Hiki kinachoendelea nchini tanzania hivi sasa ni utabili wa mwalimu nyerere wa mwaka 1995. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hiki kinachoendelea nchini tanzania hivi sasa ni utabili wa mwalimu nyerere wa mwaka 1995.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makongoromusa, Sep 6, 2012.

 1. makongoromusa

  makongoromusa Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwaka 1995 wakati CCM wanapendekeza jina la mgombe urais kupitia chama chao, Hayati Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere alialikwa katika mkutano ule kwa lengo la kusaidia upitishwaji wa jina lile. Katika hotuba yake Mwalimu aliwaonya wajumbe wa mkutano ule juu ya upitishwaji wa jina ambalo halitakuwa na sifa ya kutatua matatizo kwa watanzania yakiwamo ya rushwa,udini,ukabila na mengineyo aliyoyataja. Mwalimu alitoa picha ya hali ya siasa Tanzania kwa mwaka ule na siku za usoni hasa ndani ya CCM. Aliwaasa wajumbe wa mkutano kwa kuwaambia kwamba wakati wa kupitisha jina usiwe wa mizengwe akiwa na hofu juu ya uelewa wa mambo kwa watanzania waliowengi wakati huo 1995 na mfumo wa vyama vingi kwa chama chake.Nanukuu sehemu ya utabiri wa mwalimu juu ya kinachoendelea hivi sasa nchini mwetu,mwalimu aliwaambia wajumbe wa mkutano ule hivi: MTUTEULIE MGOMBEA ATAEKIDHI MATARAJIO YA WATANZANIA NA ANAEJUA HASWA MATATIZO YAO,WATANZANIA WANATAKA MABADILIKO,WASIPOYAONA NDANI YA CCM WATAYATAFUTA NJE YA CCM.Mwisho wa kunukuu. Ndugu zangu watanzania hakika hiki kinachoendelea hivi sasa ni kuelekea kutimia kwa utabiri wa baba wa taifa. CCM kama kawaida yao wamekuwa wakipuuza mambo mengi na hatimae sasa wanatumia nguvu kuhakikisha wanabaki madarakani,UBWANYENYE WAO NA UMANGIMEZA WAO SASA UNAWAPONZA...WATANZANIA WOTE TUTULIE TUUNGANE PAMOJA...HUU NI WAKATI WA MABADILIKO.
   
 2. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kama wanavyoona tumeamua kuyatafuta nje ya gamba
   
 3. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Hapo kwenye red ccm, pamoja na kuwa na viongozi maprofesa bado hawajapata akili ya kupatazama. wanatumia nguvu nyingi kufanya ujinga wakidhani watanzania hawana akili ya kufikiria hatma yao. lazima waachie dola, IMESHAWASHINDA.


  Tuendeleeni kuwaelimisha watanzania, waelimike ili waling'oe madarakani hili li serikali la ccm MAONGO/MAFISADI/MAJAMBAZI/WAUAJI.
   
 4. k

  kingo2012 New Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 30, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naomba mungu tufikike 2015 hao magamba waone utabiri wa mwalimu ukitimia sipati picha
   
Loading...