Hiki ni kilio changu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hiki ni kilio changu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by TANMO, Aug 19, 2011.

 1. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Wapendwa, Mabibi na Mabwana: Kwanza kabisa poleni kwa majukumu ya siku nzima ya leo. Ningependa kuwasilisha kilio changu kuwakilisha watu wote wanaotumia Baiskeli kwa shughuli zao za kila siku, Jamani naomba na sisi Tuthaminiwe. Watanzania wenzenu tunautumia Usafiri huu kwa ajili ya Biashara na pia kama usafiri kama ilivyo kwa wenzetu wanaotumia Magari, pikipiki au hata Bajaji. Mara nyingi tuwapo barabarani huwa tunapuuzwa na tunapokonywa haki zetu za matumizi ya Barabara, ingawa pia ninakiri kuwa kuna wenzetu ambao kwa namna moja au nyingine wanajikuta wanajiingiza kwenye matatizo wenyewe.

  WAENDESHA MAGARI: Chonde chonde ndugu zetu hasa kwenye miji mikubwa, pale mnapojikuta kwenye foleni na magari yanatakiwa kusimama tunaomba mtii utaratibu badala ya kutanua na kuingia kwenye barabara ya waendesha baiskeli pamoja na watembea kwa miguu. Huwa mnatukosesha sana amani pale mnapolazimisha kupita kwenye njia zetu na kutulazimisha kuwapisha kwa kutupigia honi kila mara. Pia pale mnapojikuta kwenye wakati mgumu aidha mbele anapojitokeza hata kuku msikimbilie kuwakwepa na matokeo yake kutugonga sisi wapanda baiskeli tunaokuwa pembezoni mwa barabara.

  WAENDESHA PIKIPIKI NA BAJAJI: Tunawapenda sana ndugu zetu na tunawaheshimu sana, pia poleni sana kwa maswaibu ya mara kwa mara mnayokumbana nayo na waendesha magari. Basi ninawaomba msiwe mnaendesha kwa fujo na mara mnapokuwa kwenye zile njia za wapanda baiskeli na waenda kwa miguu msiwe mnatupigia honi ambazo wakati mwingine hutusababishia ajali bila ya sababu za msingi. Nawaomba sana mtuthamini ili tuweze kutumia barabara zetu kwa usawa na usalama.

  WATEMBEA KWA MIGUU:
  Ninyi ni ndugu zetu na tumepewa haki ya kutumia barabara kwa usawa kabisa. Tunawapenda na tunathamini sana utu wenu, naomba nanyi pia msiwe mnatupuuza na muwe mnatupisha pale inapobidi kama ambavyo huwa mnawapisha wenye magari hata kama ninyi ndiyo mna haki. Leo nimefikwa na kisa (ambacho kimenifanya nilete hiki kilio), kuna mwanamama alikuwa na mtoto mgongoni alipisha gari likapita na kwa bahati mbaya nilikuwa nyuma ya hilo gari, badala ya kunipisha akalazimisha kurudi barabarani. Mimi kwa mapenzi mema nikalazimika kuingia vichakani ili tu mama na mwana waendelee kuwa salama, nimepata hasara kubwa ya Trey tano kati ya kumi na tano za mayai niliyokuwa nawahisha kwa mteja pamoja na kobazi langu kukatika na zaidi nikapoteza ukucha kwenye eneo la tukio:(

  Hivyo basi wapendwa, naomba chonde chonde msikie kilio chetu kwani bila kuendesha hizo Baiskeli wengine hatuwezi kupitisha siku na mbaya zaidi wanetu watashindwa kwenda chooni na tutashindwa kuwapeleka shule kuwapatia elimu, kwani tunaambiwa elimu ni msingi wa maisha. Rafiki yangu ameweza kupiga hatua zaidi baada ya binti yake kufaulu kwenda chuo kikuu na kila mwezi anampatia Shilingi Thelathini elfu wanazopewa na Serikali ili wasome. Na mimi nina imani kuwa nikimpeleka mwanangu shule ipo siku atanisaidia kwa pesa atakazokuwa anapewa, na mkitusaidia kwa kututhamini tunapokuwa barabarani tutaweza kufikia malengo yetu vyema.

  Asanteni kwa kusikiliza kilio changu.
  Wenu,
  TANMO (Tanzania Ni Moja)
   
Loading...