Hiki ndicho kilichojiri sakata la Escrow

Jenerali Ambamba

JF-Expert Member
Sep 8, 2014
3,311
2,000
MAELEZO KUHUSU MALIPO YA FEDHA KUTOKA KATIKA AKAUNTIMAALUM (ESCROW ACCOUNT)


1.0. Utangulizi


Mnamo tarehe 26 Mei, 1995,Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kampuni ya Independent Power TanzaniaLimited (IPTL) waliingia katika Makubaliano ya Ununuzi wa Umeme (Power PurchaseAgreement – PPA), uliokuwa unazalishwa na IPTL huko Tegeta, Dar es Salaam.Makubaliano haya yalikuwa ni ya miaka 20.

Chini ya Makubaliano hayo,malipo ambayo TANESCO ingeyafanya kwa IPTL yalikuwa ya aina mbili:

(i)Malipo ya manunuzi ya umeme– Energy Purchase Price;

(ii)Malipo ya kiwango chamalipo ya uwekezaji – Capacity Purchase Price au Capacity Charge.

Baada ya miaka kadhaa, IPTL naTANESCO waliingia katika mgogoro mkubwa kuhusiana na ukokotoaji wa kiwango chamalipo ya uwekezaji na mgogoro huu uliwasilishwa katika Mahakama ya Usuluhishiwa Migogoro ya Kibiashara – ICSID. Kutokana na hatua hii, TANESCO walitumiahaki yao chini ya PPA kutoa Notisi ya Pingamizi la Malipo (Invoice DisputeNotice), sambamba na kuomba kufunguliwa kwa Akaunti Maalum (Escrow Account),ili malipo yote kwa “Disputed Invoices” yalipwe kwenye akaunti hiyo hadi palemigogoro hiyo itakapotatuliwa.

2.0.Escrow Account

Tarehe 5 Julai, 2006, Serikaliya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Nishati na Madini (GoT);IPTL na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) waliingia katika makubaliano ya kufunguaAkaunti Maalum (Escrow Account) ambapo GoT ingetekeleza Makubaliano yaUtekelezaji (Impelmentation Agreement) chini ya PPA kwa kuweka fedha katikaakaunti maalum. Fedha hizo zingeendelea kushikiliwa na BoT mpaka pale IPTL naGoT wangekuwa wamemaliza tofauti zao kuhusu viwango vya malipo ya uwekezaji.
Kwa mujibu wa Kifungu 7.7 chaMakubaliano ya Ufunguzi wa Akaunti (Escrow Agreement), fedha zilizomo kwenyeAkaunti hiyo zingeendelea kuwepo na kuwa katika mamlaka ya “Escrow Agent”, nakwamba fedha hizo zingetolewa tu kama kuna hukumu ya Mahakama inayoamurukutolewa kwake au kama pande mbili za Makubaliano (IPTL na GoT) zitawasilishamakubaliano yanayoridhia kutolewa kwa fedha hizo kwa upande uliotajwa katikaMakubaliano hayo. Kifungu hicho kinasomeka kama ifuatavyo:

“In the event of any Dispute between the other Partieshereto resulting in adverse claims or demands being made in connection with theEscrow Account, or in the event that the Escrow Agent in good faith is in doubtas to what action it should take hereunder, the Escrow Agent shall be entitledto retain the Escrow Account until the Escrow Agent shall have received (i) afinal award of the arbitrator pursuant to Section 8.6 hereof directing deliveryof the Escrow Account (or funds therein) or (ii) a written agreement executedby the other Parties hereto directing delivery of the Escrow Account (or fundstherein), in which event the Escrow Agent shall disburse the Escrow Account (orfunds therein) in accordance with such order or agreement. Any arbitrator’saward shall be accompanied by a legal opinion by counsel for the presentingParty reasonably satisfactory to the Escrow Agent to the effect that such awardis final and non-appealable. The Escrow Agent shall act on such award and legalopinion without further question”.

3.0.Uamuzi wa Mahakama

Tarehe 5 Septemba, 2013,Mahakama Kuu ya Tanzania ilitoa uamuzi uliogusa umiliki wa fedha zilizopokatika Akaunti Maalum iliyokuwa chini ya udhibiti wa BoT. Uamuzi huu uliotokanana maombi yaliyokuwa yamefanywa na mmoja wa wanahisa wa IPTL – VIP Engineering& Marketing Limited (VIP) ambaye aliiomba Mahakama iridhie kufutwa kwashauri ambalo VIP walikuwa wamelifungua Mahakamani (Misc. Civil Application No.49/2002 & Misc. Civil Application No. 254/2003). Maombi hayo yalitokana namakubaliano ya mauzo ya hisa za VIP katika IPTL kwenda kwa kampuni ya PanAfrican Power Solutions (T) Limited (PAP). Katika uamuzi huo, Mahakama, pamojana mambo mengine iliridhia kufutwa kwa mashauri hayo na kuelekeza kwamba malizote za IPTL, kikiwemo kiwanda cha kufua umeme zikabidhiwe kwa mmiliki mpya waIPTL ambaye ni PAP.
Baada ya uamuzi huo waMahakama, BoT ilipokea mawasiliano mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati naMadini (MEM) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao walikuwa na maonikwamba fedha zilizopo kwenye Akaunti Maalum zitolewe baada ya masharti kadhaakutekelezwa. Baadhi ya masharti hayo ni kama ifuatavyo:
Utolewe ushahidi kwamba PAP ndiyo wamiliki wa hisa zaMechmar katika IPTL;
Kufikiwa kwa muafaka wa mgogoro wa ukokotoaji wakiwango cha Malipo ya Uwekezaji kati ya IPTL na TANESCO;
Hakikisho kwamba baada ya kulipwa kwa fedha hizo, IPTLhawatadai chochote kuhusiana na tozo zinazobishaniwa.

4.0. Mkutanowa MEM

Tarehe 24 Septemba, 2013,Katibu Mkuu MEM aliitisha mkutano kwa ajili ya kujadili maombi ya Serikali yakuruhusu kutolewa kwa fedha za escrow. Mkutano huu ulimshirikisha Gavana waBoT, Katibu Mkuu Hazina (PST), Mwakilishi wa AG na wawakilishi wa TANESCO.Katika mkutano huu, BoT ilitoa hoja ambazo ilitaka zizingatiwe kabla yakutolewa kwa ruhusa ya kutolewa kwa fedha hizo. Hoja hizo ni:

(i)Ushahidi kwamba hisa zaMechmar zinamilikiwa na PAP na
ushahidi kwamba umiliki huoumesajiliwa na BRELA;
(ii)Ushahidi wa suluhu yamgogoro kuhusu tozo kati ya IPTL na TANESCO na kwamba suluhu hiyo imeamuliwakwa manufaa ya
IPTL;

(iii)Iwapo IPTL na GoT wakotayari kusamehe riba inayotolewa kwa
dhamana za Serikali ambakofedha za “Escrow” zimewekezwa,
endapo uwekezaji katikadhamana hizo utakatizwa kabla ya
wakati (pre-matureredemption);

(iv)Nini kauli ya Wizara yaFedha kuhusiana na uamuzi wa kutolewa
kwa fedha hizi na iwapouongozi wa Kitaifa una habari na suala
hili; na

(v)Iwapo GoT imejihadhari nauwezekano wa madai yanayoweza
kufunguliwa na wadaimbalimbali, wakiwemo Standard Chartered Bank (Hong Kong) ambao wanasemekanakuidai IPTL.

4.1. Timuya Wataalam

Baada ya majadiliano,iliagizwa kwamba iundwe Timu ya Wataalam ili kuzifanyia kazi hoja zilizoibuliwana kujadiliwa, na kuwasilisha Ripoti kwa PS – MEM kwa ajili ya hatua muafaka.BoT iliwakilishwa katika timu hiyo ambayo iliwasilisha Ripoti yake tarehe 30Septemba, 2013, ikiwa

na mapendekezo yaliyohitajikufanyiwa kazi kabla ya kutekelezwa kwa uamuzi wa mahakama kuhusu kutolewa kwafedha. Mapendekezo hayo yalishabihiana na hoja zilizokuwa zimetolewa na BoT.

5.0.Barua za AG na PS - MEM

Kufuatia kuwasilishwa kwaRipoti hii ambayo nakala zake zilisambazwa kwa wadau wote, BoT ilipokea nakalaya barua ya tarehe 7 Oktoba, 2013, iliyotoka kwa AG akielezea msimamo wakekuhusiana na yale yaliyoelezwa na timu ya wataalam. Katika ushauri wake, AGalishauri kwamba, baada ya kufikia muafaka kuhusu mgogoro wa tozo kati ya IPTLna TANESCO, fedha zilizomo katika Escrow Account zilipwe kwa IPTL kama uamuziwa Mahakama ulivyoelekeza.
Tarehe 15 Oktoba, 2013, BoTilipokea nakala ya barua iliyoelekezwa kwa PST, ikinukuu ushauri uliotolewa naAG (kwa barua iliyotajwa hapo juu) na kushauri kwamba uamuzi wa Mahakamautekeleze ili kuiondolea Serikali madhila ya mashauri yanayoweza kuepukika.Barua hii iliandikwa na PS – MEM.

6.0. Makubalianoya Kutoa Fedha

Tarehe 21 Oktoba, 2013, GoT naIPTL walisaini Makubaliano ya Kutoa Fedha zilizomo katika Escrow Account ilizilipwe kwa IPTL. Makubaliano hayo yalijulikana kama “Agreement for Delivery ofFunds to Independent Power Tanzania Limited”. Makubaliano hayo yaliambatana naMuhtasari wa kikao cha pamoja cha uhakiki wa malipo ya tozo kati ya IPTL na TANESCO,pamoja na barua ya PS – MEM, ikiwasilisha Makubaliano hayo na kuiomba BoTiliruhusu malipo hayo kwenda IPTL kama uhakiki ulivyobainisha.

7.0.Ushauri wa kuujulisha uongozi wa Nchi

Mnamo tarehe 24 Oktoba, 2013,BoT ilimuandikia PST, ikimuomba kuchukua hatua kadhaa kuhusiana na malipo yaIPTL. Miongoni mwa mambo yaliyoshauriwa na BoT yalikuwa ni:
(i) Kwamba ufungaji wa EscrowAccount uzingatie kwamba mamlaka ya kufanya hivyo yako kwa Paymaster General;
(ii)Kwamba, kwa kuzingatiaunyeti wa suala hili na ukubwa wa malipo husika, Waziri wa Fedha apate fursa yakuwajulisha Mheshimiwa Rais na Mheshimiwa Waziri Mkuu ili waeleze kamawanaridhia au la; na
(iii)Kwamba GoT iombe kutolewakwa kinga itakayoikinga GoT dhidi ya madai yanayoweza kujitokeza baada ya malipohayo kufanyika.

8.0.Kinga dhidi ya Madai na Mashtaka

Baada ya kupokea maombi hayo,BoT ilisisitiza kwamba ingependa kupata hakikisho kwamba baada ya malipo hayo,hakutakuwa na madai au mashtaka yoyote dhidi yake au GoT. Kutokana na msisitizohuo, tarehe 27 Oktoba, 2013, IPTL ilitoa hati ya Kinga (Indemnity) ambayoiliikinga BoT pamoja na GoT dhidi ya madai yote, ya sasa na ya baadae, mashauriya kisheria, pamoja na kuahidi kuzifidia BoT na GoT gharama na tozo zozoteambazo zitawagharimu au zitakazotokana na uamuzi wao wa kuruhusu kuchukuliwakwa fedha za Escrow au sehemu ya fedha hizo, kwa mujibu wa Makubaliano ya KutoaFedha.

9.0.Maombi ya TRA kuhusu VAT

Kwa barua iliyoelekezwa kwaPST na nakala kwa Gavana wa BoT, Mamlaka ya Mapato (TRA) iliomba msaada wa PSTkatika kukata kiasi cha Shilingi 26.9 bilioni, kama Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) kwa malipo ambayo yaliwekwa kwenye Escrow Account. Kiasi hichokilikokotolewa kutoka katika kiasi cha Shilingi 176,649,195,314.00 ambachokilikadiriwa kuwepo katika Escrow Account.
Hata hivyo, katika ushauriambao ulitolewa na AG tarehe 18 Novemba, 2013, ilielezwa kwamba malipo yaCapacity Charge hakikuhusisha VAT na kwamba kiasi chote kilichokuwamo katikaEscrow Account kilikuwa ni malipo ya IPTL pasipo na VAT. Ushauri wa AGulitokana na barua ya BoT na ile ya PST ambazo ziliomba ufafanuzi kuhusu sualahilo kabla ya uhamishaji wa fedha kwenda IPTL.

10.0. Kibali cha kuhamisha fedha kwenda IPTL


Mnamo tarehe 14 Novemba, 2013,PST aliwasilisha kwa utekelezaji, maagizo ya Mheshimiwa Rais ambaye aliagizakwamba “Maamuzi ya Mahakama Kuuyatekelezwe kama alivyoshauri AG”. Maagizo ya Mheshimiwa Raisyaliwasilishwa kwa PST kwa barua ya tarehe 13 Novemba, 2013, na ilisainiwa naKatibu wa Rais, Bwana Prosper Mbena.

Baada ya kupata maelekezohayo, BoT ilimwandikia PST, ikiomba muongozo kuhusiana na suala la madai ya TRAkuhusiana na VAT. Barua hii iliandikwa tarehe 15 Novemba, 2013, na nakala yakekupelekwa kwa AG, na ilizingatia ukweli kwamba madai ya kodi za Serikaliyanachukuliwa kama madai yenye umuhimu wa juu (first charge) katika malipoyoyote.

Ni barua hii ndiyo iliyoletaufafanuzi wa AG - kwa barua yake ya tarehe 18 Novemba, 2013 - ambao ulisisitizakwamba malipo ya capacity charge hayakuwa na VAT na kwamba fedha zihamishwekwenda IPTL bila kukata fedha za VAT.

11.0. Utekelezaji wa maagizoya kuhamisha fedha

Kama ilivyoelezwa hapo juu,fedha za capacity charge zilikuwa katika makundi mawili. Moja likiwa katikafedha za Kitanzania, wakati kiasi kingine kilikuwa katika dola za Marekani.Makundi haya mawili ya fedha yalikuwa yamewekezwa katika uwekezaji wa ndani nawa nje, kwa kuzingatia kifungu 3.4 cha Escrow Agreement.
Kiasi kilichokuwa kimewekezwanje ya nchi kilikuwa ni dola za Marekani 22 milioni, wakati fedha za Kitanzaniaziliwekezwa katika hati fungani za siku 182, ambapo kiasi cha shilingi148,071,613,572.93 kiliwekezwa. Kiasi kingine cha shilingi 8,020,522,330.37,kilikuwa ni salio katika akaunti, kwa vile kiliwasilishwa baada ya kuwauwekezaji umeshafanyika. Mpaka kufikia tarehe 25 Novemba, 2013, salio katikadola za Marekani, pamoja na faida lilikuwa ni dola 22,198,544.60, wakati saliokatika fedha za Kitanzania lilikuwa ni shilingi 161,389,686,585.34,likijumuisha na faida katika uwekezaji ambayo ilikuwa shilingi5,297,550,682.04.
Kwa barua ya tarehe 25Novemba, 2013, BoT iliwasiliana na IPTL, ikiijulisha kuhusiana na saliolililokuwepo kwenye Escrow Account mpaka kufikia tarehe hiyo, na kutoamapendekezo kuhusiana na namna ambavyo malipo ya fedha hizo yangefanyika.Katika barua hiyo, BoT ilitoa mapendekezo kadhaa kwa IPTL. Mapendekezo hayoambayo yalizingatia “macro stability position” ya nchi, yalikuwa ni kamaifuatavyo:
Page 8 of 12
(i) Kwamba Malipo ya Dola 22,198,544.60 yalipwe mara moja
ifikapo tarehe 26 Novemba,2013;

(ii)Kwamba umiliki wa hatifungani zilizokuwa hazijaiva uhamishwe
kutoka BoT kwenda IPTL;

(iii)Kwamba ulipaji wauwekezaji huu ufanyike kila hati inapoiva na
kama kutakuwa na ulazima wakuvunja uwekezaji kabla ya muda wa kuiva kufika basi hilo lifanyike baada yatarehe 1 Januari, 2014 ili kuepuka kuongeza ujazi uliopitiliza wa fedha katikauchumi, hasa katika mwezi wa Desemba, 2013; na

(iv)IPTL itoe taarifa zakibenki ili kuwezesha uhamishaji wa fedha zilizotajwa katika kipengele (i) hapojuu kwenda IPTL.
IPTL ilikubaliana na ushaurihuu kwa barua yao ya tarehe 25 Novemba, 2013. Ushauri huu wa BoT ulirudiwa tenakatika kikao cha pamoja kati ya Uongozi wa juu wa BoT na mwakilishi wa IPTL,kilichofanyika tarehe 26 Novemba, 2013 ambapo iliazimiwa kwamba:

(i)Kwamba baada ya kupokeamaelekezo kutoka IPTL, BoT itashauri
juu ya utaratibu unaotumikakatika kuhamisha umiliki wa hati
fungani (Treasury Bills); na

(ii)Kwamba IPTL iwasilishebarua ya maelekezo ya kuhamisha fedha
zilizokuwemo katika EscrowAccount. Barua hiyo ihusishe pia maombi ya kuhamisha hati fungani.
IPTL, kupitia barua ya tarehe28 Novemba, 2013, ilielekeza yafuatayo (nanukuu)

“RE: DELIVERY OF FUNDS IN THE TEGETA ESCROW ACCOUNTS please refer toyour letter dated 25th November 2013 Ref: No. NC. 53/135/068/11/14 and themeeting held at your office.
A) USD ESCROW ACCOUNT
Page 9 of 12
Kindly transfer the sum of USD22,198,544.60 to our account of PAN AFRICA POWER SOULTIONS (T) LTD, c/o IPTLUSD A/C NO. 9120000125324 STANBIC BANK TANZANIA LIMITED
SWIFT CODE: SBICTZTX
B) TZS ESCROW ACCOUNT Kindlytransfer the sum of TZS 8,020,522,330.37 to our account of PAN AFRICA POWERSOULTIONS (T) LTD c/o IPTL TZS A/C NO. 9120000125294 STANBIC BANK TANZANIALIMITED SWIFT CODE: SBICTRZTX
C) Further more kindly arrangeto transfer all the Treasury Bills from Bank of Tanzania Escrow Account to PANAFRICA POWER SOULTUIONS (T) LTD c/o IPTL AS PER THE High Court of Tanzaniaruling dated 5th September 2013.
Your kind assistance towardsthe above will be highly appreciated” (mwisho wa kunukuu).
Wakati malipo ya fedhataslimu, yaani dola 22,198,544.60 na shilingi 8,020,522,330.37 yalilipwa tarehe28 Novemba, 2013, uhamisho wa hati fungani ulifanywa tarehe 5 Desemba, 2013,ulihitimisha jukumu wa BoT kama Escrow Agent. Tarehe19 Desemba, 2013, BoTilimuandikia PST kuomba kufungwa rasmi kwa Escrow Account, kwa vile madhumuniya kufunguliwa kwake yalikuwa yametimizwa na kufika mwisho.

12.0. Hitimisho

Ieleweke kwamba katikakutekeleza wajibu wake kama Escrow Agent, BoT ilikuwa ikiwajibika kwa kufuatamatakwa ya Makubaliano ya kutunza fedha hizo (Escrow Agreement). Makubalianohayo yalitoa haki na wajibu wa kila upande, na kwa upande wa BoT, wajibu huoulihusisha kuzitunza fedha hizo na kuhakikisha kwamba hazitumiki nje yamadhumuni ya kuhifadhiwa kwake; kuwekeza katika miradi inayoruhusiwa, nakuziwasilisha kwa mmiliki aliyekubalika, pale matakwa ya Kifungu 7.7 chaMakubaliano hayo yanapokuwa yametekelezwa. BoT ilitekeleza majukumu hayo ikijuakwamba kama benki, jukumu la msingi na la asili ni kulipa pale inapotakiwakufanya hivyo, yaani payment on demand. Katika mazingira ya suala hili, demandilifanyika pale wahusika (IPTL na GoT) walipotekeleza matakwa ya kifungu 7.7kwa kuwasilisha makubaliano ya kukabidhi fedha IPTL.
Kwa kuwa BoT ilipewa jukumuhili kwa Makubaliano, uwajibikaji wake na mipaka ya uwajibikaji huo inabakikuwa ni ile iliyoelezwa kwenye Makubaliano hayo. Hata hivyo, BoT ilikwendambali kuhakikisha kwamba utekelezaji wa uamuzi wa Mahakama, pamoja naMakubaliano ya kukabidhi fedha unapata baraka za wakuu wa nchi kama vileMheshimiwa Rais na Waziri Mkuu. BoT pia ilihakikisha kwamba mahitaji yote yamsingi kama vile, Makubaliano ya Kuhamisha Fedha, kinga dhidi ya madai aumashitaka baada ya malipo, na suala la kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)vinapata ufafanuzi, baraka na muongozo unaostahili. Na hii ndiyo maanautekelezaji wa Uamuzi wa Mahakama ulichelewa kwa takribani miezi mitatu tokaulipoamriwa na Mahakama.
Tunahitimisha kwa kusemakwamba BoT ilitekeleza wajibu huu kwa uaminifu, weledi na uadilifu wa hali yajuu, na bila kukiuka vifungu vya Escrow Agreement.
BoT haihusiki na malumbano juuya wamiliki wa IPTL na uhalali wa umiliki wao wa hisa za kampuni hiyo. Vilevile, BoT haihusiki na uhalali wa madai ya wadeni wa IPTL, kwa vile wajibu wakekwa mujibu wa Makubaliano haukutakiwa kufika hatua hiyo.

Ni sisi Wazalendo wa Nchi hii.
Tunawasilisha.
 

Attachments

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom