Hiki ndio kitakachofuata baada ya marudio ya uchaguzi wa Zanzibar

FakeID

Member
Feb 29, 2016
89
96
Kile kilichoitwa uchaguzi wa marudio wa Zanzibar umeshakamilika na kama ambavyo ilitarajiwa na mgombea wa CCM ameibuka na ushindi ambao wao wenyewe wanauita wa kishindo.
Lakini dunia nzima inafahamu ya kwamba uchaguzi huo ulifanyika katika mazingira ya vitisho, ubakaji wa demokrasia na kutokuwepo kwa maridhiano, hali iliyosababisha vyombo vya ulinzi na usalama kuhamia kisiwani humo kwa ajili ya kuhakikisha uchaguzi unafanyika na Dr Shein anashinda kwa gharama yoyote ile hata ikibidi kwa damu kumwagika.

CCM na watu wa system wameyafanya haya makusudi sababu tayari wanajua jinsi wananchi walivyowepesi kusahau, na hii yote ni sababu walisahau machungu ya kuporwa ushindi wa Lowasa kwa hiyo wanaamini kwamba hata Wazanzibar pia watasahau katika hiki kilichotokea.

Kitakachofanyika kuanzia sasa itakuwa ni maigizo yanayopangwa na kila chombo cha habari kama ambavyo amekuwa akipambwa Magufuli kwa kila anachofanya, yaani tujiandae kumuona Shein katika mtindo wa tofauti wa kufanya mambo yanayolenga kutafuta umaarufu ili mioyo ya Wazanzibar iliyopondekapondeka, iliyosononeshwa na ubabe wa wanyang'anyi hawa isahau yote yaliyotokea.

Chonde chonde wazanzibar, kusahau dhuluma hii ni dhambi kubwa sana hata ibada zetu itakuwa ni bure mbele ya Mungu, tutapata laana ya vizazi na vizazi. Huu ni muda muafaka wa kumuonyesha Shein ya kwamba hatukumchagua. Tafadhali UKAWA katika kipindi hiki tunahitaji kuwa wamoja sana kuliko kipindi chote cha uhai wa umoja wetu, tuungane kuionyesha dunia ya kwamba Wazanzibar wanamhitaji Maalim Seif mpaka wakamchagua Octoba 25 .2015.

Wasalaam.
 
Zanzibar yetu haiko kama unavyofikiri,kiongozi yeyote akitenda jambo kwa mafaa ya wananchi tutampongeza na kumuunga mkono. Pia ataripotiwa kwa anachofanya na si kupambwa kama unavyodhani. Nyumbu wewe.
 
Zanzibar yetu haiko kama unavyofikiri,kiongozi yeyote akitenda jambo kwa mafaa ya wananchi tutampongeza na kumuunga mkono. Pia ataripotiwa kwa anachofanya na si kupambwa kama unavyodhani. Nyumbu wewe.
Unasema zanzibar haipo hivyo eee
 
kuwa mkweli sijawahi kupewa au kuona ushahidi wa kuibiwa kura wa lowasa.Kelele za kuibiwa ushindi ni kubwa kuliko ushahidi wa kuibiwa.

Kuhusu zanzibar; Ipo siku haki itapatikana, Nilitamani kuona Muungano huku Zanzibar iko chini ya Maalim Seif. Hii ingesaidia mamilioni ya watanganyika wanaoamini mpinzani hawezi kutawala hili taifa. Hii laana imesababisa wametuwekea wabunge wengi wa CCM na madhara yake mmeyaona ktk UFISADI ndani ya KAMATI ZAO PENDWA za bunge.
 
Back
Top Bottom