#COVID19 Hili la Chanjo ni hiari yako kuchagua kati ya hatari ndogo na hatari kubwa

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,874
Kuhusu chanjo ni hiari yako kuchagua kati ya hatari ndogo (Low risk) na hatari kubwa (High risk).

Kila chanjo ina lengo moja tu. Lengo la kuongeza kinga katika mwili wako.

Na kila chanjo lazima iwe na ingredient ya weakened antigen au tinny fragmentation of diseasing -causing organism yaani sehemu ndogo ya kiumbe au kirusi kinachosababisha ugonjwa huo ambacho kimedhoofishwa na kisicholeta madhara ktk mwili.Huingizwa kama code ili mwili wako uweze kutambua, kukumbuka na kupambana na Antigen (kirusi) cha namna hiyo pindi kitakapoingia kama maambukizi muda au siku yeyote katika mwili.

Lengo lake unapotumia chanjo hii ina kwenda ku trigger mwili wako kupitia white blood cell, ambayo hupelekea kuzalishwa kwa antibodies hivyo Kuimarisha KINGA yaani immune system au body natural defense ili kuwa na uwezo wa kukumbuka, kutambua na kupambana dhidi ya kirusi pindi kinapojitokeza.

Chanjo haifanyi chochote katika mwili wako zaidi ya kuongeza Kinga ya mwili wako . Chanjo haikuzuii wewe kupata Corona ila inaongeza uimara wa kupambana na kirusi na kukiangamiza kabla chenyewe hakijakudhoofisha , anayetumia chanjo ana hatari ndogo (Low risk) ya kupata corona , na hata akipata ana hatari ndogo (Low risk) ya kudhoofishwa na kuangamizwa na kirusi sababu ya uimara wa Kinga (Immunity) aliyo nayo mwilini kwake kutokana na chanjo.

Mtu anayetumia chanjo ana hatari ndogo (Low risk) ya kuambukiza wengine sababu ya uwezo wa kinga yake ya mwili kupambana na kirusi hivyo kutokuwa highly exposed ktk transmission.

Mtu ambaye hajatumia chanjo anakuwa hatari kubwa (High risk) ya kutokuwa na uimara katika mfumo wake wa kinga wa mwili yaani (Immunity system).

Sababu White bood cell haiwi triggered kutengeneza cell ya antibodies inayosaidia kuimarisha kinga katika mwili wake hivyo anakuwa na hatari kubwa (High risk)

Hivyo mtu huyu ana hatari kubwa (high risk) ya kupata corona, Mtu huyu ana hatari kubwa (High risk ) ya kudhoofishwa na Corona kwa urahisi sana na kwa haraka hata kufa sababu mwili wako unakuwa mwepesi sana kushambuliwa sababu ya kutokuwa na uimara wa mfumo wa kinga au uimara wa kinga katika mwili wake. Hivyo anakuwa na hatari kubwa (High risk)

Mtu huyu ana hatari kubwa saana (High risk) kuambukizwa na kuambukiza wengine sababu corona/antigen/germ/kirusi ni rahisi kuingia na kusettle katika mwili wake bila kusambaratishwa kutokana na kinga yake kuwa dhoofu hivyo kuwa High exposed in transmission hivyo anakuwa na hatari kubwa High risk.

Ndio maana watu wanaoathiriwa sana na COVID ni watu ambao kinga yao sio imara ,aidha wana magonjwa nyemelezi ,kuwa na umri mkubwa kuanzia 40 kwenda juu au pia unaweza kuwa na umri mdogo ila kinga yako ikawa ipo chini au dhoofu.Hawa wanakuwa katika hatari kubwa (High risk ) ya kuambukizwa.

Hivyo silaha pekee kwake ,kwako,kwao na kwetu ni kuchanja ili kuongeza kinga na kuepukana na hatari kubwa (High risk) ya kupata corona.

Siku zote kumbuka hakuna dawa ya Corona ila kuna chanjo, Chanjo ni silaha muhimu na ya msingi katika mapambano dhidi ya corona katika uwanja wa vita ndani ya miili yetu.

"The vaccine is the critical tool in the battle against COVID-19 at the war-field in our body.

1. Chanja

2. Vaa barakoa

3. Epuka mikusanyiko

4. Safisha mikono yako

Chukua hatua zingine muhimu za kitaalamu na kisayansi

Abdul Nondo.
 
Imepita awamu ya Kwanza ya korona Kinga zetu zimepambana

Ikaletwa awamu ya pili Kinga zetu zikapambana

Sasa imeletwa hii ya awamu ya Tatu.

Natumai Kinga zetu zimeshazoea hayo mamikiki mikiki ya korona
 
Mambo ya Chanjo na Corona yaliharibiwa sana na mwendazake, wananchi hasa wa mikoani hawataki hata kusikikia hii kitu kabisa.

Yaani kutahitajika elimu ya ziada kuwafanya wananchi hasa wa kanda za ziwa kuchanja hii chanjo.
 
Pale mwanasayansi wa siasa anapoelezea sayansi ya chanjo, watanzania tutafika mbinguni tumechoka sana.
 
Mambo ya Chanjo na Corona yaliharibiwa sana na mwendazake, wananchi hasa wa mikoani hawataki hata kusikikia hii kitu kabisa.

Yaani kutahitajika elimu ya ziada kuwafanya wananchi hasa wa kanda za ziwa kuchanja hii chanjo.
Makofi kwa mwenzake!! pwa pwa, pwa, pwa
 
wagonjwa wa,
1.KISUKARI
2.PRESHA
3.MOYO
4.SARATANI
5.UKIMWI
wagonjwa wa maradhi hayo wanapaswa wachue tahadhari sana maana Corona itatumaliza sana.
 
Nikujifunza na kusoma, kaka.
Kwahiyo hapo Mkuu tatizo ni udhaifu wa kinga za mtu au ni aina ya kirusi chenyewe? Kwa maana kirusi chenyewe ni hatari na kinga zetu za mwili hakiwezi kupamba nacho ndio maana inabidi tutumie chanjo au kwamba tatizo ni wenye udhaifu wa kinga zao za mwili hivyo huitajika kutumia chanjo ili kuzipa nguvu kinga zao?
 
Kuhusu chanjo ni hiari yako kuchagua kati ya hatari ndogo (Low risk) na hatari kubwa (High risk).

Kila chanjo ina lengo moja tu. Lengo la kuongeza kinga katika mwili wako.

Na kila chanjo lazima iwe na ingredient ya weakened antigen au tinny fragmentation of diseasing -causing organism yaani sehemu ndogo ya kiumbe au kirusi kinachosababisha ugonjwa huo ambacho kimedhoofishwa na kisicholeta madhara ktk mwili.Huingizwa kama code ili mwili wako uweze kutambua, kukumbuka na kupambana na Antigen (kirusi) cha namna hiyo pindi kitakapoingia kama maambukizi muda au siku yeyote katika mwili.

Lengo lake unapotumia chanjo hii ina kwenda ku trigger mwili wako kupitia white blood cell, ambayo hupelekea kuzalishwa kwa antibodies hivyo Kuimarisha KINGA yaani immune system au body natural defense ili kuwa na uwezo wa kukumbuka, kutambua na kupambana dhidi ya kirusi pindi kinapojitokeza.

Chanjo haifanyi chochote katika mwili wako zaidi ya kuongeza Kinga ya mwili wako . Chanjo haikuzuii wewe kupata Corona ila inaongeza uimara wa kupambana na kirusi na kukiangamiza kabla chenyewe hakijakudhoofisha , anayetumia chanjo ana hatari ndogo (Low risk) ya kupata corona , na hata akipata ana hatari ndogo (Low risk) ya kudhoofishwa na kuangamizwa na kirusi sababu ya uimara wa Kinga (Immunity) aliyo nayo mwilini kwake kutokana na chanjo.

Mtu anayetumia chanjo ana hatari ndogo (Low risk) ya kuambukiza wengine sababu ya uwezo wa kinga yake ya mwili kupambana na kirusi hivyo kutokuwa highly exposed ktk transmission.

Mtu ambaye hajatumia chanjo anakuwa hatari kubwa (High risk) ya kutokuwa na uimara katika mfumo wake wa kinga wa mwili yaani (Immunity system).

Sababu White bood cell haiwi triggered kutengeneza cell ya antibodies inayosaidia kuimarisha kinga katika mwili wake hivyo anakuwa na hatari kubwa (High risk)

Hivyo mtu huyu ana hatari kubwa (high risk) ya kupata corona, Mtu huyu ana hatari kubwa (High risk ) ya kudhoofishwa na Corona kwa urahisi sana na kwa haraka hata kufa sababu mwili wako unakuwa mwepesi sana kushambuliwa sababu ya kutokuwa na uimara wa mfumo wa kinga au uimara wa kinga katika mwili wake. Hivyo anakuwa na hatari kubwa (High risk)

Mtu huyu ana hatari kubwa saana (High risk) kuambukizwa na kuambukiza wengine sababu corona/antigen/germ/kirusi ni rahisi kuingia na kusettle katika mwili wake bila kusambaratishwa kutokana na kinga yake kuwa dhoofu hivyo kuwa High exposed in transmission hivyo anakuwa na hatari kubwa High risk.

Ndio maana watu wanaoathiriwa sana na COVID ni watu ambao kinga yao sio imara ,aidha wana magonjwa nyemelezi ,kuwa na umri mkubwa kuanzia 40 kwenda juu au pia unaweza kuwa na umri mdogo ila kinga yako ikawa ipo chini au dhoofu.Hawa wanakuwa katika hatari kubwa (High risk ) ya kuambukizwa.

Hivyo silaha pekee kwake ,kwako,kwao na kwetu ni kuchanja ili kuongeza kinga na kuepukana na hatari kubwa (High risk) ya kupata corona.

Siku zote kumbuka hakuna dawa ya Corona ila kuna chanjo, Chanjo ni silaha muhimu na ya msingi katika mapambano dhidi ya corona katika uwanja wa vita ndani ya miili yetu.

"The vaccine is the critical tool in the battle against COVID-19 at the war-field in our body.

1. Chanja

2. Vaa barakoa

3. Epuka mikusanyiko

4. Safisha mikono yako

Chukua hatua zingine muhimu za kitaalamu na kisayansi

Abdul Nondo.
Acha upumbavu wako hapa. Unadhani kila kitu ni siasa uchwara za kujiteka? Pumbavu sana.
 
Back
Top Bottom