Hiki ndicho wasichoelewa watanzania wengi mpaka sasa hivi...

Mh JPM alianza kampeni zake kwa kusema hapa kazi tu,ameisafisha nchi na anaendelea kuisafisha mpaka sasa,Huduma za Jamii zimekuwa vizuri,nidhamu maofisini ipo sasa hivi,humu ndani wote mashahidi,lakini kitu nilichokioana kwa watanzania wengi ni wanafiki na wamejaa ushabiki wa kijinga na wenye kupoteza muda,,,hebu tujiulize yule mtu ambaye hapo awali alikuwa anafanya shughuli yake halali na kulipa kodi ameingiliwa? La hasha kazi imeendelea na Maisha yake yanasonga,mtumishi aliyekuwepo ofisini kihalali na mshahara wake ukiwa unaingia kama kawaida mpaka sasa hivi Luna kitu kimemuathiri? La hasha yote yako sawa.Sasa watanzania tunataka nini tena,JPM wakati wa kampeni zake alishasema maswala ya mikataba ya madini,jamani tuwe wepesi wakukumbuka mambo!!! Kiongozi wetu anafanya haya yote kwa manufaa ya nchi yetu sote,ni lini Magufuli huyu akamchukia mpinzani na wakati akiwa anashukuru baada ya kupita uraisi alisisitiza yeye ni rais wa wote na muda wa siasa ushapita na wote ni kitu kimoja,na ndio maana hata majimbo ya wapinzani alipita na kupata ushirikiano,na isitoshe Magufuli kakaa bungeni na wabunge wote wanafahamiana vizuri kabisa.Yatupasa tumsome na tujue anataka nini huu ni muda wa kusonga mbele na kuijenga nchi yetu.Huku kujifanya kila kitu ni kupinga na kuonekana kwenye media ni upuuzi.Mazuri ya nchi yanakuja...TUBADIRIKE NA KUSOMA NYAKATI.Rais wetu Fanya kazi huu ni wakati wa mapambano na ni vita kubwa ya kuipeleka mbele nchi yetu..Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Serikali yeu.

Sukari kaingia bei ya 1kg = Tshs 1,600 - 1,800.....

Tangu kaingia akaharibu kwa kupandisha bei. Leo ni kati ya Tshs 2,500 - 3,000 kwa kilo!!!

Unasemaje eti!!?? Huduma ktk maofisi ya umma ni nzuri?

Acha kudanganya watu.

Inaonesha wewe ndiye miongoni mwa wale "watu wasiojulikana" mnaotetea utawala huu kwa nguvu kuuubwa hata kwa kumwaga damu za watu siyo??

Kama unataka kuelewa kuwa mambo ni "business as usual ", tembelea maeneo ya sekta huduma za afya na maji na umeme (nishati)

Afya...

Bado tatizo la dawa hasa ktk vituo vya afya na zahanati za vijijini liko palepale. Sijui hospitali za mijini kwa sbb mimi siishi mjini DSM ama Dodoma nk, mimi ninaishi zangu ktk moja ya vijiji huku Shinyanga....

Ku - terrorise watumishi wa umma kama manesi, madaktari,walimu nk ili wafanye kazi zao kwa woga (nidhamu ya woga), si ishara ya kuboreka kwa huduma za kijamii, bali ni kudidimiza kabisa ubora wa huduma za kijamii...!!

Kama unajisifu kwa hili, nakusikitikia sana kwa sbb utakuwa u kipofu wa ufahamu na fikra wewe...!!

Nishati/umeme....

Bado si reliable. Umeme unakatikatika hovyo na huku vijijini ndiyo basi kabisa. Yaani nguzo na nyaya zilizosambazwa vijijini ni kama mapambo tu. Huku kijijini mkubwa mnaweza kukosa umeme hata kwa siku mbili bila maelezo yoyote toka kwa wahusika...

Hii haiitofautishi awamu hii ya Magufuli na zilizopita ktk eneo hili kwa sbb mtindo wa utoaji huduma bado ni uleule, hakuna tofauti yoyote ile kama unavyojaribu kurusha rusha vijisifa hewa ambazo kiukweli hizi ni political propaganda ambazo siku zote huwa ziko mbali na ukweli na uhalisia halisi wa mambo...

Na katika eneo hili la nishati/umeme, ishu si kufanya maonesho ya nguzo na nyaya za umeme huko vijijini, bali tunataka umeme unaowaka 24hrs na wa bei nafuu (affordable) kwa wananchi maskini wa nchi hii ili wapikie waokoe mazingira, wasukume maji na kumwagilia bustani hata mashamba yao....!!

Maji....

Hapa ndio balaa Kabisa.. Njoo huku vijijini uone kina mama, watoto, wababa wanavyopata shida ya kutafuta maji yalipo....

Unafahamu kuwa kuna baadhi ya maeneo mengi sana vijijini wanapata huduma ya maji umbali wa zaidi ya kilometa 10 baada ya miaka zaidi ya 50 ya uhuru??

Unafahamu kuwa maeneo mengi ya nchi kuna mabomba na visima vya maji ya kupampu ambayo ni mapambo tu lakini hakuna/hayatoi maji na wakati huohuo kitakwimu wanahesabu wanatoa huduma ya maji ya bomba??

Tena kwa taarifa yako haya hata hayajafanyika wakati huu wa Magufuli bali ni miaka 10 ama 7,6 iliyopita....!!

Huyu ndugu yako Magufuli tangu aingie madarakani hana analolifanya kwa sasa zaidi ya wimbo usio na radha wa viwanda, kukimbizana na akina Lissu, makinikia, watumishi hewa, hewa hewa nk badala ya kujikita na utoaji wa huduma za kijamii (watu) .....

Hoja yangu hapa ni kukataa hiki ulichokileta hapa kwa sbb, there is no any difference since then.... Hakuna tofauti kwa sbb CCM haijabadilika, ni ileile na sera zake ni zilezile zenye very low impacts ktk maisha ya watu...!!

Tofauti pekee inayoonekana hata kama utabisha ni kuzidi kutokomea kwa moyo wa kujitoa na kujitolea wa watanzania, chuki na visasi kuongezeka miongoni mwetu, uhasama, mauaji yasiyo na maelezo na mgawanyiko mkubwa miongoni mwa wanajamii jambo ambalo si utamaduni wa watanzania.....

Mwisho umesifu kuwa sasa Taifa linapata mapato ya kutosha kutokana na serikali chini ya Magufuli kudhibiti mianya ya ukwepaji ulipaji kodi na kuondoa biashara bandia (zisizo halali). Hii maana yake mapato ya serikali yameongezeka kulinganisha na enzi za Jakaya Kikwete at the same time kiwango cha uwekezezaji (wigo wa walipa) kikiwa kilekile/uleule.....

Swali fikirishi kwako ni hili:

Wakati wa Jakaya Kikwete ama Benjamini Mkapa mapato yalikuwa ni kidogo kulinganisha na makusanyo anayofanya sasa huyu unayemsifia.....

Mbona hawa walifanya mageuzi makubwa sana ya kiuchumi na kijamii huku wakiwa na fedha (Mapato) kidogo kulinganisha na Magufuli?

Kwa namna Magufuli anavyojisifu na nyie kumsifu ktk eneo hili, ni wazi ktk miaka yake hii miwili tu aliyokaa madarakani, tungelishaona mabadiliko makubwa sana ya maisha ya kiuchumi na kijamii ya nchi kwa ujumla na mwananchi mmoja mmoja. Lakini hali ilivyo na hata wewe ukiwa mkweli kwa nafsi yake iko tofauti kabisa kwani malalamiko ya hali ngumu ya kimaisha ni kila mahali vijijini na mijini....!!

Ni wakati wa kina Benjamini Mkapa na Jakaya Kikwete, hizi barabara za lami zilijengwa, viwanda vilivyopo, waliboresha maslahi ya watumishi kwa karibu kila mwaka kwa vitendo na si kwa maneno kama huyu jamaa yenu huku akiwa na visingizio kibao.

Ni kwa sbb gani eti??

Hebu tuambie wana jukwaa wenzako, ni economic projects ngapi mpya (ukiachilia mbali hizi za ufadhili wa fedha za kigeni) zimeanzishwa na kukamilishwa chini ya Magufuli???

Hakuna. Bali ni taabu na kilio kila mahali.

Na ndiyo maana huyu jamaa yenu Pombe Magufuli anajaribu kuzima kila aina ya sauti za ukosoaji na zilizo kinyume naye kwa sbb hofu yake ni kuogopa kuibuliwa kwa udhaifu na mapungufu kama haya.....

Hana lolote huyu na kama unabisha, miaka mitano ya uwepo wake ktk madaraka inapita kama upepo na hatakuwa hata cha kuonesha asipojirekebisha na badala yake, damu za watu wasio na hatia anaowatesa na kuwaua ndizo zitakazokuwa zinamlilia toka ardhini....!!
 
Back
Top Bottom