Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 27,542
- 34,871
USA ilikuwa koloni kubwa la UK, kwanini sio mwanachama wa jumuiya ya madola ?View attachment 2224792
Ilibidi miguu ya kiti itengenezwe mifupi kwasababu Malkia Victoria alikua mwanamke mfupi kwa umbo, wasingeweza kuweka miguu ya kiti mirefu na kumuacha Malkia akining’inia.
Baada ya Victoria alitawala mtoto wake Edward, nae alipokewa na mtoto wake George V aliyerithiwa na mtoto wake Edward ambae ilibidi aachie kiti baada ya kumuoa mwanamke wa Kimarekani tena aliyetalakiwa. Kitendo hiki kilisababisha Albert ambae ni baba yake Malkia Elizabeth kuapishwa kama Mfalme George wa sita.
Sasa hivi Malkia Elizabeth katika umri wa miaka 96 jua limezama na nguvu za kutawala zimemwishia. Mtoto wake Charles anajiandaa kuapishwa. Nimeona kiti cha enzi kimetolewa inawezekana kinapigwa msasa kwa maandalizi ya sherehe ya kusimikwa rasmi kwa Charles kama Mfalme.
Charles atataka miguu ya kiti iongezwe? Wakati kiti kinatengenezwa Uingereza ilikua na Madola 3/4 ya dunia, hivyo kupata dhahabu ya kutengeneza kiti cha Enzi haikua shida. Sasa hivi mambo yamebadilika. Hata dhahabu ikipatikana wana harakati watapaza sauti na kuhoji ulazima wa kutumia dhahabu kutengeneza miguu ya kiti cha Mfalme.