, basi tufanye kwa misingi iliyobora na sio kwa kuwakandamiza wengine, tutakuwa tunafanya kazi ya kukinga maji kwenye kikapu cha makuti!
nawasilisha hoja! naomba tujadili kwa hoja
GanGo

- kwanza kuna investments kubwa imefanywa katika maandalizi, matangazo, gharama zote hizi zinapotea bila sababu ya msingi, na kusababisha hasara kubwa kwa waandaaji
- Pili ni usumbufu uliojitokeza kwa wepenzi wa burudani, naamini kuna watu wengi wamejiandaa na wengine labda walisafiri kutoka maeneo ya mbali na hata wengine kuhairisha vitu vingine ili waudhurie tamasha hili
- Tatu, ni kwa namna gani wasanii na watumbuizaji walivyojiandaa na wengine walitumia gharama zao na wengine walikataa show sehemu za mbali kwaajili yahili. Najaribu kufikiria tu endapo kungekuwa na mualikwa toka nje ya nchi sijui ingekuwaje
- kwanza suala Leaders clubs kutumika kwa fiesta au matamasha mengine mengi sidhani kama limeanza mwaka huu, ni zaidi ya miaka 12 sasa linafanyika hapo, bila kipingamizi sasa leo kusema ni kelele ni logic ambayo haileti maana kabisa
- Pili kwanini zuio litolewe siku moja kabla wakati maandalizi yameshafanyika, hivi kulikuwa na haja ya kusubiri siku moja kabla ndo zuio litolewe, na je kama kuna malalamiko yametoka wapi na hospitali gani kulalamikia hili
- Tatu, hivi unaposema uende Tanganyika Parkers inamaana huko tanganyika Parkers hakuna binadamu wanaoishi huko? tena naamini kawe ndo kuna watu wengi kuliko maeneo ya hapo Leaders! au kwa kuwa watu wengi wanaoishi kawe ni wa vipato vya chini kwa hiyo wao kelele ni kutu cha kawaida
- nne mwaka jana tu Rais alibariki hili tamasha lifanyike pale pale na tena mpaka asubuhi, sasa tunashangaa hayo matamko leo kuwa pale ni usumbufu yanatoka wapi? Pia hapo hapo tunaona kiongozi mkubwa wa mkoa anashiriki uhamasishaji lakini leo barua inatoka kwa mtu mdogo kabisa