Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,399
Leo mchana mjini Nairobi kumetokea mlipuko wa bomu karibu na hoteli ya kitalii katika eneo la WestLands.
Eneo khasa lilipotokea mlipuko huo ni lile la naba 14 Riverside ambako ipo hoteli ya Dusit D2 ambapo watu kadhaa wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Napenda kutoa salamu za rambirambi kwa wote walofariki kutokana na ajali hiyo na kuwaombea kupona haraka kwa wahanga wote wa tukio hilo.
Taarifa zilizopo hadi sasa ni kwamba bomu au mabomu (IED) yalilipuka kutoka ndani ya gari lililokuwa limepaki nje jengo hilo la Riverside karibu kabisa na hoteli hiyo ya Duset D2.
Vikosi vya usalama askari kanzu na vikosi maalum kutoka KDF walifika eneo la tukio kukabiliana na hali hiyo huku kikundi cha kigaidi cha Al-Shabab kikitoa taarifa ya kuhusika na bomu hilo.
Katika mambo ambayo yamenifanya niulize masuali kadhaa ya kiudadisi ni jinsi askari wa vikosi maalum vya KDF ambao walifika kwenye eno la tukio na kwa muda mrefu kukaa sehemu moja wakisubiri hatua ya kuingia ndani ya jingo hilo kukabiliana na magaidi wenye silaha au hata mabomu.
Je endapo sehemu walofikia hawa askari maalum wa KDF pangekuwa napo pamewekwa bomu jingine je, askari hao si wangepotea Maisha?
Suali la pili, je wenzetu wao wana umbali gani rasmi wa kujiokoa yaani "bomb evacuation assembly point" kutoka eneo la tukio maana sehemu nyingi ni mita kuanzia 400 na kuendelea?
Angalizo:
Nimeuliza tu suali naomba radhi kama nitawakzwaza ndugu zetu na majirani zetu wakenya.