Hili jukwaa linapoteza maana kwa kuvamia na watu wasio madaktari

kombaME

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
2,115
2,808
Habarini humu,

Nadhani lengo la jukwa hili ni kuwapa nafasi wale wenye matatizo ya kiafya kupata suluhisho la matatizo yao, lakini muda mrefu nimekuwa nafuatilia humu, mtu anaweza kuleta tatizo lake lakini bahati mbaya sana wengi hutoa majibu ya kupotosha kabisa, mtu anaweza kutoa maelezo au akatoa ''shule'' ya uwongo kabisa na inaweza isimpe suluhisho yule mwenye kutaka msaada.

Ushauri wangu, tuwape nafasi madaktari wetu watusaidie kupitia jukwaa hili sisi wengine ambao tupo kwenye taaluma zingine tuwe wauliza maswali, sio kuja kutoa kitu ulichosimuliwa au kugoogle, jua tu malaria ni ile ile ila sio wagonjwa wote wa malaria watapona kwa ALU, kuna factor nyingine nyingi za kuangalia, so sio kwasababu wewe ulipona malaria kwa coartem ndo umshauri mwingine atumie, sio always hivyo.

AHSANTENI
 
wengine ni ma profesa na dr.manyau nyau mkuu kama tiba ya hosp. inazingua sie tunatoa mawazo ya kitaa (dawa) na zinatibu kweli. kuwa mvumilivu.

mambo ya ukijikata, huduma ya kwanza ni kujikojolea kwenye jeraha hatari san.
 
Kabisa mkuu... Kuna siku nilikuwa naona mada kuhusu UTI nilichoka kabisa na huku mtaani wengi sana wanadanganywa hivyo hivyo. Maana UTI imekuwa biashara kubwa siku hizi.
 
Habarini humu,

Nadhani lengo la jukwa hili ni kuwapa nafasi wale wenye matatizo ya kiafya kupata suluhisho la matatizo yao, lakini muda mrefu nimekuwa nafuatilia humu, mtu anaweza kuleta tatizo lake lakini bahati mbaya sana wengi hutoa majibu ya kupotosha kabisa, mtu anaweza kutoa maelezo au akatoa ''shule'' ya uwongo kabisa na inaweza isimpe suluhisho yule mwenye kutaka msaada.

Ushauri wangu, tuwape nafasi madaktari wetu watusaidie kupitia jukwaa hili sisi wengine ambao tupo kwenye taaluma zingine tuwe wauliza maswali, sio kuja kutoa kitu ulichosimuliwa au kugoogle, jua tu malaria ni ile ile ila sio wagonjwa wote wa malaria watapona kwa ALU, kuna factor nyingine nyingi za kuangalia, so sio kwasababu wewe ulipona malaria kwa coartem ndo umshauri mwingine atumie, sio always hivyo.

AHSANTENI
Wachangiaji wengi wao wanatoka katika jukwaa la Chitchat sasa na hili jukwaa wamelifanya kama vile jukwaa la pili la chitchat kungelikuwa na Moderator wa kuliongoza hili jukwaa na kuondosha baadhi ya Comment za chit chat kidogo jukwaa lingekuwa zuri lakini wapi? tuende hivyo hivyo tutafika tunapokwenda mkuu.
 
Back
Top Bottom