Hiki ndicho kilichowaangusha CHADEMA - Wanachama wake!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Moja kati ya sababu ya kuanguka kwa chama cha chadema kwenye chaguzi mbali mbali zilizopita ni wanachama wake kushindwa kuelewa wanataka nini na hivyo kushindwa kuwashawashi Watz wengine ambao walikuwa bado hawajaamua Chama kipi wakichague!

Ilikuwa ni kawaida ukiongea na Mwanachadema sababu za kuichagua chadema atakwambia CCM watoke tu basi hakuna kingine hata kama likija jiwe tutalichagua lkn cha muhimu CCM itoke, sasa hii sababu ni ndogo sana kuweza kuwashawishi watu wenye akili zao kuichagua chadema!

Hivyo chadema jifunzeni kuwa na sera ambazo zinaeleweka na kwamba zinauzika na siyo kuwaambia watu kwamba sababu ya kuichagua chadema ni CCM imetawala muda mrefu hivyo basi ni lazima itoke, hiyo siyo sababu ya kunishahiwishi kuichagua chadema, bali ni hisia tu na nchi haiwezi kuongozwa na hisia tunataka sera zilizotulia na kueleweka na pia kuwa na uwezo wa kujibu maswali magumu na siyo majibu kama watoke tu basi, hilo haliwezi kuwapa ushindi kamwe!
 
Jazba na ujengaji hoja ni vitu viwili tofauti. Matusi na uwezo wa kuingiza fikra zako ndani ya kichwa cha mtu ambaye humjui kabisa na unakutana naye kwa mara ya kwanza, ni vitu viwili tofauti. Kibaya zaidi wanakuwa wanabebwa na hisia badala ya kutafuta mbinu mbalimbali za kujenga hoja. Lakini kumlaumu mwanachadema ni kumuonea, mgombea wao kashindwa kuongea kama mtu ambaye kweli anafanana na nia walizokuwa nazo wale wote waliokuwa tayari kumuunga mkono.

Lowassa alikosa ushawishi wa ziada ili aweze kupata kura nyingi zaidi. Akabakia kuomba kura za mahaba, lakini mahaba ni kitu cha ziada, kwanza unaanza ushawishi wa mgombea mwenyewe. Huwezi ukayapata mahaba bila ya kwanza kuonyesha kupitia nguvu ya hoja zako, ni namna gani wewe kama mgombe una kitu kipya kwa walio wengi. Lowassa kabebwa na uwezo wa usimamiaji wa masuala ya logistics ambao wasaidizi wake walikuwa nao, vinginevyo hata hizo kura milioni sita kuweza kuzipata katika hali aliyokuwa nayo kipindi chote cha kampeni, ni kwamba kazi ngumu imefanyika.

CHADEMA wajipange, na huu ndio muda wa kuingiza damu mpya, damu ambao mpaka mwaka 2020 itakuwa imeshakiuza chama katika muonekano mpya wa kiushindani. Vinginevyo kutegemea jazba, matusi, dharau na kebehi, hakuwezi kuipatia CHADEMA nafasi ya kuwaongoza Watanzania. Ni kosa kubwa sana kumdharau mtu wa hali ya chini, huku ukifikiri kuwa hana uwezo wa kuyapima mambo kadri anavyoyaona.
 
Moja kati ya sababu ya kuanguka kwa chama cha chadema kwenye chaguzi mbali mbali zilizopita ni wanachama wake kushindwa kuelewa wanataka nini na hivyo kushindwa kuwashawashi Watz wengine ambao walikuwa bado hawajaamua Chama kipi wakichague!

Ilikuwa ni kawaida ukiongea na Mwanachadema sababu za kuichagua chadema atakwambia CCM watoke tu basi hakuna kingine hata kama likija jiwe tutalichagua lkn cha muhimu CCM itoke, sasa hii sababu ni ndogo sana kuweza kuwashawishi watu wenye akili zao kuichagua chadema!

Hivyo chadema jifunzeni kuwa na sera ambazo zinaeleweka na kwamba zinauzika na siyo kuwaambia watu kwamba sababu ya kuichagua chadema ni CCM imetawala muda mrefu hivyo basi ni lazima itoke, hiyo siyo sababu ya kunishahiwishi kuichagua chadema, bali ni hisia tu na nchi haiwezi kuongozwa na hisia tunataka sera zilizotulia na kueleweka na pia kuwa na uwezo wa kujibu maswali magumu na siyo majibu kama watoke tu basi, hilo haliwezi kuwapa ushindi kamwe!
chadema na ukawa kwa ujumla wanajua vizuri sana wanachokitaka, KUWA WAPINZANI WA AERIKALI.
 
Bao la mkono je?
 
Mmekua nchi kwa kubaka demokrasia time wanyamazia.Maelezo mengi ambayo tumechoka kuyasikia. Inaonyesha ni jinsi gani hamjiamini kwa kutaka kutuaminisha kwamba mmshinda kihalali. Ukawa ipo imara sana subirini 2020 hatutakubali kupelekwa km mlivyo kwa kutumia nguvu ya dola.
 
Huu msemo kama nilishwahi kuusika mahali mara kadhaa kuanzia 2000-2005-2010-2015 na sasa umehamia 2020!
 
Back
Top Bottom