Hiki ni nini kwenye hii picha ya gari?, nimejaribu kuulizia kwa wadau wengine wananiambia ni waandishi wa habari

Na wanajuaje kuwa hii radio imesajiliwa au bado maana kwa tz nzima sio mchezo? Asante sana mkuu, kwa hiyo yapo kila sehemu au?
Umefanya vizuri kuuliza. Hilo dungu hapo juu ni Antenna kwa ajili ya kufuatilia masafa( Spectrum monitoring)...kazi yake ni kukagua muingiliano wa masafa ya simu,mawimbi ya utangazaji,radio call nakadhalika….hilo pia hukagua mawimbi haramu ambayo watu wanajipatia...elewa kwamba masafa ili uyatumie lazima TCRA wakupatie kwa hiyo hilo dungu linakagua kubaini wezi wa masafa na hata wezi wa simu wanaweza kupatikana kwa hilohilo dude...Linaitwa mobile Spectrum monitoring antenna. Je una swali la ziada?
 
Na wanajuaje kuwa hii radio imesajiliwa au bado maana kwa tz nzima sio mchezo? Asante sana mkuu, kwa hiyo yapo kila sehemu au?
Kila mtumiaji wa masafa kwa mfano waongoza ndege,radio call za polisi au taasisi mbalimbali,Radio za FM,MUX kama vile Star Times,Telecoms kv VODA TIGO nk wote hawa hupatiwa leseni na kugawiwa hayo masafa na TCRA...Masafa ni kama kitalu cha mboga ambapo watu hugawana kwa hiyo mwenye wajibu wa kugawa ni TCRA...hivyo yeye kama TCRA anafahamu kila safa na ana uwezo wa kungámua nani ni mwizi wa masafa kwa kutumia hilo dude...lenyewe likipita pahala lina scan na kubaini masafa yaliyopo...ndio maana unasikia kuna watu wamepandishwa kizimbani kwa kuingiza nchini vifaa vya masafa visivyotakiwa wananaswa na TCRA...hivyo hilo dude linaleta ndani mrejesho. Pia linaweza kubaini ubora wa huduma za mawasiliano.

Wao watajua tu kwamba hii haijasajiliwa kwa sababu wao ndio watoa leseni kwa mujibu wa sheria za EPOCA. zisome hapa https://www.researchictafrica.net/c...c_and_Postal_Communications_Act_no_3_2010.pdf
 
Hapana aisee hao sio TMA
Akitokea mwingine akasema ni gari la kurushia matangazo, utatumia kigezo gani ku-demerit maoni yake na ku-merit ya kwako? Tumejibu hiyo picha objectively, bila kuwa subjected na prior assumptions ulizokuwa nazo, au unless wewe unalijua hilo gari personally.
 
Hiyo siyo kwa ajili ya kutafuata habari, hapana...

Hilo gari ni maalum kwa ajili ya kuzuia na kukata mawasiliano kwa watumiaje...

Mara nyingi linaambatana kwenye msafara wa Rais au viongozi wakubwa...


Cc: mahondaw
 
Nalijua personally...nilipata fursa ya kuuliza maswali kwenye maonyesho ya nanenane miaka saba iliyopita...binafsi nachukia mtu anaependa kutoa jibu kwa swali ambalo hana majibu ya uhakika...JF tuna tatizo hilo sana. Ni vema jambo kama huna taarifa nalo ukakaa kimya...binafsi nimetoa jibu na Pasco amekazia kwa kuweka link kabisa...sasa huyo anaempotosha mleta swali hamtendei haki.
Akitokea mwingine akasema ni gari la kurushia matangazo, utatumia kigezo gani ku-demerit maoni yake na ku-merit ya kwako? Tumejibu hiyo picha objectively, bila kuwa subjected na prior assumptions ulizokuwa nazo, au unless wewe unalijua hilo gari personally.
 
Back
Top Bottom