Hilary Clinton na shinikizo kwa viongozi wa Africa juu a Gadaffi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hilary Clinton na shinikizo kwa viongozi wa Africa juu a Gadaffi

Discussion in 'International Forum' started by Kisoda2, Jun 14, 2011.

 1. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Bibi Clinton amewataka viongozi wa Africa kumshinikiza Gadaff kuacha mapigano na kum taka aondoke madarakani nchini Libya.
  Wakati huo huo akiwataka kuwatambua/Kilitambua baraza la waasi kama wawakilishi halali wa wananchi wa Libya.
  Ameyatamka haya akiwa huko Addis ababa makao makuu ya AU.

  Je, hii kitu ndo ilimleta mpaka kwetu na kujidai kutuletea neema.

  source:Dutch welle Asubuhi ya leo.
   
 2. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Kwa msisitizo zaidi amewataka viongozi hao kuwafungahs virago wawakilishi(Mabalozi) wote wa Gadafi popote walipo Africa.

  Hii mpaka lini Africa tunamuliwa na hawa wanaojiita wapenda amani?
   
 3. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  50 years of inDEPENDENCE!!!!!!!
   
 4. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Huyu bibi hana kheri yoyote kwa Afrika zaidi ya ushawishi muovu.
  Kwetu nchi ya kiuingwana alikaribishwa na tetemeko la ardhi.Kile kituko cha kuuliwa Fazul ni zawadi kutoka kwa wapenzi wa Marekani na watu wanaojipendekeza ili kujitafutia fedha za misaada.
  Al shabab wajitayarishe kumpokea mjini Mogadishu kwa ninavyowaelewa wamarekani na siasa zao huyu mama atatua pale kutoa pongezi na kuahidi pesa kutoka hazina zao za dhulma za Libya na Iraq na akishaondoka itatangazwa ushujaa wake ili kukipatia chama chake sifa.
  Hapa kwetu hutosikia akina Chadema na Lisu wao wala wabunge wa CCM wakihoji Symbion ya Hillary Clinton tofauti na ile Dowans ya Al Adawy.
   
 5. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  kwani richmond/dowans ilitokea wapi mkuu? ni swali tu. Al adawy alikuwa front tu maskini ya Mungu mzee yule. Kitu kimoja ujue ni kuwa wenye Downs/richmond ndiyo hao hao wenye symbion and we are just victims!
   
 6. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Nimefurahi Utingo kwa mara ya mwanzo umezungumza maneno ya hekima.
  Sasa tuseme ni kipi kinachomfanya Lisu amnyamazie Clinton na Symbion.Au tuseme kwenye Dowans alikerwa na ile kanzu tu ya shareholder?.
  Unakumbuka alitaka mitambo ya Dowans itaifishwe!.
   
 7. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,609
  Likes Received: 6,774
  Trophy Points: 280
  Mwanamama anahimiza demokrasia, lakini hatuambii hao rebel wa Benghazi wamechaguliwa na raia wepi lini na wapi, na kwa nini wao wawe ndiyo serikali ya libya?
   
 8. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Sipendi kumungumzia lisu au yeyote...jiulize mwenyewe who is running the world now? kwa mfano miezi kadhaa iliyopita Gaddafi alikuwa rafiki mkubwa wa italy, france na hata EU, leo is the big enemy na wanamtafuta wamwue. What has gone wrong? Who is at the top of all these things happening?

  Kama gaddafi hata yeyote anaweza kudhibitiwa sembuse Lisu? You need to know that kuna systems katika ulimwengu huu inayotaka sana ku-dominate kila kitu kwa gharama yo yote ile. ndiyo maana nimekwambia aliyeleta richmond (kutoka marekani), ndiye aliyeleta Dowans (kutoka Costa rica?) now comes Symbion (USA) !!!??? jiulize kwa makini hapo
   
 9. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ndio maana nikakwambia utingo leo umekuwa na hekima sana.
  Naamini wewe kama mimi ulipokuwa mdogo hukupelekwa klinik kupata chanjo.
   
 10. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hahahaaaa, kwa kweli umenifurahisha na umenikumbusha mbali sana..ulimwengu murua sana ule wa zamani. Nilipiga mswaki kwa mizizi, tumbo likiuma nilitafuna mizizi na hata malaria nilichemshiwa mizizi.
   
 11. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  hilo ndo balaa lake,
  maana kanaongea tena bila aibu rebels ndo wawakilishi halali!!
  Basi na yemen watwambie waandamanaji ndo wawakilishi au kwa vile hawashiki mitutu, hawawezi wakilisha raia wa yemen?
   
 12. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  leo hii unatwangwa dawa mseto!!!
   
 13. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  na huambiwi mseto huo umechanganyikana na nini...matokeo yake wengine wanaishia kubabuka ngozi!
   
Loading...