The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,494
- 2,040
Nikiri wazi kuwa nchi yetu inajichanganya sana kwenye mwendelezo wa uongozi wake. Ukiangalia tunavyoongozwa ni kana kwamba tumeongozwa na vyama tofauti vya kisiasa, wakati inajulikana fika kwamba tangu tupate uhuru tumeongozwa na chama hichohicho, sana sana kilijibadilisha jina.
Takribani Kila awamu imekuja na mtazamo unaokinzana na awamu iliyotangulia, ingawa kilicho nisukuma kuandika hapa ni huu mtiririko unavyokwenda tusipo upatia dawa utatuchelewesha sana kama nchi.
Alipoingia madarakani rais wa awamu ya pili alisema anafungua nchi, akimaanisha aliyemtangulia aliifunga.
Rais aliyemfuatia wa tatu akaifunga tena Kwa miaka yake 10 alipomaliza tu aliyemfuatia yaani rais wa awamu ya nne akaifungua kweli kweli nchi ikawa wazi balaa.
Ndipo akaja huyu wa awamu ya tano huyu ndo alikomesha aliifunga si kuifunga tu yeye aliifungia kabisa, na ni kipindi cha miaka mitano pekee sijui kama angemaliza kumi hali ingekuwaje.
Alipoondoka wa awamu ya tano amekuja huyu wa awamu ya sita naye karudi kuifungua nchi, Kwa dalili za awali za ufunguaji huu unaonyesha ataifungua Kwa kiwango kinachomlazimu anayemfuatia aifunge tena.
Huu utaratibu utatuchelewesha sana inamaana nchi yetu itakuwa maarufu sana Kwa kufunga na kufungua nchi.