Hiki kiburi, jeuri na dharau Prof. Kitila Mkumbo nguvu anaipata wapi

Mjenga Nchi

Member
Apr 21, 2020
6
19
Hivi majuzi, Katibu wa Siasa na Itikadi Ndg Humphrey Polepole, Kwa niaba ya Chama aliongea na wandishi wa habari Kama mlivyomsikia alisema,

1) Wale wasaka Ubunge wanaovuruga majimbo ya CCM hawatateuliwa maana ni walafi wa madaraka.

2) Wale walioteuliwa na Rais katika majukumu mbalimbali mfano makatibu wakuu wa Wizara, Ma RAS, DC Ma DAS, wanaojiingiza kusaka Ubunge kiama kinawasubiria.

3) Wale wanaosaka Ubunge kwa kusema wametumwa na Rais NI waongo.
Sasa swali langu Prof KITILA ni Moja ya walioanza kampeni mapema, sauti zipo CCM na video.

NI moja ya walioteuliwa na Rais lakini akaona ukatibu mkuu Wizara ya maji haufai na haumtoshi, Ni moja ya waliotumia Sana Lugha ya kwamba wao wametumwa na Rais. Amepuuza tamko la Polepole.

Majuzi alikutana na wajumbe wa kata ya Kinampanda na kuwapa elfu 50 kila mmoja, Jumamosi alikutana saa kumi na Mbili Jioni na wajumbe wa kata ya Mukulu na kuwagawia elfu 20 kila mmoja.

Chama kina taarifa na vyombo vingine vya serikali vinataarifa. Nilikwepo katika kikao chake, akiongea nasi alisema, (audio ipo na wala siyo siri)

1) Amesikitishwa sana na kushanganzwa Sana na JIWE kumteua Mwigulu na

2)kwamba hababaishwi na uteuzi huo

3) Anawambia wajumbe wampe kura nyingi mpaka aliemteua Mwigulu apate aibu.

Swali ambalo inabidi tujiulize mimi na wewe huyu kama anakaidi viongozi wetu wa chama sasa hicho kiburi anakitoa wapi?

Je, kukiuka hivi haya maelekezo, DHARAU hizi na kiburi hiki ni maandalizi ya kurudi Upinzani?

Prof. Kitila kuwa makini huenda ulizoea staili yako ya kiuhanaharakati katika vyama vya upinzani huku ni tofauti maana tunafuata misingi na katiba ya chama chetu.
 
Ndio mtajua faida ya kuwa na mfumo huru wa vyama vingi ,demokrasia ya kweli ya kati nchi na tume huru, vinginevyo wote mtategemea kupata ubunge na udiwani kupitia chama kimoja kwa kuongozwa na matakwa ya mtu mmoja anaeamua nani apitishwe na nani atangzawe mshindi

Kukiwa na demokrasia ya kweli, hakuna haja ya watu kuwa watumwa wa vyama vya siasa hasa chama kilichoshika dola bali hata mgombea binafsi angetosha kusimama yeye kama yeye.

Wacha na wengine waendelee kuhamia alafu tuone kama wote watapata fursa za kugombea au kupewa vyeo baada ya uchaguzi.
 
Hata huku Same mashariki kuna mzee anaitwa Mashafii Anapita akiwa na baadhi ya Makatibu kata wa CCM wakijinadi na kumchafua Mama Anne kilango kua hafai ,Naomba chama changu cha CCM hao ambao wameanza kujinadi wakatwe mapema maana wanatumia hela kutafuta ubunge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Prof Mjanja Mjanja mache aendlee na tabia zake ukisikiliza ile hotuba ya Comrade Polepole ina muhusu 100%, Kama ni Mimi hata form ya Ubunge sitachukua unaweza jikuta unakosa vyote, Hawakukosea waliosema mtaka mtaka mbili kwa pupa………
 
Kiongozi hicho kikao Cha Kinampanda labda zilifa nyika kwa Video Conference ..
.hapa kwetu tungewakamata tu!
 
Wanakulana

Jr

Tatizo ni kwamba Kitila yupo na mpishi na huyu jamaa yetu naye anategemea senti za magae kuwapa ili wamrudishe lakini ukiongea na majority wengi wanamtaka Kitila na pesa wanavuta kotekote
 
Tuache hizi siasa za majitaka. Nina miaka zaidi ya mitano sijawahi kufika Kinampanda. Tafadhali sana
Inawezekana hujafika Kinampanda, ila ukawa umefika Ulemo, Shelui, Kiomboi, na maeneo mengine ya jimbo hilo kufanya haya yaliyosemwa na Mjenga Nchi

Ila yote heri tu, maana wote ninyi ni wanaIramba na wote wawili pamoja na chama chetu CCM tumeshiriki kuua Upinzani kwa njia katili kabisa.

Basi ni vema upinzani huu ukiingia na kukua ndani ya chama chetu ili nasi tuone umuhimu wa kuvumiliana katika minyukano ya kisiasa ila kwa hoja!
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom