Hiki kisasi ni kibokoooo!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hiki kisasi ni kibokoooo!!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Chipyopyo, Jun 5, 2010.

 1. C

  Chipyopyo Member

  #1
  Jun 5, 2010
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF
  Muoneni huyu dada ambaye alianza kusema hivi:

  Sikia Chip, wewe unanifamu long time na mahusiano yetu kwa kiwango kikubwa unayafahamu. Sijamkosea Josh wala kumfanyia hiyana yoyote ile, hata yeye mwenyewe hajanikosea hata siku moja.

  Josh ananijua tangu sekondari na hata nilipomaliza shule na matokeo kuwa mabaya ni yeye alinipeleka chuo akisaidiana na wazazi wangu hadi nikamaliza ngazi ya cheti.

  Pia diploma ni yeye ndiye aliyefanya kazi kubwa mpaka nikamaliza na akanishauri niende kusoma shahada kabla ya kuanza kazi nikaona ni jambo jema.

  Nikaprocess chuo nikapata huku Dar na kwa kuwa nilibahatika kupata mkopo full niliona nisimsumbue kuhusu fedha na hasa kwakuwa alikuwa amekwisha introduce swala la ndoa, nikaona nimpe nafasi ya kujipanga vizuri.

  Kinachoniuma hadi leo hii ni kuwa kilitokea kidudu mtu kikavunja penzi langu ghafla na wakafunga ndoa na mpenzi wangu Josh ambaye nilitaraji aje kuwa mume wangu mpendwa. Tukio hili sielewi lipangwa muda mrefu au limetokea ghafla mana tulikuwa bado tupo close sana mpaka nilipokuja ambiwa kuwa mwenzio anaoa sikuamini na sijaamini bado.

  Sasa basi, kwa kuwa bado nampenda mpenzi wangu na najua na yeye bado ananipenda na isitoshe yeye ndiye aliyefanikisha kunifikisha hapa nilipo ambapo ndiyo ninamalizia degree yangu ya kwanza this June.

  Ni hivi nikitoka hapa (kumaliza chuo), nahakikisha naivunjiliako mbali ile ndoa na kisha naolewa mimi, Josh anajua kupenda, anajua kutunza, anajua kubembeleza, anajua kitandani unahitaji nini pia ni mwaminifu saana thus why naamini labda kashinikizwa kuoa haraka au kuna mchezo wa giza kachezewa. So! Nina sababu gani ya kumpoteza? Kama ni huruma kwa nini huyo mwanamke mwenzangu asingenionea mimi huruma kwani anatujua vizuri saaana.

  Josh bado ananipenda thus why haishi kunijulia hali na pindi ninapokutana nae akiwa na huyo mkewe wa sasa huwa anshtuka na kufadhaika sana, zaidi ya yote anaonekana kuijutia hiyo ndoa ingawa anashindwa kuongea kwani amepungua sana na inaonekana hawaelewani vyema na mkewe.

  Ni lazima Josh aje kuwa mume wangu, kanitoa usichana, sijamjua mwingine till now na sihitaji kumjua yeyote zaidi ya Josh

  Tujaribu kumshauri jamani.
   
 2. futikamba

  futikamba JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2010
  Joined: Jan 18, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Oh hooo.... wajanja wamemuwahi??
  Ajifanye 'Da Sophy' tu, atafaidi kiulaiiini.
  Duh! Ila namuonea hurumaa..... maskini. Lakini wanaume nini kinawaingia mpaka kuwatenda wenzenu kiasi hiki? GADEEEM! Ah!
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Huyu dada ni m.pumbavu.

  Yaani baada ya kumaliza chuo kufikiria utaishi vp na kuyakabili vp maisha ..ati anapanga kuvunja ndoa ya mwanamke mwenzake? Mhh..

  Ngoja atolewe kilema cha maisha labda atatia akili.
   
 4. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  utavunja ndoa hiyo, halafu uyo mwanamke atakupiga bom hilo litakalokufanya maisha yako na elimu yako yote usiifaidi, ulishawai kuwa kilema wewe.....we cheza na ndoa za watu tu...wivu wa ndoa una nguvu kama nyuklia dadangu...utajajilaumu sana.
   
 5. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Tatizo tunaangalia sana hizi tamthiliya elfu kidogo zinazoonyeshwa na vituo vyetu vya runinga!
   
 6. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,427
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwa sababu mawasiliano kati yake na Josh bado yanaendelea suala la msingi akimaliza chuo aendelee na taratibu nyingine za kimaisha km kutafuta kazi au masomo zaidi. Iwapo kuna dili chafu ilichezwa na huyo mke wake wa sasa itajulikana tu na Josh atatambua ukweli na kurudisha penzi lake kwako. Iwapo Josh mwenyewe na huyo mke wake ndo wamecheza huo Mungu atamlipia na atapata mume mwema. Kumbuka ubaya haulipwi kwa ubaya. Thats the way it is!
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ndoa hailazimishwi, ndoa inapangwa na Mungu mwenyewe. Sikuzote likuepukalo halina kheri na wewe huenda kuwa hamjaowana na jamaa ikawa ni kheri yako, huwezi juwa kesho inakuwaje, kama ulivyokuwa hujuwi hatima yako na mwenzako ingekuwaje. Inawezekana ukitulia na kuwa na subira mkaowana bila kutarajia imekuwaje. Hakuna haja ya kufanya kisasi na bilisi mkaja kuumizana bure, hila hazifawi kwa wenye nia njema na busara, siku zote mpanda hila huvuna majanga.
   
 8. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nadhani ni muhimu huyo binti akubali matokeo na ku-move on na maisha yake...;pia ni muhimu atambue kwamba life has got twists, bends, surprises etc which you are axpected to face one way or another...
  Let her pull herself together and tread on...;it is not the end of the world after all... :painkiller:
   
 9. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Una kila sababu ya kuvunja hiyo ndoa, tena uwahi mapema kabla hajazaa nae, but think before you act, its fatal, ni dhambi!
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ati?

  Ngoja amwagiwe tindikali usoni tuone kama Josh ataendelea 'kumpenda' na 'kumjali'..he he he..
   
 11. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #11
  Jun 5, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,122
  Trophy Points: 280
  ...........ukitaka kumfaidi Josh wako kwa muda mrefu,we mtafute muwe mnakula nae uroda...najua hawezi kukataaa!!!! ikibidi hata beba mimba yake kwa ukumbusho lakini usivunje ndoa yake!
   
 12. Bourgeoisie

  Bourgeoisie JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Acha dada acha kabisa kulipiza kisasi kama hiki! Ndiyo tunajua kuwa wanaume ni wachache lkn naamini ukitulia Mungu atakupa aliyekuwa bora zaidi kuliko huyo Josh. Ifahamike pia mwanaume anaweza kuyajenga mapenzi ambayo hayakuwa moyoni hata baada ya kumuona tu mwanamke, hivo ucjidanganye kuwa hampendi huyo mkewe. Angalia upande wa pili wa shilingi ili usiyakose yote (Mume na elimu):target:
   
 13. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,813
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Mimi nilifikiri huyu dada atashukuru kuwa Josh alikuwa malaika aliyeletwa kwakwe ili amsomeshe na sio ili awe mume wake!
   
 14. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ushauri mwingine kama wa pepo vile!
   
 15. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Swali ni kwamba.... Alikuwa anampenda au alikuwa anamuonea huruma??
   
 16. Zneba

  Zneba Senior Member

  #16
  Jun 7, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umenifanya nicheke saana
   
 17. R

  Ramos JF-Expert Member

  #17
  Jun 7, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huyu dada sio "marriage material". bila shaka ni "simple sex material". Anaweza kuendelea kutoa huduma kwa jamaa, if he needs it anyway...
   
 18. Fab

  Fab JF-Expert Member

  #18
  Jun 7, 2010
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 763
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivi wife material na asiye wife material inakuwaje???nini tofauti yake?
   
 19. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #19
  Jun 7, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  People mna mioyo nyinyi????

  Sioni tatizo la huyu dada.....

  All is fair in love and war............
   
 20. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #20
  Jun 8, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Aaachane na mawazo ya kuvunja ndoa ya mwenzake, nae ajipange kimaisha na atapata mtu mwingine atakayempenda zaidi ya huyo Josh.
   
Loading...