Hiki kinachoendelea nchini tanzania hivi sasa ni utabili wa mwalimu nyerere wa mwaka 1995. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hiki kinachoendelea nchini tanzania hivi sasa ni utabili wa mwalimu nyerere wa mwaka 1995.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by makongoromusa, Sep 6, 2012.

 1. makongoromusa

  makongoromusa Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwaka 1995 wakati CCM wakipendekeza jina la mgombea urais kupitia tiketi ya chama hicho katika mkutano wao mjini dodoma,marehemu baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,alionya juu ya kupendekeza jina ambalo halitakuwa na mvuto kwa wananchi na pia ambalo halita maliza kiu ya matatizo ya watanzania wakati huo akiwa na hofu ya kwamba sasa watanzania wamebadilika(yaani 1995).

  Mwalimu Nyerere alisema kwamba,nchi yetu kwa sasa(yaani 1995) ina matatizo mengi ambayo utatuzi wake utategemea mtu mwenye uwezo wa kuayatatua akawaomba wajumbe wa ule mkutano kwamba wasifanye makosa kuteua jina la mtu ambaye atainyima sifa CCM za kuendelea kuongoza nchi katika siku za usoni....Napenda kunukuu sehemu yenye utabiri juu ya haya yanayoendelea sasa Tanzania: "WATANZANIA WANATAKA MABADILIKO,WASIPOYAONA NDANI YA CCM WATAYATAFUTA NJE YA CCM"...mwisho wa kunukuu.

  Tukumbuke kwamba maneneo haya aliyasema mwaka 1995 kwa maana kwamba alishaona uelekeo wa siasa hasa ndani ya CCM...lakini kutokana na umangimeza na ubwanyenye wa CHAMA CHA MAPINDUZI,viongozi wake wameyapuuza maneno haya na sasa tunashuhudia UTABIRI WA MWALIMU nyerere ukitimia....TUWE WATULIVU, HUU NI WAKATI WA MABADILIKO TUUNGANE WOTE.
   
Loading...