Mkuu naomba hayo mambo 10 uliyosema ndio Utapeli wa QNET nipe kwa namba tafadhali mana hapa nilipo nimeshashawishiwa niuze hata kiduka changu ilimrandi nipate ile milioni 5,300,000/= ninunu ile bidhaa., yaani hivi naandika naamini majibu yako ndio yatakayonipa jibu rasmi niuze duka langu nikanunue au niachane na QNET kabisa.
soon utatembea una ongea peke yako
 
Kuna hili kampuni ambayo naona kama inacheza UPATU. Kuna jamaa yangu aliingia kwa 2,000,000. Sasa ni zaidi ya mwaka hajapata chochote.

Sasa wana wadanganya vijana kuwa kuna ajira bila ufafanuzi wakifika mjini wanawaambia watambue wazazi wao watume fedha ili walipie bidhaa walizochagua hili waweze kuongeza credit na kupata hela na wamepanga nyumba Msakuzi kwa Majeshi Makali Mawe.

Kila anayefika anatakiw atoe sh 50,000. Wanalala kama Selo chakula wanafanya donation. Kwa ufupi ni hivyo kama kuna mwenye uelewa juu ya hilo anipe ufafanuzi maana naona ni utapeli mtupu.
 
Kuna hili kampuni ambayo naona kama inacheza UPATU. Kuna jamaa yangu aliingia kwa 2,000,000. Sasa ni zaidi ya mwaka hajapata chochote
Sasa wana wadanganya vijana kuwa kuna ajira bila ufafanuzi wakifika mjini wanawaambia watambue wazazi wao watume fedha ili walipie bidhaa walizochagua hili waweze kuongeza credit na kupata hela na wamepanga nyumba Msakuzi kwa Majeshi Makali Mawe. Kila anayefika anatakiw atoe sh 50,000. Wanalala kama Selo chakula wanafanya donation. Kwa ufupi ni hivyo kama kuna mwenye uelewa juu ya hilo anipe ufafanuzi maana naona ni utapeli mtupu.
Thread za qnet zimejaa humu mbona nyingi search usome
 
Nafikiri kuwakusanya watu kwa mtindo ulioelezea ni kosa kisheria.

Mfikishie mtendaji kata hilo swala.

Kuhusu uhalali. Qnet wanafanya network marketing kwangu mimi that is a fancy way of saying pyramid scheme.

So ni hivyo
 
Kuna hili kampuni ambayo naona kama inacheza UPATU. Kuna jamaa yangu aliingia kwa 2,000,000. Sasa ni zaidi ya mwaka hajapata chochote
Sasa wana wadanganya vijana kuwa kuna ajira bila ufafanuzi wakifika mjini wanawaambia watambue wazazi wao watume fedha ili walipie bidhaa walizochagua hili waweze kuongeza credit na kupata hela na wamepanga nyumba Msakuzi kwa Majeshi Makali Mawe. Kila anayefika anatakiw atoe sh 50,000. Wanalala kama Selo chakula wanafanya donation. Kwa ufupi ni hivyo kama kuna mwenye uelewa juu ya hilo anipe ufafanuzi maana naona ni utapeli mtupu.
Sasa si waondoke warudi makwao?
 
Watu wa ukumbi huu habarini

Nimeona nije kwa hii inayoitwa QNET kampuni ambayo wanasema kwamba inatoa fursa ya kibiashara kwa watu ulimwenguni.

Binafsi nimehudhuria mikutano miwili ya QNET kupata maelezo mbali mbali kuhusiana na hii biashara lakini nilichokuja kugundua hawa QNET huwatumia hawa mawakala wao kusema uongo kwa watu wasiojua mambo ya bisahara za Online inakuwane, lakini pia kwenye mafunzo yao hulinganisha kama tunavyonunua bidhaa kutoka Ebay, Alibaba nk.

Sasa hapa nimekuja kuonyesha huu udhaifu wa QNET na hiyo mitandao mengine wanayoipigia kelele.

1. Unaponunua bidhaa Ebay kwa mfano hapa nina uzoefu mkubwa kwamba inabidi niongee na seller/muuzaji anayeuza ile bidhaa tena naongea naye binafsi lakini kwa QNET ni tofauti inabidi uongee na kampuni ya QNET kupitia wakala/ ama mteja kama wewe utakayekuwa kupitia duka lake la Online.

2. Ebay tunakuwa na uhuru wa malipo tunalipia kupitia online mimi mwenyewe binafsi baada ya kufanya maongezi na seller nikitaka juu ya ile bidhaa, Lakini QNET inabidi fedha zako milioni 5 labda na laki 2 au 3 (inategemea na rate dola ) umpe mteja kama wewe mkononi akunulie wewe kwenye Kampuni ya QNET kupitia account yake ya online. (Hapa ikumbukwe kwamba unapolipa online siku zote bei za dola huwa zina varies kwaiyo lazima kutakuwa na chenji sina hakika kama wanawarejeshea wale watu walio lipia zile bidhaa chenji iliyobaki.

3. Kwenye Ebay huwa kuna uhuru wa kuchagua bidhaa mbali mbali kwa maelfu na bei tofauti kabisa yaani kuna bidhaa unanunua ata $1 au chini ya $ 1 na kuendelea lakini QNET wao ili ujiunge na ule mradi wao wa ile chain ya mtu 1 kuliani kwako na 1 kushotoni kwako nilazima ununue ile bidhaa kwa milioni 5 labda na laki 2 au 3 huwezi pata chini ya hapo labda watoe ofa huwa inatokea mara chache sana, na bidhaa zenyewe utashangaa wamechagua bidhaa maalum kama water filter, saa ya kuvaa mkononi, mkufu wa dhahabu, bio disk labda na dawa za virutubisho (bidhaa zao ni chache) nje ya hapo huwezi pata bidhaa nyengine. Lakini cha kushangaza zaidi mimi katika maisha yangu sijawahi kwenda dukani nikakuta bidhaa 5 tofauti mwenye duka akanambia zote hizo bei ni moja tu kila ntakachogusa, lazima kutakuwa na tofauti ya bei, lakini swali jengine kwanini hizi bidhaa ni kuanzia milioni 5? ukienda kwenye Ebay ambayo wanailinganisha utakuta haya mambo ni tofauti sana zaidi ya sana.

4. Ebay unaweza nunua bidhaa lakini kama sivyo uliyotaka labda ina kasoro ya kile ulicho ki-brouwse kwenye mtandao unaweza ku complain kwa seller na akakurejeshea fedha zako (refund) na labda bidhaa yake ukamrejeshea itategemea na makubaliano yenu mtakavyoelewana lakini QNET ukishanunua bidhaa hata ije na kasoro gani huwezi ku- complain na hela yako ndio imekwenda wala hakuna guarantee wala chochote ikija bidhaa kama umeipenda ni hiyo kama hujaipenda ni hiyo hiyo (no refund). Binafsi Ebay wameshanirejeshea hela zangu kwa sababu bidhaa niliyonunua waliniletea rangi tofauti na rangi niliyoichagua na kuipenda wakati wa ku-browse mtandaoni.

6. Ebay kuna uhuru ata wa kumpigia simu yule seller mkaongea vya kutosha na ku-bagen yaani akupunguzie bei na sellers wanafanya hivyo ni jambo la kawaida lakini QNET bei unayoikuta kwenye hilo duka la mtu haina bagening, bei zao ni fixed huwezi punguziwa bei ata iwe vipi.

7. Ebay wanakuweka wazi kabisa kwa mfano kipindi hichi cha Corona kwamba bidhaa yako inaweza kuchelewa kufika labida inaweza kuchukua ata miezi 4 kutokana na safari za ndege kupigwa marufuku wakati wa kusafirisha bidhaa yako kwa baadhi ya nchi, sasa kama unataka kuendelea kununua unanunua hutaki unaacha lakini QNET mpunga ukishaupeleka kwa yule wakala yeye kashatia $200 zake mfukoni kwa kila wateja wateja 2 haya ya bidhaa kuchelewa hayajadiliwi tena wala chochote ndio imetoka tena usubiri tu.

8. Ebay na Makampuni mengine kama Alibabab na AliEpress unaweza kujenga urafiki na hawa Sellers japo hamujuani kwa mambo mengine mbali mbali lakini QNET huyo Victor VJ mkuu wa kampuni yao kule China ata hana habari na wewe kabisa wala hana time wewe hoja zako utaishia kwa mteja mwenzako aliyekuunganisha na kukusajili.

9. Ebay na Makupuni mengine unaweza nunua bidhaa kwa ajili ya biashara yaani wanakuletea bidhaa kama ni viatu au spea zikifika hapo ukaweza fanya biashara na kutengeneza faida halafu ukaagiza tena na tena lakini QNET unanunua ile bidhaa kwa matumizi ya nyumbani tu halafu unapatwa na kazi ya kutafuta watu wengine uunganishe.

10. Bei ya bidhaa ya QNET sio bei halisi ya ile bidhaa unayonunua utakuta kama hii water filter inauzwa mpaka Tshs 600,000/= tuseme laki 800,000/= lakini QNET huwezi ipata chini ya milioni 5., yaani hapa mimi nimegundua kwamba hawa QNET zile milioni 5 nyuma ya pazia ni kwamba ni bei ya kujiunga tu na ile kampuni lakini hudanganya na kusema ni bei ya bidhaa mana bidhaa ile ile ukiagiza Ebay basi unaipata kwa bei yenye wastani wa laki 6 au 8 Tshs.

SASA TUJE KWENYE MAMBO MENGINE TOFAUTI NA MTANDAONI:

Ndugu zangu QNET hawa mawakala wao hutumia neno fursa, yaani akija mtu kutaka ujiunge na QNET atakwambia kuna fursa nzuri ya kutengeneza maisha yako kwa muda mfupi sana lakini nataka nikuzindue kitu unapoingia QNET inabidi utoe milioni 5 kununua ile bidhaa na kujiunga lakini ili fedha zako zirudi ni kwamba mpaka uweze kuwashawishi watu wengi kidogo ndio fedha zako ziwe zimerudi kwasababu mpaka unawashawishi watu 16 tu kujiunga QNET tayari kwenye hawo watu 16 QNET kama kampuni washatengeneza milioni 80, wameshatengeneza milioni 80 lakini wewe uliyetoa milioni 5 bado utakuwa umerejesha hela zako kama milioni 3 tu hivi bado una kazi ya kushawishi wengine ili urejeshe pesa zako. Sasa emu niambie itakuchukua muda gani kuwapata watu 2 kushotoni na kuliani kwako lakini itachukua muda gani hao watu 2 nao kupata kila mtu watu 2 kuliani na kushotoni mpaka kufikia hao 16? Utagundua ugumu wa hii wanayoiita fursa ya Kibiashara.

Mimi nilikuwa aproached ni Dr. mmoja anasema yeye alikuwa daktari Muhimbili sasa ameacha kazi kwa sababu QNET imemletea tija mpaka mke wake na watoto wake wako huko QNET, Lakini kuna jirani yangu mmoja hapa amejiunga sasa ana miezi 4 hela yake tu haijarudi alimfata aliyemuunganisha jibu alilompa alimwambia mwanzo mgumu jitahidi, sasa kama mtu aliuza bishara yake ya duka akapata hela ya kujiunga au aliuza ngombe wake au aliacha ajira yake akafuatilia QNET au alitoa msingi wake wa bishara au alienda kukopa mahali hela za kujiunga ndani ya miezi minne hujajeresha hela huyu mtu atakuwa na hali gani mpaka tuiite QNET ni fursa ya kibisahra?

Lakini nimejaribu kufanya research watu wengi waliojiunga na QNET huwa hawasemi ukweli juu ya udhaifu niliouonyesha mara nyingi lugha yao imekuwa ni moja nikawa napata tabu sana kwanini hawa watu wanakuwa hivi lakini nikaja nikagundua kumbe hawa wateja wa QNET ambao tayari washajiunga kumbe huwa wanaitwa na kuhudhuria madarasa mbali mbali ya kufundishwa namna mbali mbali ya aidha kujibu hoja za watu zitakazoibuka juu ya QNET lakini hupewa elimu wao wenyewe bila ya kujijua wakajikuta QNET wanaona ni mpango mzuri sana Lakini cha kushangaza wapo watu ambao nawaona wamejiunga kitambo tena lakini physically sioni maisha yao kubadilika nawaona kawaida tu, anaye kula kwao anakula kwao, anaetembea kwa miguu sijamuona na gari nk.

Binafsi naona QNET kama hakuna budi mtu anataka kujiunga basi awe anazo hizo milioni 5 ambazo haziko kwenye bajeti yake ya maisha na ajaribu kuzisahau au achukulie kama zimepotea tu akiweza fanya hivi hapana budi basi anaweza kujisajili QNET.


Mimi kiimani ni muislamu lakini weakness nilizoziona hapo juu kwa mujibu wa sheria zetu za kiislamu nimejiridhisha kwamba biashara hii haifai, ndani yake kuna shubha na hila nyingi sana hasa hasa muanzilishi wa biashara ni mtu kutoka China na hajaweka wazi kwenye hii biashara wao kama kampuni huwa wanafanya nini na nini yaani sijaona financial details zao, pengine wanachezesha kamari, pengine freemason nk.

Naomba kutanguliza
Asante kwa uzi. Uzi bora kabisa mkuu. Binafsi nilishawishiwa na rafiki zangu wawili kwa nyakati tofauti tofauti sema niliwachomolea.

Aisee, jamaa walinitait ofisin kwao siyo mchezo.
 
Bora iendelee kuwepo na wengine waendelee kuwatapeli watu. Maana jamii yetu inawajinga wengi, kila wakielimishwa wao hawasikii.

Kuna wengine wanaitwa Wozur, kampuni inajidai imesajiliwa UK lakini kumbe hamna kitu. Wacha watu wapigwe. Ujinga wa huyu ni utajiri wa yule.
umesikika vyema mkuu
 
Back
Top Bottom