Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Nijuavyo mimi, miongoni mwa shabaha kuu za kuwa na vyama vya wana-taaluma ni kuwa na mfumo dhabiti wa kuhakikisha kuwa wana-taaluma husika, wanaendesha shughuli zao kwa kuzingatia "professional conduct" ya taaluma zao. Na hivyo sikutegemea kwamba chama cha wanasheria nchini kingeliendelea kuwa kimya wakati umma wa watanzania unaendelea kutoa kilio chao kuhusiana na nchi kuendelea kuporwa raslimali yake kutokana na mikataba mibovu inayoandaliwa na wanachama wake, kwa kwenda kinyuma na maadili ya taalima yao. Mimi naamini chama hicho kingelikuwa kinachukua hatua dhabiti ya kuwaadamisha watu hao nchi yetu isingelifikia hatua hii. Chukua ili sakata la hivi sasa la TANESCO kubwagwa na huyu mridhi wa Richmond, Watanzania hawajui ni nana wakumwamini; waziri mwenye dhamana anautupia mpira TANESCO, wakati akijua ya kuwa walikuwa wanaendesha kesi si TANESCO bali serikali yenyewe kupitia kwa mwanasheria mkuu wa serikali. Mkanganyiko huo umesababisha watu wengi kuanza kuwa na hisia kwamba uenda kushindwa kwa TANESCO kumetokana na njama za wanasheria walio liwakilisha shirika hilo kutoa kwa makusudi utetezi hafifu kwa maslahi binafsi. Katika hali hiyo sauti pekee ambayo ingeliwaondolea shaka watanzania kwa jambo hilo, ni chama cha wanasheria nchini. Rai yangu kwa chama hicho; chonde chonde, msikae kimya wakati watu wengi wa nchi hii wanaamini kwa dhati, ya kwamba dhiki walionayo imachangiwa na wana-taaluma wenu.