Hili la Chama cha Watetea Haki za Wanawake nchini Australia kuhusiana na ‘ Hedhi ‘ likitua TZ ‘ Waajiri ‘ mtakoma!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,548
108,859
Chama cha Watetea Haki za Wanawake huko nchini Australia kinapambana usiku na mchana kuhakikisha kwamba ‘ Sera ‘ ya Wanawake ambao huwa wanapatwa na ‘ maumivu ‘ makubwa au ‘ uchungu ‘ mkubwa wakati wakiwa katika Siku zao za Hedhi ( Menstruation ) wawe wanapewa Likizo ya Malipo kwa hizo Siku ambazo wanakuwa Hedhini.

Chama hicho kimeitaka Serikali ya nchi hiyo kuhakikisha hii ‘ Sera ‘ inakubalika na kwamba katika kila Kampuni kufanyike ‘ uchunguzi ‘ na kama wakigundulika Wanawake ambao hupatwa na ‘ Maumivu ‘ hayo wakiwa Hedhini basi wapewe Likizo ya Malipo kwa Kigezo cha kwamba Wanawake hao huwa wanakuwa katika hali ngumu ambayo ‘ haielezeki ‘ na vile vile Wao pia ni Wazazi ambao wengi wao huja kuwa Wafanyakazi wa Makampuni na Taasisi nyingi hivyo wanapashwa ‘ Kuthaminiwa ‘ sana.

Sipati picha hii ‘ Kitu ‘ nayo Wanawake wa Tanzania hasa wale wanaowapigania nao ‘ Wakiiga ‘ jinsi ambavyo humo Maofisi kutakuwa kunabaki tu Wafanyakazi wa Kiume pekee na pia jinsi ‘ Waajiri ‘ wengi wa Tanzania watakavyoingia ‘ gharama ‘ za lazima ili tu kutimiza matakwa yao na kuongeza Ufanisi wa Kiutendaji.

Nawasilisha.

Chanzo: CNN
 
Tutaskia mengi pot, Ngoja huku kwetu wafike kama wataweza maana hata wale TWAWEZA wanafahamu kilichowakuta!
Btw,
Bado sana kwa huku pot
 
Back
Top Bottom