Hiki chama cha wanasheria nchini kinasaidiaje ustawi wa nchi yetu?

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
0
Nijuavyo mimi, miongoni mwa shabaha kuu za kuwa na vyama vya wana-taaluma ni kuwa na mfumo dhabiti wa kuhakikisha kuwa wana-taaluma husika, wanaendesha shughuli zao kwa kuzingatia "professional conduct" ya taaluma zao. Na hivyo sikutegemea kwamba chama cha wanasheria nchini kingeliendelea kuwa kimya wakati umma wa watanzania unaendelea kutoa kilio chao kuhusiana na nchi kuendelea kuporwa raslimali yake kutokana na mikataba mibovu inayoandaliwa na wanachama wake, kwa kwenda kinyuma na maadili ya taalima yao. Mimi naamini chama hicho kingelikuwa kinachukua hatua dhabiti ya kuwaadamisha watu hao nchi yetu isingelifikia hatua hii. Chukua ili sakata la hivi sasa la TANESCO kubwagwa na huyu mridhi wa Richmond, Watanzania hawajui ni nana wakumwamini; waziri mwenye dhamana anautupia mpira TANESCO, wakati akijua ya kuwa walikuwa wanaendesha kesi si TANESCO bali serikali yenyewe kupitia kwa mwanasheria mkuu wa serikali. Mkanganyiko huo umesababisha watu wengi kuanza kuwa na hisia kwamba uenda kushindwa kwa TANESCO kumetokana na njama za wanasheria walio liwakilisha shirika hilo kutoa kwa makusudi utetezi hafifu kwa maslahi binafsi. Katika hali hiyo sauti pekee ambayo ingeliwaondolea shaka watanzania kwa jambo hilo, ni chama cha wanasheria nchini. Rai yangu kwa chama hicho; chonde chonde, msikae kimya wakati watu wengi wa nchi hii wanaamini kwa dhati, ya kwamba dhiki walionayo imachangiwa na wana-taaluma wenu.
 

MWANALUGALI

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
601
0
Hawa wanaoongozwa na Kibodya aliyemuunga mkono waziri wa Sheria na katiba kuwa hakuna fedha kwa ajili ya kuandika katiba mpya???? hawa si wanasheria ila ni wanasiasa uchwara wa sheria!!!!
 

menda

Member
Oct 15, 2010
8
20
Jukumu la kusaidia ustawi wa jamii ya nchi yetu tungetegemea chama cha wanasheria kiwe mbele kwa hilo, hata hivyo vyama vingine vya wanataaluma wana jukumu sawa kusaidia ustawi wa taifa letu.Kimya cha wanasheria na vyama vingine vya wanataaluma kukaa kimya wakati mambo yanaenda sivyo ni aibu kwa wanataaluma wote! Wakati umefika sasa kwa kusimama kidete kukemea mambo yote yanayopelekea taifa hili kuangamia ! Tusipoziba ufa leo kesho tuta...
 

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
4,560
2,000
Ni kweli taaluma zote zijitokeze kuweka pressure na umma utapata kujiamini, kwa sasa jukumu limeachwa kwa vijana ambao wanapakaziwa kuwa ni wahuni na wafanya fujo

Vijana ndiyo wameachiwa kazi ya kukesha na kulinda kura, kuandamana pale panapohitajika na kupigwa virungu pale dola inapoamua kufanya hivyo.
Kwa ujumla vijana wamekuwa jalala.
Iwapo sauti ya wataaluma ikisikika hatutasikia virungu wala maandamano, maombi ya katiba yatasikilizwa, tume huru tutapata na mengine yote kwa njia ya kistaarabu na hata kulinda kura hakutakuwepo.

Ni vema sasa wanataaluma wapaze sauti, kwani bila katiba mpya nchi itaendelea kuongozwa na RA, EL na wengine wasiozidi 10. Hawa wataendelea kutuchagulia serikali na wakereketwa wa CCM watatumika kukamilisha kivuli cha demokrasia na hivyo dunia itadanganywa kwamba uchaguzi huru na haki.WANATAALUMA TUAMKE SI WANASHERIA PEKEE
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom