Hili Halijapata Ufumbuzi kuhusu Ununuzi wa Vitu kwa Njia ya Mtandao (Online Purchase)

Navyojua vitu ambavyo serikali inavipa kipaumbele ni Kilimo,Elimu na Afya

Hivo material iliyo related na Elimu e.g Tablet na laptop,Kilimo e.g Mbegu au tractor na vitu vya afya e.g Stethescope/thermometer etc havitozwi ushuru hivi hivi nsijue kama umenunua kibiashara e.g 10pcs za Tablet hapa wanaweza kukutoza ila for personal use au instituon use havitozwi

Wameelezea kwenye tovuti ya TRA lkn sidhani kama simu ina qualify by any means kuwa educational material ndo maana watu wanapigwa kodi

so kwa mfano kama ni simu inatakiwa kulipiwa asilimia ngapi ya bei
 
Nakushauri usiagize kupitia DHL maana hao wako proved wana njaa sana
18% VAT
10% Custom duty

Hivo simu ya 300$ itakua (300*.18)+(300*.10)

Mkuu mimi nataka niagize tv moja tu vipi kwa uzoefu wako hii nayo watanitoza vat? njia nafuu kwa mzigo kama tv ya inch 39 -42 ni ipi?
 
Mkuu mimi nataka niagize tv moja tu vipi kwa uzoefu wako hii nayo watanitoza vat? njia nafuu kwa mzigo kama tv ya inch 39 -42 ni ipi?

Wala siwezi na sitojaribu agiza TV kutoka nje
Unaweza agiza DHL/FEDEX na UPS zitakusaidia na VAT na CUSTOMY DUTY ni must
 
ANGALIZO KWA WANAO AGIZA BIDHAA TOKA NJE YA NCHI
  • Nimeagiza mzigo toka USA na umesafirishwa na hawa TNT
  • Ghalama zao walizonipa ili mzigo utoke, zimenishangaza, ni kubwa kuliko makampuni yote niliyowahi kutumia kuagiza mzigo toka nje ya nchi.
  • Nimefanya mazungumzo na mhusika kwa njia ya simu na akasisitiza hata kama ni mzigo wenye thamani ya DOLA 1 hizi kwenye picha ndio ghalama nitakazopaswa kulipia. Tazama picha
1570179194022.png
wp_ss_20151113_0004.png
Kwa Ufupi
- Mzigo nilio agiza una thamani ya dola 162.97
- Shipping cost dola 44

Je ni sawa kweli?

Ndugu Brakelyn tafadhali nipe uzoefu wako mzigo wako ulipo kuja kwa TNT ghalama zilifanana na hizi nilizopewa?

Bado natafakari nini cha kufanya kuhusu hatma ya huu mzigo

Nawakilisha
 
Last edited by a moderator:
ANGALIZO KWA WANAO AGIZA BIDHAA TOKA NJE YA NCHI
  • Nimeagiza mzigo toka USA na umesafirishwa na hawa TNT
  • Ghalama zao walizonipa ili mzigo utoke, zimenishangaza, ni kubwa kuliko makampuni yote niliyowahi kutumia kuagiza mzigo toka nje ya nchi.
  • Nimefanya mazungumzo na mhusika kwa njia ya simu na akasisitiza hata kama ni mzigo wenye thamani ya DOLA 1 hizi kwenye picha ndio ghalama nitakazopaswa kulipia. Tazama picha
wp_ss_20151113_0004.png
Kwa Ufupi
- Mzigo nilio agiza una thamani ya dola 162.97
- Shipping cost dola 44

Je ni sawa kweli?

Ndugu Brakelyn tafadhali nipe uzoefu wako mzigo wako ulipo kuja kwa TNT ghalama zilifanana na hizi nilizopewa?

Bado natafakari nini cha kufanya kuhusu hatma ya huu mzigo

Nawakilisha

pole sana [HASHTAG]#Mwl[/HASHTAG].RCT ,

hili ni jambo muhimu sana kuzingatia wakati wa kuagiza mzigo kutoka nje. Mimi pia nilishapatwa na wakati huu mgumu kama wako na nikagundua yafuatayo. Mpaka sasa nina uzoefu wa miaka 6 kufanya online shopping kupitia website mbali mbali zinazouza bidha mbali mbali.

Njia za usafirishaji ninazotumia kusafirisha mizigo yangu kutoka nje

Mara nyingi kuwa nachagua mizigo yenye njia ya usafirishaji ninayopendelea zaidi otherwise huwa nawaomba sellers wanitumie mizigo kupitia Courier companies ninazotaka. Mimi huwa ni mvumilivu, naweza kusubiri hata siku 45 ilimradi nipokee mzigo kwa gharama kidogo. Mizigo mingi napendelea itumwe kwa USPS, Royal Mail, EMS, Austr.Post, Singapore Post, China post (baadhi zinaangukiwa kwenye economy Int'l na Standard Int'l Shipping) etc (hizi zote huniwezesha mimi nipokee mizigo kwa njia ya sanduku langu la posta ). Huko posta mzigo ukifika tu, nitakacholipa ni ushuru pekeyake tena kwa mizigo ambayo iko subjected to Customs Duty. Hii inanipa unafuu kwasababu kuna mizigo mingi midogo hailipiwa ushuru, vile vile naokoa gharama za clearing, sjui tbs, clearing etc. ambazo zinaongeza gharama ya mzigo wako. Vile Vile naweza kuongea na muuzaji huko nje akapunguza value ya invoice kwenye parcel na ikanipunguzia gharama ya ushuru pale itakapofika posta (japo ni illegal).

Uzoefu wangu na hizi express shipping companies (DHL-FedEx-UPS-TNT etc)

Mpaka sasa nimeshatumia DHL,FedEx na UPS.

Experience na FedEx.
FeDeX niliitumia kuingiza simu yenye thamani ya $200 mwaka juzi na sikulipishwa ushuru. Sijawahi kutumia tena FedEx hivi karibuni.

Experience na UPS
UPS nimepokea mzigo mara moja tu na sintorudia tena kutumia UPS kwa sababu zifuatazo. Mzigo ulikuwa na thamani ya $65 na bei ya usafirishaji ilikuwa $420.22 labda sababu ya uzito wa mzigo (Nilinunua kwasababu hata jumla ya gharama haikufikia bei ya dukani huku Arusha).

image.jpg


baada ya mzigo kufika JKN Int Airport Dar, customer service wa UPS wakanipa computation za kufanya clearance ya mzigo wangu na ilikuwa kama ifuatavyo:

1. Ushuru 112,000/=
2. Handling 30,000/= (wakaniambia eti TBS)
3. Handover fee 57,000/=
4. 80,000/=

Screenshot_2015_11_14_06_53_33.png


Total ikaja kama 279,000/= hivi. Nikalipa tu sababu nilikuwa nikiuhitaji sana.

Experience na DHL
Nimepokea mizigo mara nyingi sana kupitia DHL. Hivi karibuni nimepokea mzigo wenye thamani ya $150 na nimechajiwa ushuru wa shilingi 115,000/= tu ofisi za DHL Arusha na nikapokea mzigo wangu.

Screenshot_2015_11_14_06_50_18.png


Huu mwingine una thamani ya $200 na juzi dhl wanipa estimation za ushuru wa 141,800/= kutoka customs. Hivi sasa navyoReply post yako nipo njiani kuelekea DHL kuupokea.

Screenshot_2015_11_14_06_48_36.png



Experiance na TNT bado ili nashukuru sana kwa kunipa experience yako. kwahyo TNT ni kama hawa UPS tu. Umenisaidia nimewaongeza kwenye blacklist yangu.

Conclusion yangu ni kwamba, baadhi ya hizi kampuni za usafirishaji za nje zimekuwa na gharama zisizo na maana kabisa. Unakuta mizigo ni ya aina moja na ina thamani, uzito, dimension za package ni hizo hizo lakini ukipokea kupitia courier companies tofauti unapata gharama tofauti za ukomboaji. Nachoamini kwa mizigo midogo midogo hakuna haja ya kulipa clearing fee, handling, sjui handover fee. Maranyingi naagiza spare mpya za magari kupitia DHL na ni nzito, thamani kubwa kuliko hiyo nilipitisha kwa UPS lakini bado napata unafuu kuingiza kwa DHL. (TBS costs bado sijajua DHL wanakwepaje) lakini so far naona ndio courier company inayoeleweka kwangu mpaka sasa kwasababu gharama nayolipa kwao ni ya ushuru tu.
 
Kwa #1 na #2
  • Tumia United States Postal Service USPS mizigo yote utaipokelea Posta [ kwenye P. O. Box yako uliyojaza ]
  • Shipping cost ni ndogo
  • Itafika bila shaka yeyote
  • Utapewa tracking No.
  • Mzigo utaupata baada ya siku 14 - 21
Kwa #3
  • Fanya mawasiliano na omba wakusafirishie kwa ARAMEX
  • Mzigo utafika dar ndani ya siku 5-8 za kazi
  • Ila hakikisha anakuwepo mtu dar wa kukuchukulia, ili akutumie huko uliko kwa basi
  • Utapokea mzigo bila ya kuwepo kwa usumbufu wowote kama ilivyo kwa DHL
Njia zote tajwa hapo nimezitumia
Kama huna P.O.Box je?
 
Mm naagiza mzigo kila kukicha toka china lakini sijawahi kutana na mambo haya. Nikilipa sana ushuru ni buku 5 pale postal
 
Nitajuaje kama mzigo wangu umefika posta wakuu? Au inabidi nitembelee sanduku langu kila wakati?
 
mfano nimeagiza simu 1 kutoka china halaf wameniandikia kuwa ni free shiping tofauti na gharama za hyo cm kuna gharama yoyote nitakayohitajika kulipa?
 
Nitajuaje kama mzigo wangu umefika posta wakuu?
Utajua kupitia tracking number uliyopewa.
Ingiza tracking number kwenye hii link: http://41.59.0.101:1120/tracking/

Au inabidi nitembelee sanduku langu kila wakati?
Iwapo mzigo hauna tracking number basi ni vyema mara kwa mara kufika posta, zile tarehe za makadirio ya zigo kufika.
Pia kwa mzigo ambayo imekaa kwa muda mrefu bila kuchukuliwa, Posta huwa wanautaratibu wa kupiga simu kumjulisha mteja husika kufuata mzigo wake.
 
Back
Top Bottom