Hili agizo linatolewa mara ngapi?

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,240
Kikwete alilitoa alipoingia tu madarakani. Lowassa akalitoa mara kwa mara. Mama Sitta naye alilitoa mara kadhaa. Shein naye amelitoa tena. Lini litatekelezwa kwa ukamilifu wake? Kama vyombo vya dola vinashindwa kukamata hata wanaotia mimba wanafunzi ambao wanajulikana na wanaendelea kutamba mitaani vitaweza kweli kuwakamata mafisadi ambao wengine wameshakimbia nchini ama kuwauzia ufisadi wao watu wengine?

Shein aagiza wanaowatia mimba wanafunzi wakamatwe
Makubo Haruni, Musoma
Daily News; Sunday,March 02, 2008 @00:04

Habari nyingine
Watoto 11, 000 wa mazingira magumu wasaidiwa

Majambazi Geita walazimisha mwanakijiji awaonyeshe matajiri
Askofu wa Cantebury ampa kazi nzito Mtetemela
Wachimbaji wadogo Mara kutengewa maeneo
Kata 20 zafikiwa na mradi wa Ukimwi
Mapadri watakiwa kuwa kioo cha jamii
Uzembe wa wakili waiangamiza TanRoads
Naibu Waziri asikitishwa na mafisadi MSD
Mwekezaji Mponde aomba msaada kwa Waziri Msolla

MAKAMU wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein amewaagiza viongozi wa serikali mkoani Mara kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wanaume ambao kwa makusudi wanawapachika mimba au kuwaoa watoto wa kike na kuwakatisha masomo yao.

Alilitoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara mjini Musoma uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Issa Machibya, kusoma taarifa kuwa wanafunzi wa kike 207 mkoani hapa kwa mwaka jana hawakuhitimu elimu ya msingi na sekondari kwa kutiwa mimba.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa kati ya wasichana hao 73 ni wa shule za msingi huku 134 ni waliokuwa wakisoma sekondari na kwamba waliowapa mimba wamefikishwa mahakamani.

Kutokana na hali hiyo Makamu wa Rais aliagiza kushughulikiwa wanaowapa mimba, kuwaoa na kuwabaka akisema kuwa wanawaua katika elimu wasichana hao na kuwafanya kuwa masikini kitendo ambacho alisema hakitafumbiwa macho .

Alisema kuwa wazazi wamekuwa wakijinyima na kutoa mali zao kwa ajili ya kuwasomesha lakini wanakatishwa tamaa kwa wasiopenda maendeleo, wenye tamaa ya mwili kuwakatishia maisha kwa kuwapa mimba katika umri mdogo.

Dk. Shein, alielezea kuwa serikali katika bajeti yake ya 2007/2008 ilitenga zaidi ya Sh trilioni 1.18 kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu nchini na kwamba Mkoa wa Mara kwa mwaka huu umepata Sh milioni 976 kwa ajili ya uchangiaji wa ujenzi wa sekondari, huku wananchi nao wakichangia kutoa elimu bila ubaguzi.

Aliitaka pia jamii kukataa kwa nguvu zote uharibifu wa watoto wa kike kwa vile nao wanahitaji haki ya kupata elimu ili waingie kwenye ushindani wa kidunia wa sayansi na teknolojia.

Hata hivyo alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Nne inaendelea kuboresha maisha ya Watanzania kwa kuweka kipaumbele katika kuendeleza kilimo chenye tija kwa kutoa ruzuku ya mbole, utoaji wa mbegu bora ambako kwa sekta ya kilimo pekee serikali imetenga Sh bilioni 379 sawa na asilimia sita ya pato la Taifa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Wizara ya Kilimo na Chakula imetoa tani 508 za mbolea na tani 75 za mbegu ya ruzuku kwa ajili ya wakulima na kwamba kwa upande wa zao la pamba wakulima wameuza tani 1,312,300 na kujipatia Sh bilioni 6.5.

Machibya alisema kuwa Mkoa wa Mara hususan Wilaya ya Tarime, uwanda wa juu umeanza kilimo cha chai ambako wakala wa wakulima wa chai Tanzania wametoa miche 8,000 ya zao hilo na itakapopandwa kiwanda kitajengwa na wakulima wataondokana na adha ya kutafuta soko nchini Kenya.
 
Mnyika
Ukiona hivyo utekelezaji wake bado haujaanza, hivyo wanaendelea kusisitiza. Kwi kwi kwi.
 
Watekelezaji ndiyo wanao wapa mimba wanafunzi na wanafunzi hawana kitu wana njaa na shule haipandi hawajala nyumbani na hawajui kama watakula so nao wao wanajilengesha yanatokea haya .Lakini zaidi ya yote issue ni kwamba hawa jamaa hutoa matamko wakiwa majukwaani so no one take them serious maana ndiyo zao za kuzima moto .
 
Na kwa nini atoe agizo in the firsr place kama sheria zipo? Nchi haiwezi kuendeshwa kwa maagizo ya wanasiasa, inapaswa kuendeshwa kwa sheria; kama sheria hazipo kazi ya mwanasiasa ni kuanzisha mchakato wa kutunga hiyo sheria.
 
Shein aagiza wanaowatia mimba wanafunzi wakamatwe
Makubo Haruni, Musoma
Daily News; Sunday,March 02, 2008 @00:04

MAKAMU wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein amewaagiza viongozi wa serikali mkoani Mara kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wanaume ambao kwa makusudi wanawapachika mimba au kuwaoa watoto wa kike na kuwakatisha masomo yao.

Vipi kuhusu walimu wa kike wanaokandamizwa mimba na wanafunzi wa kiume? kwi kwi kwi
 
Kikwete alilitoa alipoingia tu madarakani. Lowassa akalitoa mara kwa mara. Mama Sitta naye alilitoa mara kadhaa. Shein naye amelitoa tena. Lini litatekelezwa kwa ukamilifu wake? Kama vyombo vya dola vinashindwa kukamata hata wanaotia mimba wanafunzi ambao wanajulikana na wanaendelea kutamba mitaani vitaweza kweli kuwakamata mafisadi ambao wengine wameshakimbia nchini ama kuwauzia ufisadi wao watu wengine?

Shein aagiza wanaowatia mimba wanafunzi wakamatwe
Makubo Haruni, Musoma
Daily News; Sunday,March 02, 2008 @00:04

Habari nyingine
Watoto 11, 000 wa mazingira magumu wasaidiwa
Shein aagiza wanaowatia mimba wanafunzi wakamatwe
Majambazi Geita walazimisha mwanakijiji awaonyeshe matajiri
Askofu wa Cantebury ampa kazi nzito Mtetemela
Wachimbaji wadogo Mara kutengewa maeneo
Kata 20 zafikiwa na mradi wa Ukimwi
Mapadri watakiwa kuwa kioo cha jamii
Uzembe wa wakili waiangamiza TanRoads
Naibu Waziri asikitishwa na mafisadi MSD
Mwekezaji Mponde aomba msaada kwa Waziri Msolla

MAKAMU wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein amewaagiza viongozi wa serikali mkoani Mara kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wanaume ambao kwa makusudi wanawapachika mimba au kuwaoa watoto wa kike na kuwakatisha masomo yao.

Alilitoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara mjini Musoma uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Issa Machibya, kusoma taarifa kuwa wanafunzi wa kike 207 mkoani hapa kwa mwaka jana hawakuhitimu elimu ya msingi na sekondari kwa kutiwa mimba.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa kati ya wasichana hao 73 ni wa shule za msingi huku 134 ni waliokuwa wakisoma sekondari na kwamba waliowapa mimba wamefikishwa mahakamani.

Kutokana na hali hiyo Makamu wa Rais aliagiza kushughulikiwa wanaowapa mimba, kuwaoa na kuwabaka akisema kuwa wanawaua katika elimu wasichana hao na kuwafanya kuwa masikini kitendo ambacho alisema hakitafumbiwa macho .

Alisema kuwa wazazi wamekuwa wakijinyima na kutoa mali zao kwa ajili ya kuwasomesha lakini wanakatishwa tamaa kwa wasiopenda maendeleo, wenye tamaa ya mwili kuwakatishia maisha kwa kuwapa mimba katika umri mdogo.

Dk. Shein, alielezea kuwa serikali katika bajeti yake ya 2007/2008 ilitenga zaidi ya Sh trilioni 1.18 kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu nchini na kwamba Mkoa wa Mara kwa mwaka huu umepata Sh milioni 976 kwa ajili ya uchangiaji wa ujenzi wa sekondari, huku wananchi nao wakichangia kutoa elimu bila ubaguzi.

Aliitaka pia jamii kukataa kwa nguvu zote uharibifu wa watoto wa kike kwa vile nao wanahitaji haki ya kupata elimu ili waingie kwenye ushindani wa kidunia wa sayansi na teknolojia.

Hata hivyo alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Nne inaendelea kuboresha maisha ya Watanzania kwa kuweka kipaumbele katika kuendeleza kilimo chenye tija kwa kutoa ruzuku ya mbole, utoaji wa mbegu bora ambako kwa sekta ya kilimo pekee serikali imetenga Sh bilioni 379 sawa na asilimia sita ya pato la Taifa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Wizara ya Kilimo na Chakula imetoa tani 508 za mbolea na tani 75 za mbegu ya ruzuku kwa ajili ya wakulima na kwamba kwa upande wa zao la pamba wakulima wameuza tani 1,312,300 na kujipatia Sh bilioni 6.5.

Machibya alisema kuwa Mkoa wa Mara hususan Wilaya ya Tarime, uwanda wa juu umeanza kilimo cha chai ambako wakala wa wakulima wa chai Tanzania wametoa miche 8,000 ya zao hilo na itakapopandwa kiwanda kitajengwa na wakulima wataondokana na adha ya kutafuta soko nchini Kenya.

Sijui kama hawa wanaotoa maagizo huwa wanayafuatilia kama yametekelezwa. Lakini ndivyo wanasiasa wetu walivyo.
 
Back
Top Bottom