Hiki ndio alichosema Diamond baada ya Wema Sepetu kuzungumza kwenye XXL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hiki ndio alichosema Diamond baada ya Wema Sepetu kuzungumza kwenye XXL

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Nyundo Kavu, Apr 4, 2012.

 1. Nyundo Kavu

  Nyundo Kavu Senior Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 187
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Baada ya Miss Tanzania 2006 ambae pia ni bongo movie star Wema Sepetu kuzungumza kwenye XXL ya CLOUDS FM jana kwamba alichokifanya Diamond kukataa kuchukua pesa yake ni uswahili, Diamond nae ameamua kuzungumza na millardayo.com

  Kabla ya kukupa alichosema Diamond, Wema alikanusha pia kuhusu stori kwamba alikwenda nyumbani anapoishi Diamond ili waondoke wote kwenda kwenye show Mlimani City kwa kuthibitisha kwamba hapajui hata Diamond anapoishi.

  Baada ya kukasirishwa na alichokisema Wema, Diamond aliomba kuzungumza kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM na kukiri kwamba "Millard kiukweli mimi sipendi ugomvi, na haya nisinge yasema kama yeye asingekuja kuongea uongo, yani hata sababu kubwa ya mimi na yeye kutofautiana ilikua ni kitu kidogo tu anakipeleka kwenye media na ikafika time anasema hanitaki ila mimi ndio namng'anga'nia wakati ukweli ni kwamba alikua analetwa nyumbani na rafiki zake na ndugu zake akilia anaomba isuluishwe turudiane, mpaka anampigia mama yangu mzazi, rafiki zangu na ndugu kama Shetta na Romy Jones, pia anawaambia marafiki zake waandae sehemu ya Dinner ili atokee kama Suprise"

  Diamond amesema "kabla ya show yangu ya juzi alikuja nyumbani mimi niko ndani navaa nasikia sauti yake barazani, namuuliza ndugu yangu Rommy ananiambia ni Wema, nauliza kafata nini nyumbani? mimi nina mpenzi wangu na yeye anamfahamu na hizi drama za Wema zinafanya mpenzi wangu akasirike kwa sababu anaona bado naendelea na Wema, sasa pale nyumbani nilitoka nje baada ya kukasirika ila wakanishika nisimguse, ndio wakamwambia aondoke…

  Yani baada ya kugundua kwamba mimi sitaki kuwa na yeye tena sasa anatumia kama ile hautaki kuwa na mimi, Nakuharibia sasa"

  "Wakati anakuja kunipa hela kwenye stage mi nilikua naogopa kwa sababu tayari alikuja nyumbani kabla yake ndio maana nilihisi anataka kufanya drama nyingine tena ndio maana nikamkwepa na kujifanya kama sijamuona lakini akaganda makusudi kama anataka kufanya kitu flani, mpaka mwisho baadae akamfata Q Chief anamlilia pia kawafata mama yangu na mama mdogo anawaambia mimi mtoto wenu nampenda sana ananitesa, alafu baada ya hapo anakuja kwenye Media na kuongea vitu vingine, na kunitengenezea mazingira ili mimi nionekane mbaya" – Diamond

  Katika sentensi nyingine Diamond amethibitisha kwamba kwenye hiyo show yake kulikua na wasichana wawili ambao waliwahi kuwa wapenzi wake, na walijitokeza pale kwenye stage na kumpa pesa na yeye alizipokea bila tatizo kwa sababu hana tatizo nao akiwemo Sarah ambae nlimwimbia "Nenda kamwambie" ila za Wema alizikataa makusudi kwa sababu alikua anataka kutengeneza drama manake ishu isingeishia pale.

  Platnums ameizungumzia ishu nyingine kwamba "hata nilipokua kwenye uhusiano na yeye nilishawahi kumuonya Wema mara nyingi, niliku sipendi kuwa na mtu anaeandikwa andikwa sana kwenye magazeti, kabla nilijua ni umaarufu lakini nikagundua kwamba alikua anazipeleka stori mwenyewe tena na hela ya kuwalipa waandishi anatoa, na kuna kipindi nililipa hela waandishi wasiandike hizo habari lakini Wema akatoa zaidi ya hiyo, alikua anapeleka stori mwenyewe, kama juzi alisikia naumwa niko hospitali akanipigia kunipa pole…. kesho yake nikaona stori kwenye gazeti wakati hakuna aliefahamu zaidi yake na stori imetoka vilevile, nikakasirika sana"

  "katika tukio lililoniudhi zaidi ni pale nilipogundua alipopeleka stori ya kuniharibia kwenye gazeti kwamba nina nuski na ishu nyingine kibao, baada nikakutana nae nikamuuliza kwanini unapeleka hizo habari kwenye gazeti? Akazuga kwa kumpigia simu mwandishi na kuanza kumtukana mbele yangu kwamba hizo habari ameandika tofauti, sio kama alivyomuhoji, lakini baadae wakati nimeondoka alimpigia simu na kucheka huku akimwambia tumemuweza leo, Wallah nimlale mama yangu mzazi hicho kitu ndio kiliniuma nikaona bora tuachane kwa sababu niligundua ananitumia mimi kufanya mambo yake, amesema yeye ndio alianza kuwa staa kabla yangu….. ni sawa ila mimi kuanza kwangu nimekuja na akili, yeye anataka kutumia wanaume mastaa apate umaarufu"

  "Kilichonifanya nijue kwamba amenizunguka kwenye ile habari ni wakati nilipokutana na huyo mwandishi ambae alinithibitishia kwamba Wema mwenyewe ndio aliipeleka ile habari na kweli baada ya kunizuga kwa kumtukana, alimpigia simu mwandishi na kucheka baada ya mimi kuondoka" – Diamond

  "Niliamua kuwa kwenye mapenzi na Wema na kujipa moyo kwamba nitairekebisha tabia yake, na nilikua napigiwa simu na watu mbele yake wakiniambia ananiharibia nyota mpaka analia yani, nikawa namsafisha kwa watu kwamba hayuko hivyo mpaka watu wakaanza kupenda uhusiano wetu, kumbuka baada ya yeye kuachana na Kanumba alikimbia kwenda Marekani, akarudi tena bongo na kuanza kunitongoza kwenye facebook kwa sababu alikua anajiuliza ataanza kutoka na nani ili azidi kupata umaarufu" – Diamond

  Leo kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM Diamond ataendelea kufunguka Exclusive mambo mengine hakutaka kuyasema kwenye Media lakini imebidi kwa sababu Wema ameshindwa kujiheshimu na kutaka yeye aonekane mbaya, atataja pia moja kati ya tukio la ajabu alilowahi kulishuhudia kwa Wema lakini hakulisema wala halikuharibu chochote kwenye uhusiano wao, Diamond atafunguka pia kuhusu rekodi ya Mauzo aliyoivunja kwenye show ya Mlimani City.

  (AMPLIFAYA ni saa 1 usiku mpaka saa 3)   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mna kazi!!!
   
 3. B

  Beibe Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mwanadada nadhan hayuko good upstairs kama diamonds anachosema ni ukweli.
   
 4. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 2,472
  Trophy Points: 280
  Utumbo mtupu.hamna lolote hapo
   
 5. TZ boy

  TZ boy JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 622
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Xafi xna makavu LIVE...Maana "'Huyu dada Hana hata chembe ya Aibu puuuh...
   
 6. e

  evvy Senior Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona utaaaaaaaaaaaaaaam....,,
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,510
  Likes Received: 2,250
  Trophy Points: 280
  Hawa nao wamekutana kopo na mfuniko! Wallah kuna watu wanazaa kuepuka chango la undele! Aagghhhrrr!
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  watajijuuuuuuuuuuuuuuu
  tumewachokaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

  wabadili tabia
   
 9. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #9
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  nasubiria hapa nimsikilize diamond kama nilivyomsikiliza wema kwa masikio yangu, then nita-judge nani ana ubongo wa ndege kati yao
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hawa watoto wote wamenichosha hawana adabu..huyu anasema hili ,mwingine anasema vile ... ukiangalia kwa umakini wote wana matatizo...
   
 11. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Mhhhhhhh, mambo ya mahabati hayo.
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Apr 4, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Wema si mzima kabisa kichwani!
   
 13. B

  Beibe Member

  #13
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru NN hata wewe umeliona hilo, yan akiwa kwenye zile filamu zetu sasa si ndo utasema mtu ndo huyu,....yan sasa hivi kila anachokifanya yan ni ful kuigiza anajisahau kuwa sa ingine anakua kwenye real life
   
 14. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,696
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Wote hawako vizuri kichwani..kuna haja ya kuwaacha kuliko kuwapa attention maana wataendelea kuharibu.
   
 15. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #15
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Si umewafuata wenyewe wabana puwa huku, au haujui kama hili ni jukwaa lao Masharouharo?
   
 16. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #16
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Vijana wa mjini mna mambo mengi sana.
   
 17. Eversmilin Gal

  Eversmilin Gal JF-Expert Member

  #17
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 783
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  duh ....maskin Wema
   
 18. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #18
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kisauti
   
 19. serio

  serio JF-Expert Member

  #19
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 5,927
  Likes Received: 1,139
  Trophy Points: 280
  as the twig is bent, so shall the tree grow..
   
 20. Muuza Sura

  Muuza Sura JF-Expert Member

  #20
  Apr 4, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,990
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Huyu ndo diamond nayemjua sasa!
   
Loading...