Hili kutoka kwa houseboy nalo ni neno hasaa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili kutoka kwa houseboy nalo ni neno hasaa!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by amanibaraka, Dec 28, 2010.

 1. amanibaraka

  amanibaraka JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 258
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  NIME QUOTE TOKA KWA HOUSEBOY:

  Hivi mbona katika jamii forum watu wengi mnawasakama sana Kikwete na Mwinyi tu,katika kila kitu,mbona hoja mnazoleta hazina hata miguu,kuna ushaidi wa hili?au mambo mnayomsingizia huyu jamaa?.mbona mjomba wenu alipokua anajipa mali za umma mlikua hampigi kelele au mbona hakuna hata hoja moja ya kudai jamaa arudishe hela na viwanda alivyojiuzia au fafa la Rada alilonunua mbali na bunge la uingeleza kupinga.kelele zinakuwepo kila raisi anapokua muislamu tu,au mbona viinzi vya mwanakijiji na data nyweti za ndani ya gov zinakua hazipatikani wakati wa Mkapa?.hakuna kitu kibaya sana kama kutoa data za uongo au za kizushi,kuna watu humu ndani wao wanaona kila kitu ni udini tu.Tanzania tatizo lake si kikwete au Mwinyi,Tatizo la bongo ni umasikini wa kutupwa ambao umeletwa na na kuendelezwa na viongozi wabovu bila kujali dini zao,mfano wakati wa Mwalimu (My God bless him) watanzania walikua wanakufa na njaa,tulikua tunapanga foleni masaa 8 au siku nzima kungojea kilo moja ya unga,au mchele,watu tulilazimiswa kuamia katika vijiji vya ujamaa matokeo watu wengi walikufa,ulikua ukisema tu kitu kumpinga mwalimu ndani na watu wengi walipotea kwa kuchukuliwa kiaina,tasisi na mashilika ya umma yalijaa ukabila mtupu,akaja mzee ruska akafanya alichofanya kama raisi na kumpa kijiti mkapa na kufanya alichoweza na sasa ni zamu ya kikwete .kwa mtazamo wangu bila unazi wala nini jamaa wote hawa ni wabovu .ni muhimu kuwa na data za kikweli na si ushabiki .
   
 2. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  umetumwa?
   
 3. c

  charityboy Senior Member

  #3
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umesema kweli
   
 4. c

  charityboy Senior Member

  #4
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CDM siasa hawaijui bora warudi karatu
   
 5. mabuba

  mabuba Senior Member

  #5
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 133
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  hii ni kweli tupu
   
 6. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  :bump: slow down!
   
 7. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2010
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Depends with level of utandawazi during his era, but he is still discussed,
   
 8. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2010
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,695
  Likes Received: 753
  Trophy Points: 280
  Ngoja nikae kimya
   
 9. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  But at least umeandika Kitu....Good...
   
 10. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2010
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  :teeth:
   
 11. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwenye msafara wa mamba kenge nao wamo
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nyerere pia ameshambuliwa sana hapa jamvini, wapo waliosema alikuwa mdini na Mkapa pia wakati wa kashifa za ufisadi alishambuliwa hapa JF na kuhusishwa na mgodi wa kiwira. Kinachompata kikwete sehemu kubwa ni kurithi baadhi ya matatizo ya awamu ya Mkapa ambayo baadhi yake leo hii imekuwa ni kauli mbiu ya wapinzani kwa mfano...UFISADI.... katika ufisadi wanaotuhumiwa ni waislamu na wakristo kama vile Andrew Chenge, Rostam Azizi, Edward Lowassa, Nazil karamagi, Gray Mgonja, Ibarahim Msabaha, Basil Mramba na Daniel Yona na wengineo.

  Kumshambulia Rais aliyepo madarakani kuna athari kwa watu wa dini zote kama ilivyoelezwa katika mfano wa ufisadi hapo juu. Kashfa anazotupiwa Mkapa zinawahusisha na waislamu pia katika ununuzi wa ndege ya Rais na vifaa vya jeshi kama vile Tamil somaia na vithlan aliyekimbia nchi. Hii ina maana kwamba, kumashambulia Mkapa hakuna maana unaushambulia ukristo na kumshambulia kikwete hakuna maana ni kuushambulia uislamu kwa sababu waathirika wa mashambulio hayo ni waislamu kwa wakristo.

  Naona tujenge hoja za nguvu kupinga mashambulio hayo badala ya kufikiri kwamba ni ubaguzi wa kidini. Utakapoendeza mambo hayo kuna mwingine atainuka atasema kujiuzulu kwa Lowassa na kuondolewa kwa Sitta ni chuki za kidini. Tujenge hoja za kupinga au kuunga mkono kwa kuzingatia kadhai zinazowapata wanasiasa kama vile tuhuma za Richmond au Bunge kujitenga na msimamo wa chama chenye wabunge wengi, CCM.
   
 13. S

  Subira Senior Member

  #13
  Dec 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  namuomba mungu hii forum isiwe hivi invyokwenda maana matusi na lugha chafu chafu za kukatisha tamaa mawazo ya mtu bila kujali utu wa mtu ndio yametawala humu, hebu tujaribunikutowajibu watu kwa karaha hii forum iwe ni ya watu wote kaaa
   
 14. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,640
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280


  Umezuiwa kumwaga data za Ben? Au ndo nyie mnaosubiri wengine waandike halafu mpinge? Andika wewe basi, huenda wengine hawazijui data za kuwashutumu akina Ben!
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nyerere pia anatuhumiwa kwenye operesheni ya vijiji vya ujamaa kwamba iliua watu, anatuhumiwa kwenye utaifishaji wa nyumba wakati wa azimio la Arusha, anatuhumiwa kwamba alielekeza nguvu nyingi kwenye ukombozi wa nchi za Afrika na kusahau nyumbani.

  Yote haya yamezungumzwa hapa, sidhani kama hoja hizi ni za kumchukia nyerere au za kidini bali wananchi walikuwa sehemu ya mafaniko au matatizo ya utawala wake haiepukiki kuzungumzia.

  Tujenge hoja, tusitafute majibu mapesi kwa maswali magumu.
   
 16. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,601
  Likes Received: 4,716
  Trophy Points: 280
  Hivi ni nani aliyemkingia Fisadi Mkapa kifua kuwa aachwe apumzike kama siyo Kikwete? Hizi hoja zenu za kijinga zaudini ndizo mtaji wa mafisadi kutufukarisha. Madhara ya ufisadi hayachagui dini.Akifanya ufisadi mkristo tunaumia wote wakristo, waislamu na wasio na dini, vivyo hivyo akifanya ufisadi muislamu madhara yake yanatuangukia wote wakristo na waislamu.Nimegundua kuwa wanaonzisha mijadala ya dini hapa wala wenyewe siyo wadini pengine hawana dini kabisa bali wao ni mawakala wa mafisadi. Mafisadi pamoja na watawala wanaogopa saaaaana umoja wa watanzania, na mara nyingi hoja za ufisadi zimekuwa zikiwaunganisha watanzania kwani wote tumekuwa wahanga wa mafisadi, hivyo mafisadi ndiyo wamekuja na mbinu hii ya udini ili kutugawa tusije tukapata nguvu ya pamoja kuwakabili na kuwahukumu. Sasa humu kuna watu wanaingia kichwa kichwa kushabikia hoja hizi za udini na mafisadi wanatucheeeeka kwani wamefanikiwa kutugawa. Mafisadi wanaotufukarisha Watanzania ni wa dini tofauti lakini wao wanao umoja wao wa kifisadi na wana mshikamano wa hali ya juu kulinda maslahi yao, wao ni marafiki wana kula na kunywa pamoja jasho letu halafu sisi wahujumiwa tunarushiana maneno ya kijinga, huo ni ushamba.MTU YEYOTE ANAYECHAGUA KIONGOZI KWA MISINGI YA DINI NI MPUMBAVU KABISA.Mkapa ni mkristo lakini alifanya ufisadi akishirikiana na wakristo na waislamu kutuhujumu, Kikwete ni muislamu na fisadi akishirikiana na mafisadi waislamu na wakristo kama EL,AC, NK, kwa hiyo ufisadi hauna dini na athari zake hazichagui.Watanzania tuungane kuwaangusha mafisadi wooooote na kuwahukumu hata ikibidi kuwauwa wote na vizazi vyao ili taifa lipone.
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kuna kigezo cha maendeleo ya sayansi na mahitaji ya wakati unapotaka kulinganisha utawala mmoja na mwingine. kwa mfano, JF ilianzishwa 2006 wakati huo ni utawala wa kikwete, hii ina maana kwamba tabia ya mtandao huu itaendelea kuwakumba viongozi wote wajao bila kujali dini zao kwa sababu za wakati. Lakini hatutegemei mtandao huu ukachukua nafasi kubwa ya mjadala wa tawala zilizopita na kuacha utawala uliopo.

  Kufananisha utawala mmoja na mwingine bila kuangalia vigezo zaidi kama vile uhuru wa kutoa maoni ambao umelegezwa zaidi katika utawala wa kikwete ni makosa. Utawala wa nyerere ulifinya uhuru wa kutoa maoni kwa sababu za wakati huo, utawala wa mwinyi ulipanua soko huru, utawala wa mkapa ulibinafsisha.

  Najenga hoja hizi ili kuepusha kujenga hisia za kidini tunapojadili masuala ya kitaifa.
   
 18. m

  mams JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Bwana mdogo inabidi uende shule na ukirudi huko utaacha kujadili dini na badala yake utaleta hoja zenye mshiko hapa jamvini.
   
 19. Bless the 12

  Bless the 12 Member

  #19
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ----------------

  Punguza hasira and slow down mkuu, sasa wewe unaesema watu wanaongea bila data mbona ndo wewe wa kwanza unaleta post hii bila data na kutanguliza hisia mbele?

  Hii ni home of great thinkers, msilete hoja za hisia hisia tu, Tunapoongelea maendeleo ya tanzania tutangulize facts and data. Maana ya maendeleo ya nchi ni nini? Kuna vitu vya msingi tunavyoangalia katika kupima maendeleo ya nchi, baadhi ni huduma za jamii kama afya, elimu n.k. Kuna kipimo cha uchumi ambapo kigezo ni GDP, inflation etc. Sasa basi hata viongozi wa nchi tunapowaongelea wamefanyia nini nchi lazima upime katika haya kwa takwimu halisi, mengine ni hali ya utawala bora na rushwa kama tathmini ya uadilifu wa serikali husika. Yote haya unatakiwa kuyasema kwa takwimu. Sasa basi wewe unazungumzia wakati wa Nyerere watu walikufa, je una takwimu au unahisi tu kwa kusikia? Mie nadhan wakati wa Nyerere ulikuwa wakati wa kujenga misingi ya nchi.

  Kama utakubaliana na mimi, kuna misingi mpk leo unaenjoy hujui viongozi walifanya jitihada zipi kuyafanya, mambo ya umoja wa nchi na uraia si misingi ambayo viongozi wa sasa wangeweza kufanya kwa jinsi walivyo wala rushwa. Kwa hiyo Nyerere kafanya yake kuweka misingi ya nchi lkn kwa uchumi hakufanikiwa, kwa hiyo ilikuwa jukumu la viongozi waliofata baada ya Nyerere kurekebisha hapo.

  Mwinyi bahati mbaya hakufanya vema kwenye uchumi pia na tulizidi kuporomoka na mbaya zaidi aliruhusu hata misingi ya nchi kuporomoka hata rushwa na udini ukaanza. Nadhani wote mna takwimu hizi kwamba makusanyo ya kodi kwa serikali yalishuka kufikia mpk chini ya bilioni 30 kwa mwezi sababu ya rushwa na misamaha ya kodi, hali iliyopelelea huduma za jamii kudorora, sera za free market hazikudhibitiwa hatimae hata inflation ikawa juu mpk asilimia zaidi ya 20!

  Awamu ya Mkapa ikaja kwa kurekebisha uchumi kiasi ambapo hata makusanyo ya serikali yakaboreka kutoka bilioni 30 kwa mwezi mpk bilioni zaidi ya 100 mnamo 2004, inflation ikashuka kutoka asilimia 20 mwaka 1998 mpk asilimia 5 na wakati wake wote alimantain inflation of below 5 percent. Hii iliboresha kiasi huduma za jamii kufikia serikali kumudu hata ujenzi wa barabara.lkn Mkapa hakuweza kudhibiti vizuri sera za ubinafsishaji na rushwa kwa viongozi wake. Hili tatizo lingepaswa kushughulikiwa na serikali ya sasa ya Kikwete lkn limeshamshinda.

  Awamu ya kikwete imenufaika zaidi na hazina iliyowekwa na serikali iliyopita na hii ndo nafuu yake lkn kusengekuwapo na fedha hakika hali ingetisha, maana matatizo ya rushwa na ubinafsishaji na uwekezaji holela ambao Mkapa alishindwa kusimamia yeye pia amezidi kuendekeza zaidi na ndi maana tunaongelea mafisadi. Kwa upande wa uchumi kitakwimu ameharibu kabisa hali iliyojengwa na Mkapa, sasa hivi inflation ni juu ya asilimia 10 na thamani ya pesa imeshuka kwa zaidi ya asilimia 10 (soma publication za bank of tanzania).

  Kwa hiyo ndugu yangu ni vema tutathmini kwa takwimu hizi, JK hamna analolifanya na nchi imepoteza dira. Udini anaozungumzia ccm na jk wala haupo in fact na hizi ni propaganda za chama tawala kushambulia wapinzani wasiaminike. Udini upo kwa viongozi wala sio raia.
   
 20. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #20
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kimsingi Kikwete anaonekana na kudiskasika sababu yeye ndo Raisi na anamamlaka ya kuwashtaki watangulizi wote waliofuja mali za nchi!
  Tunapokuwa wanazi tukasahau dini na siasa ni pande mbili tofauti tunakosea sana!
  Nafikiri ifike mahali pawe na Jukwaa litakalo zungumzia matatizo ya uhusiano katika nyanja zima ya dini na imani zetu!
  Maana sasa hawa wanao badili kila hoja kwa dhana ya udini hapa si kwao! lau wakiwa na jukwaa lao watakuwa nanafasi nzuri ya kutoka madukuduku yao.
   
Loading...