Hili Jicho limepotelea wapi?

Bengalisis

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
1,847
2,768
JICHO HILI LINAPOTEA

Nikiwa mdogo, Mama yangu alikuwa anawasiliana nami kwa macho, bila kutamka na nilikuwa namuelewa vizuri!!

Jicho hilo silioni siku hizi miongoni mwa akina mama.

Ilikuwa wageni wakija nyumbani, mimi kama narukaruka na kucheza mbele ya wageni bila staha, kulikuwa na namna fulani ya mama kuniangalia ilimaanisha "toka hapa". Nilielewa mara moja na kutii!

Ilikuwa wageni wakila chakula nami kutaka kudowea, basi kulikuwa na uangaliaji wa mama ambao ulimaanisha " ukijaribu tu nitakuchuna ngozi ukiwa hai!" lakini wakati huohuo kwa wageni uso wake ulimaanisha "endeleeni tu, huyu dogo ameshakula."

Ilikuwa mkiwatembelea ndugu na ukataka kulilia kitu cha watu, kulikuwa na jicho fulani hivi toka kwa mama lililoonyesha kuwa "Ukifanya ng'ee tu tukifika nyumbani nitakukaba shingo, sitaki ujinga"

Lakini wanawake wa leo, namaanisha akina mama wa leo ehhh..., vioja. Macho yao yamepofushwa na nini sijui..! Labda ni hizi kope za bandia wanazozivaa au hizi rangi wanazopaka kwenye nyusi!!

Kusema ukweli macho yao hayana mawasiliano na watoto wao.

Wazazi wetu wa zamani, Mungu awajaalie maisha marefu. Ninyi ndo mlitutengeneza tukawa hivi tulivyo leo. Hatuna tamaa ya vitu vya watu.

Nakala:
- Wanaume wote
- Akina mama vijacho wote
 
Macho yao yote wamehamishia kwa smart phone zao yaani hata wakitembelewa na wageni wako bize kwenye simu

Wakisafiri na watoto wako bize kwa simu hawaangalii mienendo ya watoto
Wako bize na simu na huku wakiwafokea wajakazi wao kuwaangalia watoto
 
mbavu zangu eti" ukijaribu tu nakuchuna ngozi"
Tupo wamama wa hivyo, mi wanangu wanaelewa vzr nikimkata jicho anajiongeza mwenyewe maana anajua what next
 
Nilichukua hili jicho kwa mama yangu aisee.

Sometimes siongei mtoto akikutanisha macho yake na yangu tu ataacha ujinga aliokuwa anaufanya.
 
Umeshakuwa sasa, kila ukitazama jicho unakuta anakurembulia.. Ila muulize Dogo taratiibu atakupa stori.

Mi Dogo tunaweza kaa anafanya ujinga wake, mamake akimuangalia tu anatulia mwenyewe afu ananikimbilia. Akati mamake hamna kitu amefanya wala kusema..
 
Jicho analo mdada wa kazi ndugu
Wazazi wenyewe macho yao yapo shilawadu yanaangalia ubuyu

Nilichojifunza hapa ni kuwa kwa sasa mke bora kabisa wa kuoa ni msichana wa kazi. Huyu ukimpata utakua umepata lulu maana anajua kuamka asubuhi na mapema, anajua kuandaa watoto, anajua kusafisha nyumba, anajua kufua, anajua kulisha mtoto, kupika, kuosha vyombo na kazi zote za ndani.
 
Mmeshafanya tafiti kwa wanawake wangapi kujua kuwa hayo macho yamepotea?
Ni hao maslayqueen mnaowabadilisha kila miezi mitatu kama ripoti za robo mwaka au wanawake wepi mnaowazungumzia?
 
Duh mkuu umenikumbusha mbali sana ila ni kweli tulipo na tuelekeapo siko kabisa
 
Heko kwa mama zetu hakika walijua kutulea vyema. Mama yangu hakuwahi kunichapa ila jicho lake lilikuwa likinionya kufanya makosa!
 
Nilichojifunza hapa ni kuwa kwa sasa mke bora kabisa wa kuoa ni msichana wa kazi. Huyu ukimpata utakua umepata lulu maana anajua kuamka asubuhi na mapema, anajua kuandaa watoto, anajua kusafisha nyumba, anajua kufua, anajua kulisha mtoto, kupika, kuosha vyombo na kazi zote za ndani.
Huyo mdada wa kazi nae ukishamuoa jicho litapotea maana naye atakuwa busy kujiremba, kuchat na kuangalia tv
 
Kwangu mtoto akiangalia mustach tu hawezi kuleta matata!
Hapo bado macho kufanya yake.
 
Huyo mdada wa kazi nae ukishamuoa jicho litapotea maana naye atakuwa busy kujiremba, kuchat na kuangalia tv

Hapana mkuu. Inaelekea kuna vitu fulani watu wakijifunza wakiwa wadogo hua hawaviachi. Ndio maana unaona kinamama wengi hapa wanasema jicho walijifunza kwa mama zao. Hata kama atabadilika kidogo hawezi kuwafikia hawa watoto wa saint ambao hata kufua chupi zao hawawezi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom