Hiki ndicho chama cha siasa cha mwenyezi Mungu

Teacher1

JF-Expert Member
Jan 29, 2011
333
149
Misingi ya nchi yetu ilyowekwa na waasisi wa taifa hili haikujengwa katika misingi ya dini au madhebnu yoyote yale na kwa miaka mingi udini haukushabikiwa kabisa katika taasisi za serikali na hata vyama vyenye mitazamo ya kidini havikuruhusiwa. Kinacho nishangaza hivi karibuni walewale walioapa kuenzi misingi ya waasisi wamegeuka na kuanza kushabikia udini inamaana miaka yote hiyo waliamini wasicholijua? Au kwakuwa nyerere kafa alikuwa akiwalazimisha kondoa udini?

Kwanza ni nukuu zipi katika vitabu vitakatifu zinazo unga mkono siasa kuendana na dini zetu? Je MUNGU NI Mfuasi wa vyama vyet dhalimu vya kisiasa?.

Mwenyezi Mungu hawezi kuwa muumini wa siasa hizi za kibaguzi yeye chama anachokifuata ni kile kinachofuata haki, unyoofu wa moyo na utii. Mungu piga upofu wanaokusingizia kuwa wewe kuwa unabagua watu kwa misingi ya siasa.ibariki Tz kuwa na amani ondoa viongozi waliotayali kuvunja haki kwasababu ya kutaka madaraka.
 
Back
Top Bottom