zegamba180
JF-Expert Member
- Oct 8, 2014
- 818
- 536
Najua wapo baadhi mtakwazika na andiko langu, ndio ukweli wandugu. Kanisa Katoliki linaendeshwa katika misingi ya umoja na nidhamu(unyenyekevu) ya hali ya juu. Ndio maana tunasema kanisa mojatakatifu katoliki la mitume. Ibada zote zipo katika kalenda Dunia nzima. Ni jambo jema sana kuwa na umoja usiogawanyika.
Toka wamisionari wasitishe misaada Afrika Kanisa limekuwa likijiendesha lenyewe kwa sadaka za waumini na wenye mapenzi mema. Sasa katika kuongeza kipato kanisa katoliki limekuwa likijenga Shule na Hospitali. Ukweli ni kwamba wanaochanga kufa na kupona ama kwa jasho ni waumini wa parokia husika. Kupitia Jumuiya zao.
michango shirikishi;
Bila kujua kipato wala idadi ya wanajumuiya, tunapangiwa kiasi sawa na jumuiya nyingine. Hata kama jumuiya yetu tupo waumnini(kaya) hai 10 tu. Jumuiya nyingine wapo waumini zaidi ya 30, nyingine 50. Tunune ama Tunung'unike tutatoa Tsh 1500,000 kwa idadi ya kaya 10, kwa kiasi cha Tsh 150,000 kwa kaya kila baada ya miezi 3. kwa kila mmoja kuchanga 150,000. Jamani wapo watu kwa mwezi mshahara wake haufikii hicho kiasi. kwa mwaka huyo muumini anapaswa kuchanga Tsh 600,000. Wenzetu walio 40 watachanga Tsh 37500 kwa kaya kila baada ya miezi 3. Kosa Paroko na Viongozi wake wamekosa ubunifu.
michango mingine itaendelea tu;
Huku harambee ya ujenzi wa shule ikiendelea kuna michango mingine nayo inaendelea utasikia ujenzi wa choo, ujenzi wa goroto, kapu la paroko n.k. Naposema kosa ni kwamba Paroko na kamati yake wameshindwa kujua kipaumbele nini kwa wakati husika. Viongozi wanakosa ubunifu wamejawa na kiburi. Mbaya zaidi kushindwa kwao kutoa elimu ya kutosha ya utoaji, ili wale matajiri watoe zaidi.
Viongozi wangu wapendwa nimeonekana mkorofi kwa kuhoji juu ya hili mara nyingi sana. Kosa Paroko na Viongozi wake hawana huruma kwa waumini wao.
Ubaguzi wa wazi unaanza;
Tumechanga wote kwa kupangiwa kiasi sawa. wanajumuiya masikini tumejibana hadi akiba ya mwisho. Shule ikiisha fomu 10,000. Ada kwa darasa la awali Tsh 700,000 kwa kuanzia. Primary Tsh 1200,000 na kuendelea. Ipo wapi nafasi ya mtoto wa mwanajumuiya masikini mimi??? Niliyeundiwa kamati ndogo kunipitia na kuhakikisha natoa mchango wa ujenzi wa shule?!! Nakuapia hakuna nafasi ya punguzo la ada kwa wanajumuiya masikini tuliochanga kwa jasho achilia mbali kusoma bure watoto wetu. Wanakuja kusoma watoto wasiochangia.
Kuisha kwa shule si kwamba kutaleta unafuu kwa waumini kama walivyoelezwa awali, michango itaendelea. Tutachangishwa tu. Ama pata shida nenda kaombe msaada utaambiwa hakuna pesa. mara ngoja viongozi watakaa na kujadili ombi lako. una shida kwa wakati huu mpaka viongozi wakae? Lini? Najiuliza mapato ya shule yanatumikaje? Nawaomba wanaJF wenzangu tukemee tunapoona mambo yasiyofaa makanisan kwetu. Ni bora useme ukweli ukatengwa kuliko kunyamaza kinafiki.