maiyanga1
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 1,317
- 1,790
Mimi ni mdau wa usafiri wa umma na kwa kiasi fulani nimetembea katika maeneo tofautitofauti. SUMATRA ikiwa ni mamlaka inayosimamia usafiri wa nchi kavu na majini, wanafahamu kwamba maeneo mengi ya vijijini wafanyabiashara ya usafiri huwatoza abiria nauli moja hata kama msafiri hafiki kituo cha mwisho? Na kama wanafahamu wanachukua hatua gani? Nna mifano kadhaa:
1. Abiria anayepanda gari Shinyanga mjini kwenda Munze (wilaya ya Kishapu) analipa sh. 3000 hii haijalishi anashuka katikati au kituo cha mwisho.
2. Abiria anayepanda gari Muheza kwenda Bombani analipa sh. 1000 hata kama anashuka kituo chochote kabla ya Bombani.
3. Abiria anayepanda gari Arusha kwenda Tanga hulipa nauli ya Tanga hata kama anashuka Segera, Hale, Muheza au Pongwe.
Wadau mnaweza kuongezea mifano mingine.
Ninajua kwamba nauli hupangwa kwa kila kilometa, ikitofautisha barabara ya lami na barabara ya vumbi.
Serikali yetu inaongelea wanyonge kwenu SUMATRA mnatuchukuliaje tunaotumia usafiri wa umma?