Ushimen
JF-Expert Member
- Oct 24, 2012
- 37,203
- 85,311
Nilikuwa nimekaa kibaruwani, na kwakuwa miezi hiyo haikua na michongo ya kazi za nje/mikoani....
Nilijikuta napata wazo la kufanya kitu, kisha nika chukuwa kalamu na karatasi na nikaweka mchoro wa kile nilichukuwa nakiona kwenye taswira. Basi mzee nikatekenya chuma huyooo nikaenda kwa shop ya jamaa anauza rejected metals.
Basi nikakusanya vipande vya chuma pamoja na vipande vya mbao, kadri nilivyo ona zitanitosha kwenye mahitaji yangu.
Day one and two, niliifanya kazi hadi ikafikia kuwa na muonekano wa chuma kisicho eleweka na nikakipaka rangi ya kuzuwia kutu.
Day three and four, nilimalizia kwa kukipaka rangi ambayo nili ikusudia uwe muonekano kwa kitanda cha mtoto. Kisha nikamalizia kwa kukata mbao kwa vipimo maalum kwaajili ya chaga na ngazi kwaajili ya mtoto kupanda wakati wa kuenda kulala.
Baada ya kukamilisha hayo, nilikipeleka nyumbani na kisha kijana akajaribisha kupanda ngazi kwa uangalifu na uoga, na akiwa ameshikilia handrails nilizo zitengeneza kwa kusudio la kumkinga asiweze kuanguka wakati wa kupanda ngazi. Baada ya hapo nilienda kununua godoro dogo kwa kipimo ambacho nilikuwa nimetengenezea kitanda hicho, na kisha nikaenda kwa fundi wa kushona seats covers na akaniundia cover iliyo tosha godoro la kitanda.
Leo nimekiweka kitanda cha kijana uoande wa miguuni pa kitanda changu, na dogo analala kwa raha burdan na akifurahia kazi ya mikono ya baba yake.