Hili jambo la wazazi kukataa wapenzi wa mabinti zao!

Fedha na mali ni kitu ambacho mzazi aweza kumrithisha mwanae, ila mke au mume mwema, atoka kwa BWANA.

Source: Biblia Takatifu
Umetoa summary nzuri. Unaweza kumpa mtoto mali na elimu, lakini mume/mke bora ni zawadi. Wengi wanalia japo wamechaguliwa wake/waume na wazazi wao...
 
Mzazi anamchango mkubwa katika kutoa ushauri kama niliyemleta anafaa au vipi.
Japo anatakiwa anipe sababu za kwanini anamuona huyo mtu hafai ili na mimi nijiridhishe.Ila hii inaaply sana kwa wale wachumba ambao mzazi anakuwa anamfahamu kwa muda mrefu akimwona akikua au akiwa anaendesha maisha yake kwa kipindi fulani.
Kuna nilichojifunza kupitia ndugu yangu wa karibu hasa katika kushauriwa kuwa nani anafaa au hafai.
Kwa shida aliyoipitia huyo ndugu yangu mzazi akinishauri namsikiliza kwakweli mana nimeshuhudia.
 
Love at first sight,daah mpe pole ndugu yako maana namfahamu mamii.
 
Matatizo ya kupata konkasheni utotoni...Kwann uharibu thread ya mtu...?

Umamfahamu Mtambuzi kweli wewe...? Hebu angalia profile yake ungalie mada zake...? Kwataarifa yako huku watu wenye vi-blog uchwara ndio wana-copy na Ku-paste...
 
hii ilinitokea miaka kadhaa nyuma.. moyo ulivunjika, nilisikitika sana kipindi hicho. Ila sasa nimekua, nadhani nawaelea zaidi wazazi sasa kuliko kipindi kile nimezibwa macho na mapenzi. Nakumbuka zaidi baba alikuwa hataki kumsikia kabisa, na mama pia lakini mama alijitahidi kuonesha kuwa upande wangu ingawa nilijua kabisa na yeye haimpendezi lakini ili kunifanya nisijisikie vibaya alionesha kunikubalia hali anajua na mimi nilijua kabisa hamna ambacho kingebadilika maana nilikulia kwenye familia ambayo msemaji wa mwisho ni baba na hamna namna yoyote wa kubadilisha maamuzi yake, akisema, amesema..it's final.
Mara nyingine wazazi wanakuwa wapo sahihi, ni vizuri kutuliza akili na kutafakari kwa makini na kwa mtazamo wao pia
 
Mimi ingawaje walinikubalia ila walipoteza imani kubwa niliyokuwa nayo kwao. Walisema mahitaji yao nami nilikuwa bint mtiifu. Ilipofika wakati wakutimiza ahadi zao waliniumiza.

Wazazi mtimize ahadi kwa watoto wenu. Sitamani wadogo wangu wapitie uzoefu huo.
Usiku ule sauti ya baba kuwa hataniuza ilijirudia mara nyingi nililia kama nimepigwa, gafla kutoka mtoto wao mpendwa nilikuwa mali nalinganishwa na ng'ombe na ada walizonilipia.

Thanks kwa mdogo wangu wakiume alipoingilia kati na kuwambia wakumbuke ahadi zao wakaona haya.

Huwa sipendi kuliongelea hili ila kwa wale wazazi wenye watoto msiwaahidi ahado ambazo mnadhani hamtatekeleza.
 
Wazazi wanayohaki ya kumchagulia mume mtoto wao, wazazi hawawezi kukuchagulia kibaya na pia ni vyema kupata baraka za wazazi unapoingia katika ndoa. Wazazi wameshapitia maisha ya ndoa na wanajua changamoto za ndoa na mapungufu ya mtoto wao tangu utotoni hivyo ni vyema wakuweke katika mikono sahihi.
Baba yako alichaguliwa mke na nani?
 
Mimi ingawaje walinikubalia ila walipoteza imani kubwa niliyokuwa nayo kwao. Walisema mahitaji yao nami nilikuwa bint mtiifu. Ilipofika wakati wakutimiza ahadi zao waliniumiza.

Wazazi mtimize ahadi kwa watoto wenu. Sitamani wadogo wangu wapitie uzoefu huo.
Usiku ule sauti ya baba kuwa hataniuza ilijirudia mara nyingi nililia kama nimepigwa, gafla kutoka mtoto wao mpendwa nilikuwa mali nalinganishwa na ng'ombe na ada walizonilipia.

Thanks kwa mdogo wangu wakiume alipoingilia kati na kuwambia wakumbuke ahadi zao wakaona haya.

Huwa sipendi kuliongelea hili ila kwa wale wazazi wenye watoto msiwaahidi ahado ambazo mnadhani hamtatekeleza.
Pole sana na wewe utakuwa mzazi somo la mtambuzi lina mafunzo mazuri
 
Wazazi/wazee wanaangalia mambo mengi na kuyafuatilia pamoja na historia ya mwanaume na ukoo wake.
*magonjwa ya kurithi
*tabia halisi ya ukoo na mila zao
*ushirikina/unyanyasaji/ migogoro ya mali na urithi.
--ndoa zinachangamoto nyingi sana ni vyema kupata baraka na radhi za wazazi
Siku hizi wanafuatilia hilo?
 
hii ilinitokea miaka kadhaa nyuma.. moyo ulivunjika, nilisikitika sana kipindi hicho. Ila sasa nimekua, nadhani nawaelea zaidi wazazi sasa kuliko kipindi kile nimezibwa macho na mapenzi. Nakumbuka zaidi baba alikuwa hataki kumsikia kabisa, na mama pia lakini mama alijitahidi kuonesha kuwa upande wangu ingawa nilijua kabisa na yeye haimpendezi lakini ili kunifanya nisijisikie vibaya alionesha kunikubalia hali anajua na mimi nilijua kabisa hamna ambacho kingebadilika maana nilikulia kwenye familia ambayo msemaji wa mwisho ni baba na hamna namna yoyote wa kubadilisha maamuzi yake, akisema, amesema..it's final.
Mara nyingine wazazi wanakuwa wapo sahihi, ni vizuri kutuliza akili na kutafakari kwa makini na kwa mtazamo wao pia
Chujio, kwa case yako unaamini wazazi walikuwa sahihi?? Kwa nini unadhanib walikukataza usiolewe na huyo kijana?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom