Hili Gwaride la utambuzi kwa watumishi wa serikali, siliafiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili Gwaride la utambuzi kwa watumishi wa serikali, siliafiki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bi. Kiroboto, Jan 10, 2012.

 1. Bi. Kiroboto

  Bi. Kiroboto Member

  #1
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tangu mwaka jana kumekuwa na taarifa kwamba serikali inafanya utaratiwa utakaoiwezesha kudhibiti ulipaji mishahara kwa watumishi hewa. Njia pekee na rahisi iliyokusudiwa kutumika ni kupanga siku ambapo watumishi wote watatakiwa kufika katika maeneo yao ya kazi. Itakuwa ni mwisho wa mwezi ambapo watumishi watapokelea mishahara yao ofisini kwa mwajiri wao badala ya pesa kuingizwa ktk akaunti zao; ni kwa utaratibu huu ambapo mtu/watu maalum watakuwa wanaorodhesha watumishi wote ambao watapana nafasi ya kuhudhuria kusanyiko hili. Haijaeleweka vizuri kwa watumishi wote iwapo zoezi hili litaanza na kumalizika lini. Binafsi mimi nimeongea na mwajiri wangu na amenidhibitishia kuwa ameishapokea barua kutoka wizarani na kwamba zoezi hili litafanyika hapa halmashauri kwetu mwishoni mwa mwezi huu(Jan). Binafsi, siungi mkono malipo kwa watumishi hewa. Ila tatizo langu lipo kwenye gharama na usubufu ambao baadhi ya watumishi watapata.Kwanza haijaeleweka zoezi hili litadumu kwa muda gani. Kinachofahamika ni kwamba endapo mtumishi atashindwa kuhudhuria zoezi hili, mshahara wake utasitishwa na atalazimika kufuatilia kwa gharama zake mwenyewe hadi hazina kuu ili kurejeshewa. Haijafahamika iwapo kutakuwepo na faini yoyote kwa wale watakaoshindwa kutekeleza kwa wakati zoezi hili au utaratibu utakaotumika ili kuwarejeshea tena ujira wao.Pili haijafahamika iwapo serikali itafidia gharama na usumbufu kwa baadhi ya watumishi wake waliopo likizoni, safarini, masomoni na baadhi ambao kwa bahati mbaya wakati wa zoezi hili watakuwa wagonjwa(mahututi) vitandani. Nimefikiria mtumishi ktk halmashauri ya wilaya Mafia ambaye yuko likizo Bukoba, mwenye mshahara wa Tsh 250000/= Na vipi mtumishi wa kipato kama hicho aliyefuata taratibu zote na kufanikiwa kwenda masomoni let's say Arusha wakati yeye anafanya kazi Mafia au Tandahimba. Ikubukwe kwamba tuna watumishi wengi sana wanaojisomesha kwa gharama zao wenyewe baada ya waajiri wao kuwaruhusu na kusema hawana hela ya kuwasomesha. Sitaki kuamini kwamba serikali hailitambui hili. Kimsingi kinachoonekana hapa ni kwamba mwanzo serikali imeishakiri kushindwa kudhibiti tatizo hili la watumishi hewa kwa kutumia utaratibu uliokuwepo miaka mingi. Sasa imeamua kumtwisha zigo mtumishi aliyejitolea kufanya kazi ktk mazingira magumu ambayo wengine wameyakimbia na ndio hao wanaoitwa hewa! Kwamba mtumishi wa Halmashauri ya wilya Mafia ambaye yupo masomoni Kilimanjaro atumie zaidi ya Tsh 200,000/= kusafiri kuja kusaini cheki ya Tsh 250,000/=??! This is nonsense. Hii ina tofauti gani na adhabu ya kawaida? Huyu mtumishi masikini kaikosea nini serikali yake? Mimi naona kosa lake ni pale alipokubali kufanya kazi katika mazingira ambayo wengine(wajanja) wamekimbia.Lakini, ndio tuamini kwamba serikali imekosa njia nyingine ya kudhibiti tatizo hili hadi imeamua kugawana zigo hili na watumishi wake-tena waaminifu kabisa? Je, tuamini kuwa hii ndiyo suluhu ya kudumu kwa tatizo hili? Je, haitakuja kuwa routine kila baada ya miaka kadhaa? Ushauri wangu kwa serikali, naamini inatambua adha ambayo baadhi ya watumishi watapata kutokana na zoezi hili, ijaribu kutumia njia mbadala ambayo haitaleta usumbufu kwa watumishi wake. Itazame gharama, usumbufu na muda atakaopoteza mtumishi wakati wa zoezi hili. Lakini pia itambue kuwa vyovyote itakavyokuwa bado lazima kutakuwepo na watumishi kadhaa watakaoshindwa kuhudhria zoezi hili. Fikiria mtumishi aliyelazwa mahututi hospitali, sina hakika ana nafasi gani ktk zoezi hili.Mimi nadhani serikali ni taasisi kubwa, ina uwezo mkubwa. Kwani inashindikana vipi hao watu watakaohusika na uhakiki huu ktk taasisi fulani kushugulikia watumishi wote bila kujali wanatokea wapi. Naamini siku hizi kuna maendeleo makubwa katika information technology. Watumishi wote wa serikali wamo kwenye database, sioni mantiki ya kunisafirisha kutoka Musoma kwenda Tandahimba kuhakikiwa ilhali nina kitambulisho na nyaraka zote muhimu za kiofisi zinazohalalisha uwepo wangu pale Musoma.Kama huamini fuatilia kwa muajiri wangu. Kwa mfano, ina maana serikali haijui idadi ya watumishi wao waliopo masomoni na vyuo walivyodahiliwa? Inashindwa vipi kuwahakiki huko waliko? Mimi nadhani umefika wakati iheshimu maslahi kidogo wanayopata watumishi wake. Sipendi kuona zoezi hili limekamilika likiwa limeacha mifuko ya watumishi mitupu.Hii haina tofauti na kulipia haki ya msingi ya mtumishi. Ningependa kuona zoezi hili likifanyika kwa utaratibu ambao utakuwa wa kudumu na njia ya kuhakiki watu iwe ya kisasa zaidi sio ya namna hii vijana wa kileo wanaita kuuza sura. Sipendi kuona zoezi hili muhimu kuendeshwa kwa zima moto.Mungu ibariki Tanzania...
   
 2. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,357
  Likes Received: 2,986
  Trophy Points: 280
  Najaaa.
   
 3. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  National pay day hiyo!aliiongea mkulo kwny bajeti nilidhami wanatania kumbe kweli wezi watakamatwa tuuu hapo!
   
 4. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hope something went wrong wakati naisubmit, it wasn't my fault ndugu yangu.
  However, kama umeelewa ujumbe you could say something wealth than this,huh!
   
 5. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  kwahiyo national payday tutakuwa hatuendi kazini ili watumishi wa uma wapate mishahara? bora wafanye ivyo ili wale tunao wadai iwe rahisi kuwabana
   
 6. Bi. Kiroboto

  Bi. Kiroboto Member

  #6
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hey, mrimi, umetumwa?
  Mbona nakuPM hata hujibu. Wht's wrong wit yu guy?
   
 7. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #7
  Jan 10, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu, I share your concerns but unfortunately akili ya watawala wetu ndio imeona kuwa hiyo ndiyo solution! Na hii ni reflection ya utawala wao,. WATANZANIA TUAMKE. TUCHUKUE HATUA KWA MANUFAA YA SISI WOTE NA VIZAZI VYOTE VIJAVYO!
   
 8. Bi. Kiroboto

  Bi. Kiroboto Member

  #8
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi kiukweli sioni kama zoezi hili ndio muarobaini wa tatizo, maana watapita mara moja wataondoka. Kusema kweli chanzo cha wafanyakazi hewa ni wakuu wa halmashauri na taasisi mabalimbali, sio wafanyakazi wenyewe. Kimsingi serikali ilitakiwa kuwabana hao na sio kuwatwisha wafanyakazi zigo hili. So long as maafisa utumishi, wakurugenzi na wakubwa wa hazina ni walewale mimi naona kama ni kanyaboya tu watumishi tunachezewa hapa.
   
 9. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  Binafsi sikubaliani na mfumo huu kwani utaleta usumbufu,gharama,dhulma na social&family disputes! Hwever kwa kuwa 'wababe' mmeshadhamiria kufanya hivyo,ningependa kupata majibu ya maswali yafuatayo: 1. Kwa kuwa kila mtumishi wa umma yuko chini ya mamlaka husika(wizarani-k/mkuu,halmashauri-DED, Wakala/Idara/mamlaka-DG), je serikali itachukua hatua gani kwa mkuu wa mamlaka husika aliyekuwa akiwasilisha ji/majina ya ghost workers pale itakapobainika? 2. Je watumishi walio masomoni nje ya nchi kwa ufadhili wa wahisani/yeye mwenyewe hali ya kuwa anategemea mshahara wake ili aweze kujikimu kimasomo au ili familia yake iliyo tz iweze kujikimu? 3. Na ikiwa masomo yake huko nje ni 5yrs,ni nani atakayefuatilia huko hazina ili kupata uhalali ili 'mayai' yake huko hom yasioze? 4. Je tatizo la ghost workers liko pia ktk sekta binafsi?if no wanatumia njia gani kulizuia?if yes na wao wana private pay day? 5. Hapo kabla mfumo huu wa dirishani ndo ulikuwa ukitumika,je kuna literature yyte inayoonyesha kuwa tatizo la ghost workers halikuwepo?
   
 10. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Kwa ajili ya kuhalalisha na kulinda maslahi ya ajira yako kama mtumishi wa serikali inabidi utii amri tu. Yote uliosema sahihi lakini lau ungepata msiba utatoka huko ulipo uje nyumbani kuwa na nduguzo wakati wa huzuni. Hivyo basi zoezi hili ni la mara moja au mbili katika kipindi chote cha kuajiriwa hadi kustaafu tunaliona kuwa tatizo. Ama ndio miongoni mwa madudu hewa munaoinyonya serikali kila mwezi? Atakaekuwa na udhuru wa kweli na kueleweka baada kujieleza mbona hawatadhulumiwa haki zao. Kuwa mstaarabu siku hiyo uende ukahakikiwe.
   
 11. Bi. Kiroboto

  Bi. Kiroboto Member

  #11
  Jan 11, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu unaonaje kama ungetuhakikishia ikiwa hili zoezi la zima moto la mara moja au mara mbili kwa kipindi chote cha utumishi litadhibiti kabisa uwepo wa wafanyakazi hewa.

  Kwa ufahamu wako unataka tuamini kwamba tatizo lipo kwa wafanyakazi wa kawaida, sio maofisa wa wanaoshughulikia ajira eg. maofisa utumishi wakurugenzi nk. ndio mana unathubutu kuwaita watumishi madudu hewa. Umesahau kuwa hawa watakaopata adha hii ni wale waliojitolea kufanya kazi ktk mazingira magumu ambayo wengine wameshindwa wakakimbia.

  Unaonaje kama ungetuthibitishia hapa jinsi gani mtumishi wa kawaida ambaye akiajiriwa analazimika kukaa kazini hadi miezi sita au zaidi kabla ya kuingia kwenye payroll anavyoweza kuwa mdudu hewa? Ningeridhika sana kama ugeweza kutuonesha hapa namna gani huyu mtumishi wa kawaida anavyoweza kulipwa mshahara pasipo kufanya kazi, na kama ikitokea hivyo uzembe umetokea kwa nani?

  Naona kama ni kituko kufananisha msiba na matokeo ya uzembe wa watu wachache ofisini wasiotekeleza wajibu wao? Umesema watumishi wenye sababu za msingi, sijakuelewa vizuri ndugu yangu. Katika baadhi ya sababu zilizotolewa hapo juu wewe umeona ni sababu gani isiyo ya msingi? Je, ni watumishi ambao kwa bahati mbaya watakutwa mahututi vitandani? Je, ni wale walioko safarini pengine nje ya nchi kikazi au kwa matibabu? Na vipi utaratibu gani umewekwa kushughulikia madai ya hao watumishi uliosema wenye udhuru wa kueleweka ambao hautakuwa na usumbufu? Let's think big my dear.

  Hakuna mtu anayetetea malipo kwa wafanyakazi hewa hapa, kinacholalamikiwa hapa ni utaratibu unaotumika ni wazi kabisa utaleta adha kwa watumishi ambao kimsingi sio kosa lao. Inawezekana isionekane kama ni tatizo kwako pengine wewe zoezi hili litakukuta kituoni kwako, au labda wewe ni miongoni mwa wateule hao wachache waliochotewa mihela kwa ajili ya kufanya uhakiki huu, au pengine wewe ni miongoni mwa wale wenye mishahara minono na posho kibao- so huwezi kuhisi machungu yanayomkabili huyu mwalimu atakaye tumia gharama mara mbili kuja kusaini cheki ya 250,000/=

  Let's be serious jamani. Hili jambo ni mzigo kwa watumishi wa kawaida.
   
 12. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Wanaotafutwa hapa ni watumishi hewa. Baada ya kubainika basi wahusika wa ngazi za juu yao ndio watakaowajibishwa. Hili ni dola sio utendaji kama wa watumishi wa majumbani au vibarua usiokuwa na mipango.
   
 13. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,120
  Likes Received: 6,604
  Trophy Points: 280
  Tena kwetu ni jpili inawezekana hata tukashindwa kwenda church.
   
 14. C

  Chaldmhola Member

  #14
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ukweli ni kwamba, utambuzi unafanywa kwenye maeneo yao ya kazi (physically), zoezi hili linaendelea hivi sasa. Kwa wasiokuwepo kwa sababu yoyote ile, mafaili yao yatatumika kuwatambua. Baada ya utambuzi, mishahara italipwa kupitia benki na siyo dirishani.
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Mbona taarifa yako ni tofauti na wafanyakazi waliyopewa??
   
 16. Bi. Kiroboto

  Bi. Kiroboto Member

  #16
  Jan 11, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mkuu hapo ni wapi zoezi hili linafanyika? Hilo ni jambo la heri kabisa hata mimi naliunga mkono 100%.
  Lakini taarifa rasmi kutoka kwa mwajiri wangu inanitaka kurudi ktk kituo changu cha kazi tarehe za mwisho wa mwezi huu kwa ajili ya zoezi hili. Na hii sio kwangu tu, bali na watumishi wenzangu tunaofanya kazi ktk halmashauri moja wote wameishapatiwa taarifa hiyo.
   
Loading...